Katika kuadhimisha miaka 40 ya CCM, je tunazingatia misingi ya maadili ya taifa?

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
TUKIWA TUNAADHIMISHA MIAKA 40 YA CCM.JE TUNAZINGATIA MISINGI YA MAADILI YA TAIFA?

Na Petro Magoti

*Maadili ni Taratibu*Kanuni na Sheria zilizokubalika ktk jamii zinazotumika kuongoza Mahusiano kati ya Makundi ya Watu na namna wanavyofanya mambo yao kwa kuzingatia misingi ya Utu na Haki.

Kanuni hizi huwa na taratibu zinazoainisha tabia na Mienendo inayokubalika na isiyokubalika katika jamii lakin lengo lake kuu ni Kufanya Kilicho Sahihi.Ndo Dhamira ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi.

Ili kupata radha kamali ya Maadili ya Kitaifa tujikumbushe nyuma kidogo.Mwalimu J.K.Nyerere alikuwa Mwanasiasa aliyeongoza Mapambano ya Ukombozi wa Nchi yetu Tanganyika enzi hizo na Baadaye Tanzania 1964.

Falsa ya Mwalimu Nyerere Ndiyo iliyozaa itikadi ya Kijamaa na Chama chetu na Maadili yake binafsi.

Maadili ya Mwalimu Nyerere yalijikita kwenye falsa ya Itikadi ya Chama chetu na Siyo vinginevyo.

Ni muhimu mnoo Kusisitiza jambo hili hasa katika nyakati hizi za Rushwa, Ufisadi, Madawa ya kulevya, Na hasa tunaileta CCM MPYA na Tanzania Mpya kuelekea ktk Uchaguzi Mkuu wa chama chetu Tawala CCM.

Ni Muhimu mnoo KusisitiA jambo hili hasa nyakati hizi kwa sababu wengi wnahubiri Maadili kama kwamba Maadili yanaweza kuelea JUU JUU bila kuwa na Mizizi katika Falsafa na Itikadi.

Msingi Mkuu wa Wa Falsafa ya Mwalimu ni USAWA wa Binadamu.Katika Chimbuko la Maadili ya Taifa, Inategemewa kuwa Matendo au Maamuzi ya Kimaadili ya Viongozi wa Umma na Jamii nzima yafuate Misingi fulani wakati wa kutimiza Majukumu yao ya kila siku.

Je tunapataje Misingi ya Maadili ya Taifa? *Ahadi kumi za TANU na Misingi minne ya Azimio la Arusha na Miiko ya yake ambapo kwa Pamoja ndiyo Misingi au Chimbuko la Maadili ya Taifa letu*.Misingi hiyo Iliasisiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K.Nyerere.

Misingi ya Maadili ya Taifa letu.

i) *Binadamu Wote ni Ndugu Zangu na Afrika ni Moja*
>Serikali ya Chama chetu CCM imeendelea Kueneza Upendo, Umoja Mshikamano na Udugu.Mh Rais na M/Kiti wa CCM Dr Magufuli Amekuwa akisisitiza Msingi wa Kujenga Amani, na Mshikamano na Umoja baina Ya mtu na Mtu, Familia, kwenye Koo, kaya hadi Ngazi ya Kimataifa.Ambapo Viongozi Chinj ya Serikali ya CCM hubeba dhamana ya Maamuzi ktk Mustakabali wa Maisha ya Watanzania/Wananchi.Ikiwa Binadamu wote ni Ndugu zako basi Utatenda Matendo yanayoleta Faida ktk Jamii.

ii) *Nitaitumikia Nchi yangu na Watu wake Wote*
>Serikali ya CCM Chini ya Dr Magufuli ameendelea kusisitiza Nchini kote na Viongozi wote wa Chama na Serikali.Hasa Waajiliwa, Watumishi, Wafanyakazi wote, Mashirika ya Umma na Binafsi ktk kuhudumia watu wanatakiwa kuwa WAAMINIFU na Waadilifu.Hata ktk Ngazi za Familia na Siyo Waajiliwa tu kuwa Waaminifu na Waadilifu ni Msingi wa Kutekeleza Majukumu ya Kila Siku.

Katika Sheria ya Maadili ya 1995 Ya Umma inasema kuwa Kila Raia awe ni Kioo Cha Maadili bora ya Taifa.

iii) *Nitajitolea Nafsi Yangu Kuondoa Umaskini, Ujinga, Magonjwana Dhuluma*

>Serikali ya CCM kuanzia Chama kimoja hadi Sasa Vyama Zaidi ya 23 Tumekuwa CCM Imekuwa ikiwaomba kila mmoja kushirikiana na Wenzake kuondoa Ukoloni na Leo tunamwomba kila Raia Kufanya kazi kwa Bidii ili kuondoa UMASKINI.Katika Kufanikisha ahadi hii kila Raia asiwe Mbinafsi, Mdhurumaji wala Anayeonea Wengine hasa Wanyonge

*Ahadi ya Uadilifu* kwa Viongozi wa Umma inasema " Nitaepuka Tabia ambayo inavunja heshima ya Uongozi wa Umma hata ninapokuwa nje ya Mahali pa kazi au Nitakapoacha kazi.Ili Nchi iheshimike ni lazima Viongozi wajiheshimu ktk Tabia zao wakiwa ofisi.

iv) *Rushwa ni Adui wa Haki ;Sitopokea Wala Kutoa Rushwa*
>Serikali ya CCM Chini ya Mh Rais na Mwenyekiti wa CCM Kwa Ujumla tunalaani tendo la Kupokea na Kutoa Rushwa kwa Uhalisia wake wa Ndani ni kitendo baya hata kabla ya kuangalia matokeo yake.

Hivyo Mh Rais Dkt John Pombe yake.Hivyo Mh Rais Dkt John Magufuli Alisema " Nitapambana na Rushwa na Ufisadi bila kigugumizi na bila haya Yoyote"

Serikali Ya CCM Chini ya Dkt Magufuli inachukia mnoo Rushwa na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma No 13 ya Mwaka 1995 inasema" Sitaomba, Kutoa wala Kupokea Zawadi au Fadhila za Kiuchumi au Za Kisiasa au Kupokea zawadi au Fadhila za Kiuchumi.
Rushwa ni Adui wa haki kwani tamaa mbele mauti nyuma.

V) *Cheo ni Dhamana Sitakitumia Cheo Changu Wala Cha Mtu Mwingine Kwa Faida Yngu*

>Serikali ya CCM inakataza Tabia ya Ubinafsi kwa Watu wa Matabaka yote.Kiongozi Asitume cheo chake kujilimbikizia mali isivyo kihalali.Hata Wanajamii Wasifanye hivyo.Kwani huko ni kuhujumu Uchumi wa Taifa Letu.Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na 13.ya Mwaka 1995 "Inasema" Sitatumia cheo changu au Wadhifa Wangu kwa Masilahi Binafsi, ya Famili yngu"

Vi) *Nitajielimisha Kwa Kadri ya Uwezo Wangu na Kutumia Elimu Yangu Kwa Faida ya Wote*

>Wahenga Husema"Mvumbika Mbichi hula Mbivu"
Wanasiasa na Maofisa Wanafanya Maamuzi kwa niaba ya Wananchi.

Serikali ya CCM imekuwa ikiwawashauri Maofisa wafanya Maamuzi wakiwa na Wafanyakazi Wengine pale Ofisin kwa Sababu Hufanya.

Vii) *Nitashirikiana na Wenzangu Wote Kujenga Nchi Yetu*
>Serikali ya CCM ndani ya Miaka 40 imekuwa Ikisisitiza Mshikamano wa Umma na Taifa kwa Ujumla hasa mahali pa kazi.

Ushirikishwaji wa Wananchi ktk Maamuzi mbali mbali Serikalini na ktk Masharika, Kuliongeza ufanisi na Utekelezajj mzuri wa Sera.Serikali ya CCM inasisitiza viongozi wetu ktk Ngazi Zote Wafanye Juhudi ya Kufikia Uamuzi Kwa Majadiliano.

Chama kinasisitiza Chini ya Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa, Itikadi na Uenezi Viongozi Kuwatia Moyo Wananchi kufichua Makosa na Yaliyofanywa na Lazima Kurekebisha Makosa ya Nyuma na Kuepuka Makosa mapya".

viii) *Nitasema Kweli Daima.Fitina Kwangu ni Mwiko*
>Chama kinasisitiza Viongozi Wote wa Serikali na Chama Kuwa Wakweli.Panapokuwa na Uozo kila Raia inambidi kuwa Mkweli ktk kufichua hali hiyo.Kufitini Mwenzako kwa Maendeleo yake au Cheo alichopata na Kumletea Uongo haifai.

*MASHARTI* ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma Na.13 ya Mwaka 1995 inasema: Sitatoa taarifa za Siri za Serikali au za Mteja kwa Watu Wasiohusika isipokuwa Kwa Maslahi ya Umma.

Uzalendo kwa Taifa lako ni Nguzo Muhimu ya Maendeleo Endelevu.

Uvunjifu wa Maadili kwa Pamoja ktk ofisi ni Tatizo la Mikono Michafu;Wakati Mwingine Wafanyakazi kwa Pamoja huvunja Maadili ya kazi zao.Ikiwa tendo au Maamuzi ya Aina fulani siyo Sahihi ni Mbaya, Wafanyakazi Wasitende Matendo hayo.Kwani kwa Kufanya Hivyo Watachafuka Mikono.

Mh Rais na Mwenyekiti wa CCM Alisema" Wafanyakazi Wachache Wasio Waaminifu ni Wabaya Kweli Kweli.Ni Nafuu ya Shetani Maana hawajali Shida na Mateso ya Watu Wengine.

ix) *Nitakuwa Raia Mwema wa Tanzania, Afrika na Duniani Kwa Ujumla*
>Serikali ya CCM inasisitiza na Kukumbushia kila wakati kwa Watanzania Wote Kuwa Maadili ya Viongozi ni Muhimu kama Yalivyoainishwa ktk Ahadi ya Kumi za TANU na Misingi minne ya Azimio la Arusha 1967.Misingi hiyo ni;
=Kujenga Nchi ya Watu huru na
Walio sawa.
= Kujenga Taifa linalojitegemea
= Kuweka Uchumi wa Nchi Mikononi mwa Wananchi na Kulea na Kuchagua Viongozi bora Ambao ni Waaminifu n Waadilifu lkn pia Wasiwe Wabinafsi.

X) *Nitakuwa Mtii kwa Rais na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania*

> Mwenyekiti wa CCM Dkt Magufuli anasisitiza na Kushauri Watanzania Wote pamoja na Viongozi Sharti Wawe Watii kwa Rais na Serikali Yao iliyopo Madarakani.Kwenda Kinyume na Hapo ni uharamia.

Maadili kwa Upande Mwingine yanahitaji kuona kuwa Wanasiasa, Watu wenye Nyadhifa na Nchi Zilizoendelea kujizuia kuwadhuru Wananchi Kisaikolojia, Kihisia na Hata Kimwili na Kiroho wakati wakiwa ktk Shughuli zao za Kila cku.

Imeandaliwa na
Mzalendo Petro Magoti
petromagoti9@gmail.com
CCM HQ.Place of Wisdom
 
Back
Top Bottom