VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Katibu wa Bunge, ndugu yangu Dr. Thomas Kashililah, umekosea kucheza filamu dhidi ya watani zetu wapinzani (CHADEMA na CUF). Ni kuhusu uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Katika taarifa yako kuuhusu uchaguzi huo, umedai kuwa CHADEMA hawana 1/3 inayopaswa kuwa ya wanawake. Na CUF vivyohivyo.
Twende taratibu. Kwanza, Tanzania inapaswa kuchagua Wabunge tisa. Moja ya tatu ya tisa ni tatu. Kwahiyo, Wabunge wanawake wa Tanzania (ukiachana na mambo ya vyama) wanapaswa kuwa watatu. Katika uchaguzi huo, CCM tuna wagombea wanawake zaidi ya watano. Wanaweza kuchaguliwa watatu. Na hivyo Tanzania kuwa na Wabunge wanawake watatu.
Tena, CHADEMA wana nafasi mbili katika uchaguzi huo. Yaani, ina watu wawili kuwa Wabunge wa Afrika Mashariki. Inawezekanaje kuwa na moja ya tatu ya watu wawili? CUF wana nafasi moja. Inapatikanaje moja ya tatu ya mtu mmoja? Ndiyo maana nathubutu kusema kuwa Ndugu yangu Kashililah umeicheza hovyo filamu hiyo.
Linapokuja suala la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Tanzania huwa moja na kupaswa kuwa na Wabunge tisa tu. Kinachotakiwa ni kuwa na mgawanyiko wa vyama kama alivyofanya Spika Ndugai, jinsia kama wagombea wanawake na wanaume walivyo na kadhalika. Hakuna takwa la kila chama kuwa na idadi fulani ya wanawake au wanaume. Hakuna.
CCM inaweza kutoa Wabunge watatu wanawake kwa niaba ya Tanzania. Tena italeta sifa na heshima kwa CCM yetu. Tena CCM itatamba linapowekwa mezani suala la jinsia katika Bunge letu hapa na la Afrika Mashariki. CCM itasifiwa na kupigiwa mfano. Kwani ni lazima Wabunge wanawake watoke CHADEMA na CUF?
Bastola ya nini tena jamani!?
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam