Katibu wa Bunge msalabani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katibu wa Bunge msalabani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kanda2, Oct 20, 2009.

 1. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  • Wabunge wacharuka, washangazwa
  na Sauli Giliard

  UJENZI wa ofisi ndogo za Bunge zilizopo jijini Dar es Salaam umeishtua Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ambapo mkataba wa awali unaonyesha lilikuwa lijengwe kwa sh milioni 425, lakini hadi kukamilika kwake zilitumika sh bilioni 1.13.

  Mwenyekiti wa kamati hiyo, John Cheyo na wenzake, walishtushwa na matumizi hayo jana jijini Dar es Salaam mara baada ya Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah kuwapa taarifa hizo.

  Cheyo alisema ni aibu na jambo lisilopendeza kwa chombo hicho kuwekwa miongoni mwa taasisi zenye hati chafu kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG).

  Mwenyekiti huyo wa PAC alisema, kutowekwa wazi kwa hesabu za chombo hicho pamoja na kukosekana kwa stakabadhi za malipo yaliyotumika, kumezidisha wasiwasi juu ya matumizi ya fedha za walipa kodi.

  Cheyo alifikia hatua ya kumuhoji Dk. Kashililah iwapo anapata usingizi kutokana na Bunge kupata hati chafu kwa takribani miaka miwili mfululizo.
  Aidha, kamati hiyo ilionyesha wasiwasi wa uidhinishaji wa fedha za ujenzi wa jengo hilo kwani pamoja na mkataba kusainiwa Juni 2007, uthibitisho ulisainiwa Oktoba mwaka huo.

  “Ripoti ya CAG juu ya hesabu za matumizi ya Bunge ni chafu na inashauri kuwepo uangalifu. Mwaka 2005/06 ni shaka na hati chafu, 2006/07 nayo ni hivyo hivyo, leo wewe unaingia ndiyo unadidimiza kabisa. Mkataba unasema jengo la ofisi ya Bunge litagharimu sh milioni 425, leo taarifa inasema sh bilioni 1.13 zimetumika, unafikiri utaratibu umefuatwa?

  “Kwa hali hii, utasemaje unapata usingizi? Kamati ya Bunge haitavumilia hati chafu juu ya Bunge. Bunge halilali usingizi juu ya hati hizi, inakuwaje wewe unalala usingizi?” alihoji Cheyo.

  Aidha, mwenyekiti huyo alisema hakubaliani na mchanganuo wa ujenzi wa jengo hilo na kumtaka katibu huyo wa Bunge kueleza sababu za msingi.
  Akiendelea kuzungumza katika mkutano huo uliowahusisha pia wafanyakazi wa idara nyeti za Bunge, vikiwemo vile vya hesabu, manunuzi na ugavi na mipango, Cheyo alisema, haiwezekani mkataba useme gharama ni sh milioni 425, ghafla ugharimu kiasi cha sh milioni 325, karibu ya ongezeko la asilimia 90.

  Wajumbe wa kamati hiyo walionyesha shauku kubwa ya kufahamishwa mchanganuo wa gharama hizo za ujenzi wa milioni 815 kwa kuwa hakuna maelezo ya kutosha kuonyesha zinakotoka fedha hizo.

  Baada ya kamati kuonyesha wasiwasi wa mchanganuo wa ujenzi huo, Cheyo alitaka apewe sababu tatu ni kwa nini hali hiyo itokee katika taasisi hiyo nyeti inayopaswa kuwa kioo kwa taasisi nyingine za serikali.

  Akiwaondoa wasiwasi wajumbe wa kamati hiyo juu ya hofu iliyojengeka, Dk. Kashililah alisema, mabadiliko ya mara kwa mara wakati wa ujenzi wa jengo hilo, likiwemo egesho la magari, na tatizo la umeme kwa jengo hilo, ni mojawapo ya mambo yaliyosababisha gharama kufikia zaidi ya sh bilioni moja.

  Akiendelea kutoa mchanganuo wa gharama halisi za ujenzi wa jengo hilo, katibu huyo wa shughuli za chombo hicho cha kutunga sheria aliongeza kuwa, awali mara baada ya kusaini makubaliano ya ujenzi wa jengo hilo na kutenga eneo la maegesho, ushauri mwingine ulikuja na kubadilisha ramani na eneo hilo kutakiwa kujengwa jengo jingine.

  “Kabla ya mkataba wa sh milioni 425 ulioingiwa Juni 2007 haujaisha, ndipo ziada ilipokuja ikiwemo umeme kwa kuwa uliokuwepo haukuwa na nguvu, ndipo zilipoongezeka tena sh milioni 325. Bodi ya mamunuzi haikuweza kufanya mabadiliko,” Dk. Kashililah, ambaye ni mtaalam wa mawasiliano ya mifumo ya kompyuta, aliieleza kamati ya Bunge ambayo wajumbe wake walionekana kutokubaliana moja kwa moja na ongezeko la matumizi hayo.

  Aidha, aliongeza kuwa, ofisi hiyo ililazimika kufanya mabadiliko hayo mapema bila kufanya majadiliano upya na kuubadili mkataba wa awali kwa kuwa wangechelewa, wataalam wa ujenzi wa jengo hilo pamoja na washauri waelekezi wangeondoka hivyo kukwamisha ujenzi huo.

  Akitanguliza kukiri kutokuwepo matumizi ambayo hayako bayana katika ujenzi huo na matumizi mengine ya ofisi ya Bunge, aliongeza kwamba, kumekuwepo na mapungufu mengi ambayo yanatokana na ufuatiliaji duni wa matumizi hayo na uzembe.

  Kwa mujibu wa Dk. Kashililah, baada ya kuona kuna upungufu huo mkubwa, aliamua kuunda kamati kufuatilia na hesabu zinazoonekana kuleta shaka.
  Hata hivyo, baada ya wabunge kuonekana kuhama kwenye hoja hiyo, maswali yao yalielekezwa kwenye hati za matumizi ya ofisi ya mhimili huo wa serikali kwani kiasi cha risiti za zaidi ya sh milioni 500 hazikuwepo.

  Katika hilo, ofisi ya Bunge ilieleza kwamba, hati ya sh milioni 404 zinapatikana, jambo ambalo lilionyesha wasiwasi kwa wabunge hao na kuhoji, uhakika wa hati hizo za matumizi ya miaka miwili zinazopatikana wataziamini vipi kwani huenda zikatengenezwa.

  Wajumbe hao walisema, kwa sasa inaonekana sh milioni 121 hazionekani, hivyo, ilitaka maelezo ya fedha hizo zitakavyorudi.

  Katika hilo, mwenyekiti wa kamati hiyo alisisitiza kuwa, haiwezekani hati za matumizi ya sh milioni 525 zikapatikana sasa na kuongeza kwamba, utafutaji wake, ikiwa ni baada ya miaka miwili kupita, ni sawa na ‘wizi mtupu’ na kusema, kamwe kamati hiyo haikubaliani na suala hilo.

  “Inawezekanaje risiti za miaka miwili zipatikane sasa baada ya miaka miwili kupita. Ofisi ilikuwa imelala wapi?” alihoji.

  Juu ya suala hilo la kutokewepo stakabadhi za malipo, Mbunge wa Mchinga, Mudhihiri Mudhihiri pamoja na Manju Msambya waliwachachafya watendaji hao kutoka vitengo mbalimbali vya Bunge na kutaka maelezo ya kina juu ya matumizi hayo yasiyo na uthibitisho wala marejesho.

  Wajumbe hao walionekana kutishwa na taarifa ya hesabu hizo ambayo ilimtaja Msaidizi wa Spika wa Bunge, Christopher Ndalu anayedaiwa kuwa, ametumia zaidi ya sh milioni 70 na hazionekani.

  Katika hilo, Cheyo alisema, Spika wa Bunge, Samuel Sitta alisema, inawezekana ya kwamba, anaonekana chombo anachokisimamia hakiwezi kufanya kazi, hasa juu ya matumizi hayo yanayotia shaka iwapo ni mwenyewe katumia ama msaidizi wake.

  Alisema kuwepo kwa deni hilo kubwa kwa mtu mmoja pekee kunatisha, kwani hata kama spika anasafiri mara kwa mara, haiwezi kufikia safari za Rais Jakaya Kikwete, ndani au nje kwani ratiba yake inaonyesha ya kwamba kila siku ana ziara.

  Wajumbe hao walisema, suala hilo linatisha kwani kwa safari moja tu, harudisha risiti za matumizi ya sh milioni 37 huku taarifa za ofisi ya Bunge zikibainisha kwamba, mtu huyo atawajibika kwa kukatwa mshahara wake huku ikiwa haijulikani fedha hizo zimetumiwa na yeye mwenyewe ama Spika Sitta.

  “Hii ni picha gani tunapata kwa spika? Haileti picha nzuri kwake kwani anaonekana kuwa ndiye aliyechukua fedha hizo,” Cheyo alizungumza kwa ghadhabu na kusema, kamwe kamati yake hairidhiki na watakutana katika kikao cha faragha ikiwa ni pamoja na kuiandikia ofisi hiyo barua ya onyo.

  Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zubeir Ali Maulid, alimtaka katibu huyo kueleza kuwa, iwapo msaidizi huyo wa spika yuko chini yake, ni kwa nini asifukuzwe ama kumpanga mtu mwingine badala ya kumng’ang’ania yeye ambaye anaonekana kuwa hawezi.

  Hata hivyo, Dk. Kashililah alisema, hawezi kumpangia Spika Sitta mtu wa kusafiri naye kwa kuwa hilo ni suala lake binafsi.

  Hata hivyo, katibu huyo alisema, ofisi yake kuwa Dodoma na jijini Dar es Salaam imekuwa ikiwawia vigumu katika utendaji na kujikuta baadhi ya watendaji wake wakizembea kukusanya nyaraka muhimu. Alisema hata baadhi ya nchi za nje wanazokwenda, nyaraka hizo hazikuweza kupatikana na kuahidi kupitia kamati yake, wanatafuta namna ya kuzipata na kuthibitisha matumizi ya ofisi hiyo.
   
 2. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #2
  Oct 20, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  mafisadi tu hao
   
 3. O

  Omumura JF-Expert Member

  #3
  Oct 20, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Haki ya Mungu sitaki kuamini kabisa kwamba spika naye kakubali kuingizwa katika mtego wa aina hiyo, tumekwisha!!
   
 4. Mike-Austin

  Mike-Austin Member

  #4
  Oct 20, 2009
  Joined: Nov 20, 2008
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bravo Cheyo na kamati yako...huu ni uzembe uliopitiliza, kuchukua pesa za walipa kodi bila huruma...ni sawa na polisi aliyetumwa akwakamate makahaba naye akapewa ofa ya ngono, atamshika mtuhumiwa?...kweli tuachie MAPENGO majemedari wazibe?.

  Ni kidhibiti tosha, Spika na watendaji waote wa bunge hakuna aliyeupande wetu..wanathamini wenye mali, tabaka la chini?...
   
 5. Mukuru

  Mukuru Member

  #5
  Oct 20, 2009
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tumekuwa na utamaduni wa kuwa na kamati kibao lakini huwa hakuna hatua madhubuti dhidi ya watuhumiwa wa ubadhirifu wa mali za umma. Ifike mahali watu wawajibishwe badala ya kuwa na longolongo tu.
   
 6. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #6
  Oct 20, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kukubali kuingizwa! akh nani alikwambia alikuwa nje ..sita ni fisadi tangu TIC ....anatafuta umaarufu tu tunawaita wale waleeeeeeeeee!
   
 7. mkokoteni

  mkokoteni Member

  #7
  Oct 20, 2009
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 48
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 15
  Sasa ukitaka kushangaa zaidi, uliza mshahara wa bwana Ndalu kwa Mwezi ni kiwango gani. halafu linganisha ni pesa ambayo amechukua kama imprest pesa ambayo hata atakapo staafu pensheni yake haitafika million 35. wizi mtupu!
   
Loading...