Katibu Mkuu(CCM), Dkt. Bashiru: Umoja wa Vijana CCM(UVCCM) umepoteza uelekeo

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) imeelezwa kupoteza mwelekeo hivyo kuna kazi ya kufanya kuiweka sawa.

Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally alitoa kauli hiyo jana Ijumaa Mei 3 katika mkutano na wahariri na wamiliki wa vyombo vya habari jijini Dodoma.

Dk Bashiru alisema iko haja ya kufanya mageuzi ndani ya jumuiya hiyo ambayo inategemewa kwa kiasi kikubwa na CCM.

Aliwaambia waandishi kuwa kwa sasa CCM kinaandaa vyuo vyake vya Ihemi na Zanzibar ili waanze kuwapika vijana kuwa viongozi wazuri.

Hata hivyo, alisema vijana wanaotakiwa kupikwa katika vyuo hivyo siyo lazima wawe wana CCM tu bali hata na wengine watapikwa ili wakasaidie maeneo yao.

Alisema katika kipindi cha sasa, atatumia watu mbalimbali atakaowakaribisha ili waweze kuzungumza na vijana hao kuwakumbusha misingi na umuhimu wa jumuiya hiyo.

Katibu huyo aliwataka waandishi kutumia kalamu zao kuisaidia CCM kwa kuikosoa inapobidi na kutaja mema pale inapobidi.

Kwa upande mwingine aliwataka waandishi kuandika mema hata kwa vyama vya upinzani kwa sababu hawawezi kujua kwamba chama chochote kinaweza kuwa chama tawala hivyo watoe haki kwa wote bila upendeleo.
 
Huyu ameshiba huyu anataka kumfuata marehemu Kolimba, ohhhh!

CCM haikosolewagi na wana CCM tena haswa kipindi hiki ambacho kinaongozwa na malaika anaetaka akaongoze na malaika mbinguni, wenzake kina Bashe waliambiwa wanasema sema hovyo wakidhani ATAWATEUA na hawateui ng'o.
 
mwenyekiti katibu mkuu na sekretariati yako yote ni zero mumiweke nchi kwenye lindi la damu mukaachia TISS ndio waendeshe chama chenu harafu unajifaragua kwa umbeya potea huko Bashiru historia itakuhukumu sana wewe na mwenyekiti wako
 
Hasichokijua nikuwa waliopewa chama Magufuli ruling party,wanachokifanya sio cha ccm bali wanafanya kuimarisha chama chao.
 
CCM imepoteza mwelekeo toka miaka mingi.... Kilochobaki huko ni kufanya madhambi zaidi ili kuficha dhambi zao.
Mungu anawaona
 
Acheni porojo tunataka maendeleo na sio siasa
Muwapike waweje?
Hata mradi wa karanga hawana
 
Hawa hapa
image.jpg

image.jpg
 
ATTENTION PLEASE!!
Ladies and gentlemen, boys and girls, brothers and sisters, uncles and aunties, nephews and nieces, doctors and nurses, neighbors and colleagues, students and graduates. I really don't have anything to say. Thanks for your attention.😂😂
 
Back
Top Bottom