Katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba mpya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by Jumakidogo, Dec 31, 2010.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Dec 31, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  KATIBA MPYA


  mjadala wetu mkubwa uliopo sasa kuhusu mchakato wa mabadiliko ya katiba ya nchi yetu.
  Baada ya kuandikika mada yangu fupi kuhusu katiba hapo jana, nimepokea maoni ya wadau mbalimbali, wale walioniunga mkono nawashukuru sana na, hata wale walionipinga nao nawashukuru pia. Nimelazimika kuandika tena hasa kwa ajili ya wale walionipinga na kwa mtazamo wao kuona kuwa pengine nimepotoka.
  Siwalaumu wao moja kwa moja bali naulaumu upeo wao mdogo wa kuelewa. Sikuwa na maana ya kupinga mabadiliko ya katiba, nilikuwa natoa angalizo kuwa, wakati tunadai katiba mpya je hii ya zamani watanzania walipewa fursa ya kuisoma na kuielewa kwa upana? Je, ni kweli serikali yetu haina uwezo wa kuchapisha katiba na kuisambaza nchi nzima kwa gharama nafuu ikiwa inao uwezo wa kuwalipa DOWANS mamilioni ya shilingi?
  Nyinyi mnaodai kutamba hadharani kuwa mnaijua katiba ni asilimia ndogo sana ya watanzania, nyinyi ni sawa na wale kenge walio sambamba na msafara wa mamba.
  Nyinyi ni mashabiki wa mabadiliko ya kinafiki na wengi wenu mlikuwepo wakati katiba hiyo ikitungwa na kutolewa kwa mara ya kwanza. Zaidi ya miaka 30 sasa imepita hamkuyaona mapungufu hayo. Hao wanasiasa wanaodai katiba mpya nao ni wanafiki kwa sababu wengi wao walikuwepo wakati katiba hiyo ya zamani ikiandikwa. Jambo hili halihitaji pupa wala papara kama wengi wanavyotaka kwani hata katiba hiyo ya zamani inayo mengi mazuri ambayo hayahitaji kutupwa.

  Kumbukeni kuwa katiba hiyo ilitungwa na magwiji wa wakati huo na kwa mantiki hiyo katiba hiyo inahitaji marekebisho katika baadhi ya vipengele kwani hata hii mpya mnayoidai baada ya miaka 30 ijayo nayo itahitaji marekebisho.
  Mafisadi si matekeo ya katiba bali ni matokeo ya utawala mbovu. Hata kama tutakua na katiba iliyopambwa kwa vidani vya dhahabu bado mafisadi watakuwepo, hawa hawalindwi na katiba bali wanalindwa na uongozi mbovu. Huu ni uongozi ambao sisi watanzania wenyewe kwa ridhaa yetu ndio ambao tumeuweka madarakani.
  Watanzania wote tunayo haki ya kuchangia maoni yetu kuhusu katiba mpya, maoni yetu yatakuwa muafaka baada ya kuipitia na kuisoma katiba ya zamani ili tujue mapungufu yake. Watu wachache bado hawatoshi kuwakilisha maoni ya watanzania wote na ndio maana mwenye kura nyingi ndiye mshindi popote pale duniani.
   
Loading...