DR. MWAKABANJE
JF-Expert Member
- Nov 7, 2012
- 1,976
- 3,127
Sina tatizo na mabadiliko tunayotaka ndani ya CCM juu ya katiba ya chama lakini kuna vitu kama mtanzania mwenye fikra huru lazima ujiulize.
Tunataka tupunguze nafasi za uongozi ndani ya chama na hili tunalifanya haraka na pia mtu mmoja cheo/ kofia moja ili kutumikia chama na wanachama kwa ukaribu na ufanisi ni vyema.... lakini kwa nini hili linaonekana ni muhimu na haraka zaidi wakati kile kiporo cha jaji
Warioba hatujakimaliza na tupo kimya na mbaya zaidi tulisikika tukisema hilo hatukuwahi ahidi kwenye uchaguzi uliopita na zaidi zaidi tumekwisha tumia pesa nyingi za walipakodi.
Hapa ndo nashindwa kuuona ule viongozi wetu wanauita uzalendo wapo nao...... watanzania tunahitaji katiba mpya sio wakati wa awamu iliyopita tu bado hata awamu hii tunahitaji, mtu mmoja vyeo vingi ndani ya chama hapana..... lakini pia kiongozi mmoja mamlaka makubwa hapana kwani ni hatari kwa afya ya maendeleo ya nchi.
Mchana mwema