KAULI 10 ZA KUPONGEZWA ZA IGP SIRRO.

KAULI 10 ZA KUPONGEZWA ZA IGP SIRRO.

moyafricatz

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2015
Posts
2,905
Reaction score
4,928
''Kumrudisha Mo na kutelekeza gari hili sio mwisho, Jeshi la polisi linaendelea na upelelezi, ninafahamu kati yao kuna mtanzania na tunataka tukiwapata tuongee lugha nzuri kuwa walikuwa wanataka nini'' - IGP Sirro

"Mohammed Dewji amesema watekaji hao walikuwa na wasiwasi sana, baada ya kuona hawawezi kutoka, njia pekee ni kuliacha hili gari hapa majira ya saa saba usiku, MO aliwapa taarifa wazazi wake wakaja kumchukua" - IGP Sirro.

"Nimepata taarifa kwamba waliomteka Mohammed Dewji amesema walimwambia wanataka pesa, alipowauliza shilingi ngapi hawakusema. Aliwapa simu waongee na baba yake lakini waliogopa kwa sababu wanafahamu ulinzi wetu ni imara tungewakamata." - IGP Sirro

''Wangechelewa tungewakamata na kuwakamata kwangu kungekuwa kwa tofauti, matukio haya yanapotokea yasitugawanye'' - IGP Sirro

''Kwenye gari tumekuta silaha za kivita kama AK47, 'Sub-machine gun' na Bastola 3. AK47 ikiwa na risasi 19 na risasi 16 za Bastola'' - IGP Sirro

''Kuna watu tu wachache wanajaribu kuvuruga kazi za jeshi la polisi na hatutawapa nafasi ya kufanya hivyo na sijui nia yao ni nini na wanatumwa nani kwa faida ya nani'' - IGP Sirro

"Kuna kikundi cha watu wachache wanajenga uadui na Jeshi la Polisi, kujenga uadui na majeshi yetu Polisi wakifanya kazi zao wanaingilia, ukijenga uadui na Polisi siku ya siku uje kulaumu" IGP Sirro

''Sikutaka kusema, lakini watu wetu wapo kwenye nchi zao wanafanya uchunguzi kwa kushirikiana na wenzetu wa Interpol na tunataka kuwaonyesha kuwa ukijaribu Tanzania sio sehemu sahihi labda wamezoea kwao huko'' - IGP Sirro

"Nyinyi ni mashahidi jana nimezungumzia hii press nikiwa na uhakika lakini kuna watu wachache ambao sijui nia yao ni nini?, tukijaribu kufanya wao wanatufundisha" IGP Sirro

''Hili gari walitaka kujaribu kutaka kulichoma ili wapoteze ushahidi lakini nadhani walikuwa na hofu juu ya hilo hawakufanikiwa'' - IGP Sirro. Watekaji walikuwa wanataka hela lkn hawakutaja kiasi IGP Sirro ....


Siku tisa askari wetu hawalali, wanazunguka apartment Moja na nyingne, usiku na mchana halafu Kuna mtu yupo chumbani kwake na mke wake, wanakiyoyozi lakini anatumia social media kuchallenge kazi za jeshi La polisi.
 
Siku tisa askari wetu hawalali, wanazunguka apartment Moja na nyingne, usiku na mchana halafu Kuna mtu yupo chumbani kwake na mke wake, wanakiyoyozi lakini anatumia social media kuchallenge kazi za jeshi La polisi.
Hivi Ku challenge au mtu kutoa mawazo yake kadri ya fikra zake ni kosa ? Nadhani busara kama wanaona ni wapuuzi ni kuwapuuza ila sio kutumia nguvu na muda kuwa entertain au kuwatisha...
 
427792_329517023813735_1060067675_n.jpg
 
Wacha niwe wa mwisho kuamini hii script iliofeli vibaya sana
 
Back
Top Bottom