Katibu wa CCM Kata Ya Bungu, Kibiti auawa kwa kupigwa risasi

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,432
7,055
Aliyekuwa Katibu wa CCM wilayani Kibiti maarufu kwa jina la Arife Mtulia ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana jana mida ya saa 3 usiku.

========

WAKATI serikali ikijipanga kuanzisha Mkoa wa kipolisi katika wilaya ya Rufiji, Kibiti, Mafia na Mkuranga, Katibu wa CCM kata ya Bungu, wilaya ya Kibiti, Arife Mtulia amepigwa risasi na kuuawa na watu wasiojulikana.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilayani Kibiti, Zena Mgaya, alisema marehemu ameuawa majira ya saa 4 usiku may 13 .

Alisema alipata taarifa la tukio kutoka kwa viongozi wa CCM kata.

Zena alieleza Mtulia ameuawa akiwa anatoka uwani mwa nyumba yake kwenda kuoga akiwa ameshika ndoo ya maji ndipo wauaji wawili walipojitokeza na kumuua kisha kutokomea kusikojulikana.

“Wauaji hao walitumia usafiri wa pikipiki kwa kuiacha mbali na eneo la tukio na baada ya kutimiza adhma yao walitembea kuifuata walipoipaki kisha kuondoka “alielezea Zena.

Alisema Marehemu alikuwa Katibu wa CCM Kata ya Bungu, Mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM Taifa kutoka wilaya ya Kibiti na mjumbe wa Serikali ya kijiji Nyambunda na ameacha mke na watoto.

Zena alisema kufuatia matukio ya mauaji kijiji cha Nyambunda kata ya Bungu kimeshapoteza Mwenyekiti wa kiiji, Mtendaji wa Kijiji, na wenyeviti watatu wa vitongoji vilivyoko katika kijiji hicho .

Alipoulizwa kuhusiana na uchaguzi wa ndani ya chama unavyoendelea ngazi ya shina na matawi Zena alisema wanachama wanagomea kujitokeza. “Uchaguzi wa safari hii ni mgumu hakuna anaejitokeza kugombea kabisa, watu wanahofu “alifafanua.

Nae Asha Hemed na Ramadhani Swedy walisema hali bado ni mbaya kiusalama katika wilaya hiyo na Rufiji.

Walisema jeshi la polisi lisambaze askari wake na maeneo ya vijijini ambako wahalifu hao ndio wamejikita huko.

Huu ni muendelezo wa matukio ya mauaji kama ifuatavyo:-

March 28, 2017 Mwenyekiti wa (CCM) tawi la Mparange na mjumbe wa serikali ya kijiji cha Ikwiriri Kaskazini ,wilayani Rufiji mkoani Pwani, Michael Lukanda aliuawa kwa kupigwa risasi ya kichwani na watu wasiojulikana.

March 12, 2017 Mwenyekiti wa kitongoji cha Kazamoyo, Hemed Njiwa aliuawa kwa kupigwa risasi.

March 1, 2017 mwenyekiti wa kijiji cha Nyambunda, Said Mbwana aliuawa.

Feb 24, watu watatu akiwemo Afisa upelelezi wa polisi wilaya ya Kibiti Peter Kubezya aliuawa kwa risasi.

Jan 19, 2017 Mjumbe wa serikali ya kijiji cha Nyambunda, Oswald Mrope aliuawa kwa kupigwa risasi.

Octoba 24, 2016 Afisa mtendaji wa kijiji cha Nyambunda, Ally Milandu alipigwa risasi na kufa.

Novemba 6, 2016 Mwenyekiti wa kitongoji cha Nyang’unda kijiji cha Nyambunda Mohammed Thabiti alipigwa risasi akielekea kwake.
 
Mkataba wa serikali na raia wake,ni kuhakikisha raia wako salama,na kama usalama wa mmoja wa raia umeingiliwa,basi,mkataba wetu na serikali ni kuwasaka wahalifu na kuwafikisha mahakamani na kuhakikisha hali hiyo haijirudii

Kama serikali inashindwa hilo,basi imevunja mkataba wake na raia, na inapoteza uhalali wa sisi kuiamini kwamba ina uwezo wa kutulinda.
 
a5ed578cba48c4cf7648ffad7b1e58c8.jpg
 
Back
Top Bottom