Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,468
- 113,583
Wanabodi,
Demokrasia ni very expensive!, kama tunataka demokrasia ya kweli, hatuwezi kuepuka gharama, kuigharimia ili kuipata!.
Natoa ushauri huu, baada ya kuusoma mchango wa mwana jf mwenzetu huyu, akichangia mjadala fulani humu, amesema hivi na hapa ninanukuu.
Wale wabunge la JMT na Wawakilishi wa BLW, wamegeuka wajumbe wa bunge la katiba by virtue ya ubunge wao kule JMT na BLW ambayo ni mabaraza ya kutunga sheria, lakini sio katiba!. Wananchi waliwachagua kuwa wawakilishi wao katika mabaraza hayo, kwa kuwatuma kwenda kuwatungia sheria!, nani aliyewatuma kwenda kuwatungia katiba?!, au sasa kutunga sheria ndio sawa na kutunga katiba?!.
Kiukweli kabisa kutoka ndani ya moyo wangu, na kiuhalisia, wabunge hao wa Bunge la JMT na wajumbe wa BLW, hawana "peoples mandate" yoyote ya kuwatungia Watanzania katiba!. Uamuzi wa kuwageuza wabunge na wawakilishi kuwa wajumbe wa bunge la katiba, umefanywa kuokoa gharama za kuitisha uchaguzi wa wabunge wa bunge la katiba!, "its a process to save money!, hivyo ni kweli kabisa serikali yetu imeamua kuukubali ule msemo, "if you think education is expensive, try ignorance!", hivyo imeamua "to save money" because democray is expensive!.
Kama process hiyo ingefanyika, kusingelikuwa hata na haja ya wale wateule wa rais amba ni wawakilishi "viini macho" wa wananchi!. Nimewaita "viini macho", kwa sababu logic ya uteuzi wao, toka makundi mbalimbali ya jamii, ni kuhalalisha kuwa "wananchi" wamewakilishwa!, jee ni wananchi gani waliowachagua hata kuwawakilisha?!.
Hoja ya hao wajumbe 201 itatetewa na sheria kuwa "wale wawakilishi wa wananchi, tuliowatuma kwenda kutunga sheria, pia walitunga sheria iliyompa mamlaka rais wa JMT. kuwateulia "wawakilishi" wao kwenda kuwatungia katiba yao, hivyo rais wa JMT amepata hiyo mandate ya kuwachagulia wananchi, wajumbe wa bunge la katiba by proxy iliyotolewa na wawakilishi wao, waliotumwa tuu kutunga sheria na sio katiba, na ni katika utungaji huo wa sheria, wakatunga sheria halali kumuwezesha rais kuwachagulia wawakilishi wao na kutunga katiba ambayo wao hawakutumwa!.
Najua fika hoja yangu hii itakuwa ni ngumu kueleweka na huu uzi utapata wachangia wachache kufuatia si wengi wenye uwezo wa kuzama deep kwenye issues kama hizi!.
Wasalaam.
Pasco.

Hivyo, ni muhimu process ya kutengeneza ya katiba mpya iongozwe na some normative principles. Vinginevyo, ni sawa na kuwa na sheria ambayo haina policy backing. Hizo normative principles ni pamoja na
- Process ya kutengeneza katiba lazima ifanywe na bunge la katiba lililochaguliwa na wananchi moja kwa moja.
- Hili bunge la katiba lazima liwe na unlimted power in the constitutional making. Litakuwa na unlimited power kwa sababu ilitakuwa limechaguliwa directly na wananchi ambao ndiyo wenye mamlaka ya mwisho na nchi yao.
- Mchakato mzima wa kutengeneza katiba mpya lazima uwe inclusive and participatory.
- Kufuatia hoja hii, kama ni kweli "all that starts well, ends well!", huu mchakato wa katiba unaoendelea, did not starts well, and its not likely to end well!. Its very unlikely, something that did not start well, to end up well!, hivyo nashauri hili Bunge la Katiba linalokutana Dodoma livunjwe kabla halijaundwa rasmi! (before being constituted!) kwa sababu halina "Mandate" of the People of Tanzania" kufuatia kuundwa bila ushirikishwaji wa wananchi directy but only by proxy!, tuunde Bunge la kweli la Katiba, lenye mandate of the people ndipo tuandike Katiba yetu Mpya!.
- Mkutano wa Kitaifa, "National Convention" ambao ungeshirikisha wajumbe kutoka makundi yote ya jamii (Wajumbe 3,000-5,000), ili kujadili na kuweka "dira" na "dhima" au "misingi" au "tunu" za Taifa, kujua Tanzania tunataka kujenga taifa la namna gani!.
- Baada ya kuwa na "Dira" ndipo tunaunda "Tume ya Wataalam" kukusanya maoni ya wananchi kuhusu ni nini wanataka katika katiba yao ili kuitekeleza ile dira na dhima ya Taifa ( Tume ya Warioba). Hii tume inakusanya maoni yote na ya wote, ikiwemo wanaotaka serikali moja, mbili, tatu, uchifu, ufalme, usultani etc.
- Baada ya Tume kukamilisha kazi yake, inaundwa tume ndogo ya wataalamu wa katiba, kuyachambua maoni hayo na kutoa rasimu ya katiba.
- Unaitishwa uchaguzi wa nchi nzima kwa wananchi kuwachagua wajumbe wa bunge la katiba (constituent assembly), kitendo cha wananchi kuwachagua wajumbe wao wa katiba, kunawapa mandate wabunge hawa kuwawakilisha wananchi kwenye bunge la katiba.
- Bunge hili la katiba, ndilo linapitia rasimu, likiwa na "peoples mandate", kuboresha, kuongeza, kupunguza au hata kuiweka kando rasimu nzima na kuunda mpya na katiba hiyo itaanza na maneno "we the people of Tanzania ..."
- Hatua ya mwisho ya wananchi kuipigia kura ya ndio au hapana kuipitisha, na hivyo kupata katiba mpya yenye uhalali wa wananchi!.