jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,375
- 25,453
Wanajamvi,
Kauli za wakuu wa nchi ni nzito sana!Na huwa kauli zozote wanazozitoa, huwa zinachukuliwa kwa uzito wa juu. Iwe ni kutamka kwa mdomo, ama hata kupitia mtandao mfano twitter.
Kwa kiasi kikubwa, kauli ambazo wanazizingumza, huwa zinachukuliwa hatua kwa namna moja ama nyingine. Kutegemeana na mazingira, yaweza kuwa vyombo vya usalama, ama makundi ya “vigilantes”(watu wa kujitolea). Rais Trump na pia Maghufuli, kuna kauli ambazo kwa maoni yangu zitawacost. Pia niseme kuwa kwa kiasi Fulani nakubaliana na baadhi ya washabiki wa Magufuli wanaomfananisha na Trump kweye huo upande wa uzungumzaji! Yani wanasema wanachojisikia kusema wakati wowote mahali popote bila kujali chochote. Trump yeye huwa ni mubashara pamoja na twitter!
Trump kama ilivyo kwa Maghufuli, alizungumza na mara nyingine kwa namna ambayo wanasema ni kwa kutumia “codes”. Yani ikiwa na maana ya kiongozi kuzungumza kwa namna ambayo anataka jambo flani lifanyike, lakini bila ya kusema moja kwa moja. Kwa wamarekani, wale mabosi wa mafia ndiyo walikuwa vinara wa kutumia lugha hizo za codes, pale ambapo wanataka mtu flani auwawe ama kazi flani ifanyike nk.
Trump yuko matatani sana, lakini sitaki kuzungumzia matatizo yake ambayo hayaendani na mustakabali wa dhana ama hoja ya bandiko hili.
Mwanasheria binafsi wa Trump ambaye alifanya naye kazi kwa miaka takriban kumi, alisema kuwa Trump alimuagiza amlipe muigizaji wa filamu za ngono, anayeitwa Stormy Daniels, ambaye Trump aliwahi kuwa na mahusiano naye ya kimapenzi wakati akiwa ameoa na mke wake akiwa amejifungua motto wao wa kiume aitwaye Baron. Baada ya huyo mwanasheria wake anayeitwa Michael Cohen kumalizana na mwanasheria wa porn star,pamoja na gazeti la the enquirer, Trump alimwandikia mwanasheria wake cheki kadhaa kwa malipo ya mikupuo minne, ili ioneane kama vile alikuwa akimlipa malipo ya kazi zake.(retention fees). Lakini kumbe ni malipo ambayo walikubaliana ya jumla ya usd 130,000/=. Michael Cohen alitoa ushahidi wake kwenye congress, na alikuja hadi na copy ya cheque ambayo Trump alimuandikia akiwa tayari ni rais na ina saini yake!
Mojawapo ya cheki ambazo rais Trump alimuandikia Michael Cohen kwenye malipo ya kwenda kwa kuigizaji wa filamu za ngono ambaye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Trump. Malipo yalikuwa ni ya kumfunga mdomo huyo mwigizaji pamoja na kulilipa gazeti lile ili kuweza kuinunuwa habari ile kisha kuizika. Cheki hii aliiandika baada ya kuwa rais. Hakumwambia mwanasheria wake moja kwa moja nini kifanyike, bali alitoa kauli za kulalamika na kutokufurahishwa na suala hilo. Hiyo ikawa ni kama amri ya kuwa lishughulikiwe ili lisije kumuharibia mbio za urais. Ikawa ni habari ambayo waliinunuwa kisha wakaizika. Gazeti la "The enquirer" pia linahusika. Gazeti ambalo lilitumika sana na Trump kwa propaganda na kashfa za uongo dhidi ya wapinzani wake. Ni kama ilivyo Tanzanite ya Musiba na Musiba mwenyewe. Ila bosi wa enquirer yeye yuko matatani huko mbele kwasababu demokrasia inafanya kazi.
Pia Trump aliwahi kutamka kuwa anawataka warusi wamsaidie kuzileta email za mgombea wa Democrats! Na haikupita muda, warusi wakatimiza matakwa yake. Hayo yako kwenye uchunguzi hadi sasa. Na kauli yake ni mojawapo ya ushahidi unaotumika dhidi yake na pia iliyopelekea uchunguzi unaoendelea. Pia amekuwa akisema “no collusion” kila mara, na kumsema vibaya yule Mueller!Hizo kauli zake sasa zinachukuliwa kama “obstruction of justice”, na pia ndizo zinasemekana kuwa alimtimuwa yule mkuu wa idara ya FBI, kwasababu alitaka issue ya uchunguzi wa Russia kumsaidia kwenye uchaguzi izikwe na uchunguzi ufe. Kwahiyo hizo kauli zake zinawapa wakati mgumu viongozi aliowateuwa, na hii ni kwasababu ni taifa la demokrasia! Kuna yule aliyekuwa mwanasheria mkuu anayeitwa Jeff Sessions, ambaye Trumo alimfukuza kazi. Na alikuwa akilalamika kwasababu aliji “recuse” kuhusiana na uchunguzi wa Mueller. Hiyo ina maana kuwa hataweza kuitumia nafasi yake ya uanasheria mkuu kumlinda Trump na maovu yake!
Mifano ya kauli za Trump zitakazomponza ni mingi tu, ukifuatilia yale mahojiano ya Michael Cohen kwenye congress, utagundua hilo.
Mifano ya Maghufuli
Kwa upande wa rais Maghufuli, kwanza kabisa ni kauli yake ya kuhusu “usaliti”, ambapo alikuwa akimrefer Tundu Lissu kama msaliti, kasha akasema ni msaliti wa nyakati za “vita ya kiuchumi”, msaliti dawa yake ni kuuwawa! Haukupita muda, Lissu akashambuliwa kwenye jaribio la kutaka kumuuwa!
Rais Maghufuli pia alisema “I wish I could be IGP”, ambapo ni kama vile alimaanisha kwamba IGP hafanyi kazi inavyotakiwa. Na ni kwasababu wale waliotuhumiwa na Makonda kuwa wanauza madawa ya kulevya, wakati ule pale central akiwa Gwajima pamoja na yule Yusuph Manji, ambapo yeye gari lake lilioshwa, na wale wanakwaya wa Gwajima wakawa wanaimba pale nje! Mh rais alichukizwa kabisa kuwa kwanini wale wananchi waliruhusiwa kufanya yale. Lakini ukweli ni kwamba hawakuvunja sheria yoyote ile ya nchi. Bali rais alitaka wawe wanyama zaidi. Matokeo yake, mkuu wa mkoa wa Dar kwa kutumia rungu lake la “mwenyekiti wa kamati ya usalama ya mkoa”, akaanza kumuendesha Mambosasa. Nadhani alipata sana uchungu baba yake aliposema yale maneno. Kama makonda huyu huyu ndo yule aliyekuwa mpambe wa Rizmoko, hadi akafuta viatu vyake ama sijui kufunga kamba hadharani, hakuna ajuaye anachokifanya anapokuwa haonekani. Pengine ni mtu hatari sana. Hakuna jambo lolote linalotokea ama kuhusishwa kwa Maghufuli nay eye hayumo. Lakini nilishangazwa na kauli ya rais kuwa “Mambosasa nawaona watanzania wajinga sana”, kuhusiana na ile issue ya kutekwa kwa Mo.
Hata ule uvamizi wa clouds ulianzia huko huko. Kumbuka kuwa ilikuwa ni nia ya Makonda kutaka kipindi kirushwe, ambacho kinahusu mwanamke ambaye anadaiwa kuzaa na Gwajima. Kwa kauli alizokuwa anazisema the late Ruge, utagunduwa alikuwa hataki hayo mambo. Sina uhakika kama walitaka kirushwe kwenye kipindi pendwa cha mh rais cha Shilawadu! Inavyosemekana, mkulu mwenyewe alishajipanga na popcorns kabisa! Ilipobuma, akamwambia “kijana piga kazi”!, baada ya kelele kuzidi, “akawapatanisha” kule Tanga ambapo walishikana mikono. Lakini baada ya hapo uahasama uliendelea kama kawaida. Kwenye ile press conference ya TEF wote tuliona.
Kama kuna wengine ambao mnakumbuka kauli ambazo zitawaponza hawa viongozi hao, ambao mashabiki wa rais Maghfuli wanapenda kuwafananisha, please share with us.
Rais Trump akiwa na Michael Cohen aliyekuwa mtu anayefahamu siri zote za Trump zile chafu!
Rais Maghufuli na Makonda, need I say more?
Hitimisho.
Tofauti iliyopo kati ya situation hizo mbili, ni kuwa marekani, “No one is above the law”

Mifano ya Trump.