Kididimo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 4,020
- 3,657
Habari kwenu wana JF. Nimeangalia kinachoendelea katika teuzi za karibuni kwa Mh. Prof. Kitila (Katibu Mkuu W/Maji) na jana Mh. Mghwira(RC. Kilimanjaro) na kunitia moyo fulani. Moyo wenyewe,ni matumaini ya maendeleo ya haraka zaidi,kwa wapinzani kushirikishwa moja kwa moja ktk kutenda na siyo kukosoa tu.
Ninaona dalili za Mapendekezo ya Katiba ya Warioba juu ya kuunda serikali ya pamoja yakinukia! Ukiangalia kwa undani,malengo makuu ya Vyama vyote yanafanana yaani "Kuwatumikia wananchi". Hivyo,kwa teuzi hizi mbili,naunga mkono,na ifike mahali iwe rasmi,serikali iundwe kutokana na vyama vyote.
Au wadau mnalionaje hili?