Katibu Mkuu Wizaraya Mambo ya Ndani ya Nchi afanya ziara ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa

Mar 26, 2016
21
7
Katibu Mkuu Wizaraya Mambo ya Ndani ya Nchi afanya ziara ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)



Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jaji Meja Jenerali Projest Rwegasira ametembelea Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka

Katika ziara hiyo ameweza kutembelea kituo cha Uchakataji Taarifa kilichopo Jengo la COPY-CAT zamani BMTL na kushuhudia kazi zinazofanywa na watumishi wa NIDA ambapo ni uchakataji wa taarifa na kuingiza kwenye mfumo. Katika ziara hiyo ametilia mkazo suala la NIDA kukamilisha usajili Desemba 31, 2016 na kusisitiza wafanyakazi kufanyakazi kwa kujituma na kuendana na kasi ya Serikali ya sasa ya “Hapa Kazi tu”
 
Mzee Rwegasira!! Yani huyu mzee maisha yake kama Nyerere! Ukiambiwa ni katibu mkuu lazima ukatae coz ana maisha flan ya kawaida sana
 
Hata makatibu huwa wanafanya ziara, nilijua ni wanasiasa tu tujuze vizuri.!
 
Wawalipe watumishi waliokuwa wanaratibu huo mchakato..
kuna mama mmoja mpaka kalia wakidai stahiki zao za malipo na mkurugenzi anapiga chenga, hatari.
 
Mbona hizi ziara hazielekezwi zaidi kwenye maslahi ya Taifa Kama kwenye mashimo ya dhahabu, gesi, kwenye vitambulisho kuna makaratasi tuu. Kama Pesa imeliwa inajulikana tayari.
 
Back
Top Bottom