nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,860
- 5,803
[TABLE="width: 879"]
[TR]
[TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD]
na Ali Lityawi, Kahama
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD]CHAMA cha Mapinduzi wilayani Kahama kimeibariki Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kumhoji katibu wake wa Siasa na Uenezi wa Wilaya, Masoud Melimeli, anayetuhumiwa kuomba na kupokea rushwa.
Hata hivyo chama hicho kimekana kupata malalamiko yoyote kutoka kwa mfanyabiashara yeyote yanayomtuhumu katibu wake kuhusika na vitendo hivyo.
Tamko hilo limetolewa jana na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama baada ya taasisi hiyo kumshikilia kwa muda Katibu wake wa Siasa na Uenezi kwa kutuhumiwa kujipatia shilingi 500,000 kutoka kwa mfanyabiashara mmoja kwa lengo la kwenda kutoa hongo halmashauri ya mji ili kupewa zabuni ya kuchonga vibao elekezi vya alama ya mji.
Mlolwa aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake kuwa pamoja na ofisi yake kutopata malalamiko yoyote kuhusiana na tuhuma zinazomkabili Melimeli, chama hakiwezi kuingilia wajibu wa taasisi hiyo na inatoa baraka ifanye kazi yake kwa mujibu wa taratibu zake na anaamini suala hilo litashughulikiwa kisheria.
Kauli ya mwenyekiti huyo ilikuja baada ya waandishi wa habari kumtaka atoe tamko juu la tukio la katibu wake wa siasa na uenezi kukamatwa na kuhojiwa na taasisi hiyo kuhusu tuhuma hiyo.
Hivi karibuni CCM ilifanya mabadiliko yenye lengo la kuboresha mapato yake kwa kuwaondoa baadhi ya wapangaji wake wakorofi wakati wa malipo na kuweka wapya hali ambayo kiongozi huyo aliitumia kuwaomba rushwa ili awapendelee wakati wa ugawaji wa vibanda hivyo.
Kutokana na hali hiyo mwenyekiti huyo wa CCM aliitaka taasisi hiyo kufanya kazi yake bila kuingiliwa na wanasiasa na baada ya kubaini ukweli kamati yake ya siasa ya wilaya, ingelikaa kutafuta ufumbuzi juu ya suala hilo.
Alifafanua kuwa mambo ya chama yanapitia kwenye vikao na kabla ya hatua hiyo atamuita ofisini kumhoji kuhusiana na suala hilo lakini bado maamuzi yatatokana na vikao vya maamuzi hivyo pamoja na TAKUKURU kufanya kazi yake na chama nacho kitaketi kujadili hilo na kulitolea maamuzi.
Kwa upande wake mkuu wa TAKUKURU wilaya Kahama, Enocker Ngailo, alisema ofisi yake juzi ilianza rasmi kumchunguza katibu huyo kwa tuhuma zinazohusiana na kujipatia pesa kwa mfanyabiashara kwa lengo la kutoa rushwa ili wapate zabuni halmashauri ya mji ndipo zilipozuka hizo tuhuma zingine ambazo hata hivyo hakuna mfanyabiashara yeyote aliyefika kutoa ushahidi wa kumtia hatiani.
Hata hivyo Ngailo alisema taasisi yake itaendelea na uchunguzi juu ya wafanyabiashara waliotoa pesa ili wapatiwe vibanda.