Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Nimekuwa nikayatazama majina ya makatibu wakuu viongozi tangu tupate uhuru, sijaona jina la muislam. Lakini katika marais wanne walioiongoza nchi hii mpaka leo hii kuna waislam wawili. Mzee Mwinyi alimuamini Paul Rupia, akampatia cheo cha katibu mkuu kiongozi. Mzee Kikwete alimuamini Mzee Philemon Luhanjo na akampatia wadhifa huo wa CS.
Humu jamii forum watu hutokwa povu kila wanapotazama vyeo vya mashirika makubwa. Watu wanaandaa excel sheets zinazoonyesha wingi wa wakristo kulinganisha na waislam. Inajengwa hoja kwamba ipo aina fulani ya dhuluma dhidi ya wasomi waislam. Lakini miaka 20 ya urais wa Mwinyi na Kikwete, uliwategemea makatibu wakuu viongozi ambao ni wakristo. Mzee Mwinyi na Mzee Kikwete waliwaamini wakristo, wala hawakuongozwa na fikra za kidini, walitazama utendaji kazi badala ya kutazama dini zao.
Fikra za kidini ni fikra muflis, hazifai kabisa kuendekezwa, na mara nyingi huashiria uvivu wa mtu kufikiria mambo ya maana yenye tija maishani mwake. Baba yangu mzazi aliwahi kuniambia kwamba tarehe 8 desemba 1961 yaani siku moja kabla ya uhuru, nchi hii ilikabidhiwa kwa Mungu, waislam waliikabidhi nchi kwa Mungu kivyao, na wakristo wakaikabidhi kwa Mungu kivyao. Ulikuwa ni uamuzi uliotazama mbali sana, la sivyo Tanzania ingeshameguka vipande vipande kwa sababu ya fikra potofu za udini.
Watoto wasome kwa nguvu zao zote ili baadae CV zao ziweze kuwapatia ajira, wawe wanaswali Ijumaa au wanasali Jumapili, sio kigezo cha wao kuajiriwa. Njia za mkato maishani mara nyingi humjaza mtu hasira, kwani zinaweza kumpeleka mtu mahali ambapo hakutaka kwenda. Mungu ibariki Tanzania.