angalia hata barabara zinajengwa huku huku pwani tu. mimi sijatoka western africa, maeneo nitokayo hayana shida kabisa ya usafiri. lakini huwa nashindwa kuelewa, kwanini western tz na maeneo ya north west yanadharaulika? Kigoma, central tz(singida,shinyanga etc), kagera,rukwa nk. pamoja na kusini. kama sio tz vile, cha ajabu, hata bajeti hutungwa kuwabagua watu wa huko. pamoja na kwamba maeneo yao yana resources nyingi ambazo kama tungekuwa makini kuweka pesa nyingi kwenye infrastructures huko, tungepiga hatua kuvuna utajiri wa huko. barabara mbovu pamoja na kwamba zingine zinapakana na nchi jirani ambao wangekuwa wateja wetu, reli ndo tumeuza kwa wahindi. bandari ya mtwara ingekuwa bomba, lakini wizi mtupu. nashindwa nisemeje kwakweli.