Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,694
- 149,920
Katika hali ya kawaida, tena kwa nchi zetu hizi za kiafrika zenye demokrasia changa,ni sahihi kweli kwa Bunge lenye kufuata mfumo wa vyama vingi kuwa na kanuni zinazoruhusu, Spika,naibu wake na wenyeviti wa Bunge wote watoke katika chama kimoja?
Licha ya sisi kama Taifa kuamua kuingia katika mfumo wa vyama vingi,bado kuna mambo mengi tu yanayoendana na mfumo wa chama kimoja likiwamo swala hili la Uongozi na Madaraka ya Bunge.
Ninaamini pia hata kanuni za Bunge zinapaswa kurekeshwa kutoruhusu wajumbe wa Kamati ya Haki,Kinga na Madaraka ya Bunge kutawaliwa na wabunge wa chama kimoja unless vyama vingine havina wabunge wa kutosha kuweza kuingia katika kamati hii ili iweze kutenda haki kwa wabunge wote na kuhakikisha Mhimili huu unakuwa na nguvu za kutosha na zaidi kutotawalia au kuingiliwa na Mihimili mingine kama vile serikali katika kutimiza na kusimamia majukumu yake kama Taasisi huru.
Ni wazi tumeingia katika mfumo wa vyama vingi huku chama tawala kikiwa hakina nia ya dhati ya kuona mfumo huu unastawi na kufanikwa hapa nchii na pengine tushukuru zaidi busara za Baba wa Taifa katika kutoa msukumo wa jambo hili.
Demokrasia ya Vyama Vingi hapa nchni bado ni kiini macho kwani wanaopaswa kuisimamia na kuiendeleza wengi wao ni wazee na bado wana mentality ya kizamani ya mfumo wa chama kimoja hasa wale wazee wa miaka ya 60 kurudi nyuma na vijana wachache wanaofaidkia / waliofaidika na mfumo huu kupitia wazazi wao,ndugu zao au jamaa zao walioko madarakani/waliowahi kushika madaraka ya nchi hii siku za nyuma.
The best solution ni Spika na Naibu wake wasitokane na chama cha siasa au watoke nje ya wabunge ingawa tatizo bado linaweza kuwepo maana bado tu watu wanaweza kupandikizwa.