Katibu mkuu UVCCM ateta na Waziri Jenister Mhagama

MASIGA

Senior Member
Aug 29, 2015
130
281
Katibu Mkuu Wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi mwl Raymond Stephen Mwangwala (MNEC) amekutana na kufanya Mazungumzo na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe jenista Mhagama Pamoja na Naibu Waziri wa Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe @AnthonyMavunde katika Ofisi za Wizara hiyo Leo jijini Dodoma.

Mwl Raymond ameitaka wizara hiyo kuhakikisha utoaji wa vibali vya kazi kwa wageni unazingatia taaluma na fani ambazo vijana wazawa hawana ili kulinda ajira zao. Pili, amezungumzia mazingira ya kazi kwa wafanyakazi viwandani na migodini kama vile usalama, maslahi na mikataba ya kazi kwani walio wengi huku ni vijana.

Pia amewaeleza kuwa uwezeshaji wa vijana kiuchumi bado una suasua achilia mbali serikali imeweka utaratibu wa halmashauri kutoa mikopo isiyo na riba ambayo ni asilimia 10 ya fedha zao za ndani pamoja na uwepo wa mifuko ya uwezeshaji kiuchumi iliyo chini ya wizara hiyo lakini bado uwezeshaji kwa vijana ni changamoto. Amewaomba eneo hili liwe la kipaumbele wanapokuwa katika ziara zao za kikazi.

IMG-20180903-WA0035.jpg
IMG-20180903-WA0032.jpg
IMG-20180903-WA0033.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom