Kauli mbalimbali za Waziri Mkuu kuhusu mgomo wa madaktari!

Naibili

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,730
519
kauli za mh. waziri mkuu
“Jambo hili ni la Rais. Hivi ifike mahali tumpe Rais saa 72 kwa sababu eti umebeba maisha ya watu? Mimi hilo siliafiki hata Rais hawezi kuliafiki. Hata angekuwa mtu yeyote asingekubali. Siwezi kumwambia Rais atekeleze hilo,” alisema Pinda. (hapo kwenye bluu waziri mkuu anamaanisha hata alipowaahidi madaktari kwenye mgomo wa kwanza kuwa swala la mawaziri wa afya lipo kwa rais alidanganya umma!, basi kama waziri mkuu alishalipeleka kwa rais ilikuwa ni suala la kumuuliza mh umeamuaje, tuwaambie nini madaktari au katika taarifa yake kwa vyombo vya habari angetoa taarifa nini kinachoendelea.)

“Haya matatizo ni ya muda mrefu. Dk. Mponda maskini ana mwaka mmoja na kidogo. Baba wa watu wa mwaka mmoja ndio imekuwa issue kweli? Turudi tufanye mazungumzo,” alisema Pinda.
(hapa waziri mkuu anamaanisha waziri wa afya hawezi kujiuzuru sasa mazungumzo ya nini?)

“Kama madaktari wana dhamira nyingine fine (sawa).”

“Ngoja tuone kwanza, itakapotokea tutaona nini la kufanya.”
(waziri mkuu ameona kuruhusu mgomo wa madaktari ni jambo la mwisho mpaka watu waanze kufa ndo wataona nini cha kufanya au mpaka wananchi walalamike ndo wataona nini cha kufanya)

mwisho kauli ya madaktari

"Sisi hatujabadilisha maamuzi yoyote msimamo wetu uko pale pale wa kuweka vifaa chini na hakuna mazungumzo yaliyofanyika na ofisi ya waziri mkuu tangu tulivyotoa tamko letu mpaka sasa na ndio maana tunasema mgomo unaanza kesho (leo) na hivi tunavyozungumza madaktari wanajiandaa," alisema
 
walimpa mwezi mzima akajua wameshasahau. yaani mwezi mzima anauona kama masaa 72!? hahahaaaaa...!!. Bora kufa umesimama kuliko kuishi umepiga magoti.
 
Tatizo lililopo ni Systemic. Serikali yote imekuwa legelege mno. Usanii, udanganyifu na siasa zisizo na tija. Sasa serikali haina hela, inauza dhamana kwa kasi kwenye mabenki. Tutafika wapi?
 
Tatizo lililopo ni Systemic. Serikali yote imekuwa legelege mno. Usanii, udanganyifu na siasa zisizo na tija. Sasa serikali haina hela, inauza dhamana kwa kasi kwenye mabenki. Tutafika wapi?

mKUU naomba unielimishe dhamana za serikali imekaaje??
 
Kama mh pind anasema tatizo si mponda na nkya kwa nini asijiudhuru yeye.anasema hawa watu wameingia wizarani ndan ya mwaka 1. Kwa nin hawakuyaona haya yanayotokea.kwanini walitumia siasa wakti jambo lenyewe liliitaj hekima,busara na taratibu za utumishi.kama haya yote yameshndikana acha madaktari wagome ili iwe fundisho kwa pinda na bosi wake wanaosema uongo. Wanaouguza pole ila mungu atajaria tuvuke kipind kibaya hiki
 
kauli za mh. waziri mkuu
“Jambo hili ni la Rais. Hivi ifike mahali tumpe Rais saa 72 kwa sababu eti umebeba maisha ya watu? Mimi hilo siliafiki hata Rais hawezi kuliafiki. Hata angekuwa mtu yeyote asingekubali. Siwezi kumwambia Rais atekeleze hilo,” alisema Pinda. (hapo kwenye bluu waziri mkuu anamaanisha hata alipowaahidi madaktari kwenye mgomo wa kwanza kuwa swala la mawaziri wa afya lipo kwa rais alidanganya umma!, basi kama waziri mkuu alishalipeleka kwa rais ilikuwa ni suala la kumuuliza mh umeamuaje, tuwaambie nini madaktari au katika taarifa yake kwa vyombo vya habari angetoa taarifa nini kinachoendelea.)

Hapo kwenye blue naona MP kashemka. Kama ana msmamo na anasimamia kile anachoamini alitakiwa amshauri Rais na kama Rais angekataa then angejiuzuru............. Ndiyo wenzake ambao wako serious wanavyofanya!! Siyo kusubiri wafukuzwe au walazimishwe kuachia ngazi!!
 
It is a shame to our Country having a PM who doesn't understand his obligations!!
 
JK anatakiwa kuteua waziri mkuu mwingine.
JK hana waziri mkuu kwa sasa.
Nchi haina waziri mkuu kwa sasa.
Nchi inahitaji waziri mkuu kwa mujibu wa katiba.
kwani Pindi ni waziri mkuu kwa jina tuu.
Pinda ni waziri kivuli.
Pinda haiwezi kazi ya uwaziri mkuu, ni hovyo kabisa.
My take: Sija wahi kuona waziri mkuu hovyo hapa TZ kama Pinda.
 
Tanzania inajiongoza yenyewe,wanaojiita viongozi wanajali maslahi ya kisiasa zaidi.Nasikia hivi sasa wanapeleka askali Arumeru kwenda kunyanyasa raia,hapo fedha wanazo,lakini wagonjwa wafe, ifike wakati watanzania tuwaambie hapana inatosha
 
Amenishangaza alipokiri kwa kusema "haya matatizo ni ya muda mrefu....."

Kwa hiyo madaktari wana haki ya kugoma kwa kuwa ni ya muda mrefu na hayashughulikiwi.
 
Back
Top Bottom