Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kutua Tanzania usiku huu

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
18,849
67,285
António-Guterres-UN-secretary-general.jpg


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres anatarajiwa kuwasili Nchini usiku huu wa saa 4 akitokea Kenya.

Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa atafanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Agustino Mahiga kisha kuondoka zake hapa nchini.

Waziri Mahiga atamuwakilisha Rais John Pombe Magufuli ambaye yupo Mkoani Dodoma kikazi.

Source: Azam News
 
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres anatarajiwa kutua usiku huu wa 08/03/2017 katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Mogadishu Somalia kupitia Kenya ambapo alifanya zaira ya dharula ili kutazama namna dunia inavyoweza kukabiliana na janga la njaa na ukame katika ukanda huo.

Baada ya kutua Julius Nyerere Airport,Katibu Mkuu huyo atafanya mazungumzo na Waziri wa Mashauriano ya kigeni wa Tanzania Balozi Augustine Mahiga katika eneo la wageni Mashuhuri (VIP) Terminal Two na baadae kuondoka na kuelekea moja kwa moja New York Marekani.

Balozi Mahiga anachukua nafasi ya kukutana na Guterres kwa niaba ya Rais John Magufuli ambaye toka jana yupo Dodoma akijiandaa na vikao vya chama vinavyotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Kabla ya kuja Tanzania,Katibu huyo alitembelea kambi kubwa ya Wakimbizi wa Somalia iliyopo nchini Kenya na amefanya mazungumzo na Rais Kenyetta kuhusu suala la wakimbizi wa Somalia na katazo la Marekani kuwapokea wakimbizi toka nchini Somalia.
 
Daaah nyie UKOVI....mna laana.....HIVI HAO WAGENI WOTE WANAOKUJAGA HAPA TZ RAIS huwa anaongea nao kwa lugha gani???mbna hata juzi tu KULE MTWARA MZEE WA WATU alikuwa anaongea ENGLISH vizuri tu....
Kingne hivi hao wengne waliokuwa wanaongea ENGLISH kipi hasa cha maana kilitufaidisha sisi wananchi kiasi kwamba kwa sasa hatupati????

Hapa MAGU anatuonyesha yakuwa HATA SISI watanzania ifikie wakati TUSINYENYEKEE WAZUNGU na kuacha kufata ratiba zetu kisa wao.....
Huyu ndiye RAIS sasa tumepata ANAIFANYA TAASISI YA URAIS IHESHIMIWE........
 
Back
Top Bottom