KATIBU MKUU WA CHADEMA DR VINCENT MASHINJI AMEKUWA MWIBA KABLA HATA YA KUAZA KAZI ZAKE.
Na Kilawa the Iron
Chama cha demkrasia na maendeleo CHADEMA kimemtangaza rasmi Dr Vincent MASHINJI kuwa katibu mkuu wa Chama. Anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dr Wilbroad Slaa.
Hali imekuwa tofauti kabisa na matarajio ya wengi. Kwani kabla ya Dr Vincent kutangazwa wanachama wa vyama vingine kama vile CCM walikuwa wakisambaza propaganda za ukanda huku wakimpa nafsi kubwa Mh Sumaye kuwa atapata nafasi ya katibu mkuu, ccm walifanya haya ili kuendelezea propaganda yao ya ukanda yaani ukasikazini. Utofauti uliojitokeza umewalegeza sana mahasimu hawa, kwa sasa wanatumia mda mwingi kutunga na kusambaza uongo juu ya Dr Vincent.
Pia vijana wengi ambao ni mashabiki na wafuasi wa chadema walikuwa wakipambana kisawasawa kupitia mitandao ya kijamii huku kila mmoja akimuona anayedhani anafaa ni bora kuliko wa mwingine. Wengi walidhani Kati ya hawa mmoja wao atakuwa katibu mkuu, waliojaa kwenye midomo ya watu wengi ni Mh Frederick Sumaye, Mh Tundulisu, mh John Mnyika, Salimu Mwalimu, Marcus Albania n.k.
Amini usiamini kila mmoja kashangaa kuona waliotajwa, na waliozungumzwa hata mmoja hajafanikiwa kuwa katibu mkuu.
Lakini kwa kuwa chama hiki ni makini kimefanya tofauti na matarajio ya watu waliokuwa wanasigana mitandaoni na kuamua kumpa nafasi hiyo Dr Vincent.
Hali hii imeendelea kuwatesa zaidi wapinzani wa Chadema hasa CCM hali inayopelekea kuanza kutengeneza propaganda juu ya Dr Vincent ambazo hazina kichwa wala miguuu.
Kuna maswala wanayaandika ukiyasoma unajaribu kujiuliza. Je hawa CCM walitaka nani ndo awe katibu wa chadema? Wanakasilika nini Dr Vincent kuwa katibu mkuu wa chadema kama sio mwiba?
Kama CCM wanaona mtu huyo si makini si watulie ili wapinzani wao wayumbe?
Dr Vincent toka nimemfahamu sikuwahi kuona anateteleka misimami yake, ni mtu makini, mwenye uwezo kifikira. Naamini CHADEMA haitajuta kumpa nafasi hii waliompa.
Kwa mambo wanayoyafanya wafuasi wa ccm mitandaoni tamedhihirisha wazi kabisa kuwa mtu huyu ni Mwiba wenye ncha kali, ni mwiba unaochoma na kutokea upande wa pili hivyo wanatumia mda mwingi kupambana na mtu ambaye hata hajaaza rasmi kazi.
Binafsi nalipongeza baraza kuu la chadema, nampongeza Mh Mbowe na viongozi wengine kwa umahili wao wakumbewa kiongozi anayetufaa kwa wakati huu na kuendelea.
Nampongeza katibu mkuu wa chadema Dr Vincent, na namuombea kwa mola ampe uwezo zaidi ili atende kazi yake kwa weledi zaidi, afanye kazi yake kwa uwezo alionao ili tusonge mbele.?
Mwisho nawaasa wanachadema wenzangu kumpa ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa majukumu yake. Tumuunge mkoni kama tulivyofanya kwa Dr Slaa kipindi alipokuwa katibu wetu.