Katibu Mkuu CCM, Ndg. Chongolo achana na mali za chama, utakwama

Ashugulike na vyanzo vipya ili wahuni waje waneemeke badala yakuzuia wahuni waliotafuna vyanzo vilivyokuwepo.
Ama kweli tunasafari ndefu kiuongozi.
Siku moja utaelewa endelea kujifunza! Dunia haina.usawa
 
Nimeona wengi wakizungumza na nimeona pia magazeti yakiandika na hata Leo gazeti la mwananchi limeandika.

Mali za chama ni kaburi lako ndani ya CCM, achana kabisa na kufatilia wala kutaka kujua lolote.

Ongoza chama katika shughuli zake zote fanya mipango ya chama kisaidie kwa namna zote, Ila usiguse kwenye kujua Mali za chama.

Usipite njia aliyopita bashiru, njia hiyo ni ngumu na hutashinda. Ugomvi wa bashiru na CCM ya kale Wala haukua sababu ya yeye ni CUF, bali ni kuanza kuchokonoa mambo yaliyopita na ambayo yalifanya na wakongwe.

Mali zilishaenda, lindeni zilizopo sasa zisiende. Ukianza kuuliza uliza au kuchokonoa hutaweza kufanikiwa popote.
Usimtishe Katibu Mkuu, muache apige kazi, Kama Kuna majizi lala nayo mbele! Sisi wanachama tupo pamoja nanyi viongozi wetu! Kikubwa asionewe au kusingiziwa mtu juu ya Mali alizojimilikisha za Chama!
 
Mali za chama ni kaburi lako ndani ya CCM, achana kabisa na kufatilia wala kutaka kujua lolote

Kama kuna kitu Magufuli aliwasaidia hao CCM ni kuhakikisha chama chao hakiwategemee wafanya biashara katika kukiendesha. Ndio maana alipoingia tu akaunda tume ya kuhakiki mali zake ili kiweze kujiendesha kutumia rasimali zake. Wahuni walijimilikisha mali za chama mpaka vituo vya TV kama mali zao licha ya majumba na viwanja!!! Wakina Bulembo wakajimilikisha mashule!!

Sasa Chogolo asipothibiti mapato toka kwenye vitega uchumi vya chama kwa kuwaogopa hao wahuni chama chao kitarudi kule kule kwa wakina ROSTAM,ABOOD, ZAKARIA MOHAMED ENTERPRISES, wakina PATEL na mwishowe kukosa mwelekeo na kurudi kule kule kwenye ufisadi.
 
Kwa kuwa Nd. Dani Chongole ndie immediate successor wa Bashiri ambae alipewa kazi ya kufukunyua na kugeuza kila "jiwe" ili mali za wana-CCM zibaki kuwa za CCM taasisi na sio wana-CCM binafsi.

Kwa kufanya hivyo anakosea wapi?

Hii ikiachwa kuna kuna siku "hao hao" wanaweza kusafirisha tena Twiga then tunabaki tunazamana kwa kuogopana ukifukunyua makaburi, hutabaki salama.

Hivi Nyerere aliekuwa Mkiti wa Kwanza CCM na Msekwa Katibu Mtendaji wa kwanza CCM (sawia na cheo cha Katibu Mkuu sasa), au mzee Mangula aliekaa miaka 10 kama Katibu mkuu wangekuwa na "ulafi wa mali za CCM"; hawa wa sasa wangekuta nini?

Kama kuna kansa ambayo inatafuna CCM na serikali, ni pale mtu anakwiba, then badala ya kuwajibishwa, ni either waliobakia wanapotezea kwa kumwonea "haya" aliekwiba, na hii sio sawa hata kidogo.

Mie namshauri Katibu Mkuu CCM akaze, na kama anaweza amtafute Bashiri na timu yake yampe hadidu za rejea kwa masimulizi ili kuwa na nidhani kwenye mali za taasisi.
Hao ndo huwa wanamchukia magufuli na maana hakuona haya kufukunyua huo wizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usidanganye watu. Igomvi wa Bashiru na ccm ni kutaka kunifanya mungu mtu na kumshauri mwendazake aue ue ovyo watu kwa kivuli Cha uzalrndo. Bashiru alivyoanza kuwa mchaei anashinda kwa waganga Mambo ndo yalianza kuharibika mna watu walishindwa kumuelewa kuwa Ni MC au katibu!!!
Haa kama huna cha kuandika kaa kwa kutulia usome comment za watu wengine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tengeneza Sera za Chama nzuri, jenga Chama kuanzia ulipoanzia, and then songa mbele Kaka na hiyo ndio dhana nzuri ya Uongozi.

Achana na mambo ya utukuaji makaburi Kaka.

All the best!!
Acheni kumtisha waliopola Mali za chama lazima wazirudishe watake wasitake.
Bila shaka mtoa mada ni mtetezi wao
 
Nimeona wengi wakizungumza na nimeona pia magazeti yakiandika na hata Leo gazeti la mwananchi limeandika.

Mali za chama ni kaburi lako ndani ya CCM, achana kabisa na kufatilia wala kutaka kujua lolote.

Ongoza chama katika shughuli zake zote fanya mipango ya chama kisaidie kwa namna zote, Ila usiguse kwenye kujua Mali za chama.

Usipite njia aliyopita bashiru, njia hiyo ni ngumu na hutashinda. Ugomvi wa bashiru na CCM ya kale Wala haukua sababu ya yeye ni CUF, bali ni kuanza kuchokonoa mambo yaliyopita na ambayo yalifanya na wakongwe.

Mali zilishaenda, lindeni zilizopo sasa zisiende. Ukianza kuuliza uliza au kuchokonoa hutaweza kufanikiwa popote.
Lazima zifuatiliwe, chukulia mfano CCM singida,, ina aset nyingi sana na zinaingiza mabilioni,, lakini hawawezi maliza jengo lao ambalo ujenzi wako ulisimama tangu kabla ya KAGERA WAR,,
Watu wanavimbisha vitambi tu... Miaka nenda miaka rudi
 
Back
Top Bottom