Katiba Mpya

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Habari ndugu zangu wapeendwa, leo sina mengi sana ya kuandika hapa kama ilivyo kawaida yangu. kwa kifupi sana nataka kujadili kuhusu madai ya katiba, si vibaya lakini tunapaswa kujiuliza kwanza ni nini tunachokidai katika katiba hiyo.

Nasema hivyo nikiwa na maana ya kuwa, mabadiliko tunayoyadai ni haki ya watanzania wote lakini ni wangapi leo hii aambao wamewahi kuiona na kuisoma katiba hiyo zaidi ya kuisikia katika midomo ya wanasiasa pekee.

Kwa nini kabla ya kudai mabadiliko hayo nguvu zetu tusizielekeze katika madai ya kuchapishwa katiba hiyo ili iwe wazi kwa watanzania wote waisome ili wachangie mawazo yao katika vipengele ambavyo watakuwa hawajalizika navyo ili mabadiliko hayo yachangiwe na watanzania wote.

Tunajua kuwa katiba hiyo inafichwa na kuwa ni siri kubwa kutokana na mapungufu yake. Lakini imefikia wakati sasaa iwekwe hadharani tena iandikwe kiswahili kila anayejua kusoma aisome na kuielewa ndipo tuanze kudai mabadiliko hayo. Tofauti na hivyo tutakuwa tunadai mabadiliko ya kitu wasichokijua mamilioni ya watanzania.
 
Bw Jumakidogo,

Tukifuata huo mchakato ni sawa na kusema kwamba hatutapata katiba mpya. Ukipima kutoka mawazo wanayotoa watu inaonyesha kuna uelewa wa kutosha wa katiba. Hiyo inatosha kuanza kufanyia kazi. Sisi tunaoilewa tuzungumze nao wasioielewa kitanda kwa kitanda na kichwa kwa kichwa. Tuna tasnia ya habari na mawasiliano nao wafanye kazi yao. Uliona juzi kwenye maandamano kulikuwa na kina mama walitoka vijijini kuja kudai katiba mpya! Nadhani tuwe na tahadhali sana hizi sweeping statements kwa mfano kusema watu wengi vijijini hawajui jambo fulani.... ni kama kuwadharau na kuwakadiria chini (to underestimate them) isivyo sawa na ukweli halisi.

Ukiangalia hata nguvu ya mabadiliko ya kisiasa imeanzia wilaya/majimbo ya periphery ndiyo sasa mijini (ambako tungetemea uelewa wa haraka) ndiyo wanaanza kupanda gari la mabadiliko. Wakati wa kutafuta maoni ya kuingia mfumo wa vyama vingi watu wengi walikataa hata mie wakati ule nilikataa, lakini hekima ilitumika, ukweli ni kwamba viongozi akiwamo na Mwalimu (Nyerere) waliona kwamba dunia imebadilika na mfumo wa pluralism katika siasa hauepukiki, wakaamua ni lazima tuingie kwa mfumo wa vyama vingi. Hapakuwa na madhara yoyote. Wala hapakuwa na vurugu kwamba sisi wengi tumekataa na nyie mwalazimisha.

Halafu Mwalimu alijua sisi kukataa mfumo wa vyama vingi ni zao la ujinga tu (adui mojawapo ya wale watatu) na propaganda za mfumo wa chama kimoja walizojazwa nazo wananchi tangia mwanzo. Mfumo tuliokuwa nao haukutupa uhuru wa kujifunza na kudiriki mambo mengine na kutujengea hulka ya uoga (wengi tunaita amani). Watanzania hawana amani wana uoga ni watu ambao wanapenda kukakaa kwenye ukanda wa raha (comfort zone), hawapendi kudiriki wanaogapa matokeo wasioyajua. Wanataka wawe na uhakika wa kila kitu kabla hawajakijaribu. Na Mwalimu alikuwa na akili akang'amua hilo na hivo akituaingiza kwenye mfumo wa vyama vingi.

Swala la katiba ni rahisi zaidi kuliko lile la kubadili mfumo wa kuendesha nchi. Kama tuna viongozi wenye hekima wataelewa kuwa tuendako na katiba hii si sahihi. Kizazi hiki cha sasa siyo cha CCM, ni kizazi kinachoanza kuelewa kuwa ''high risk ina high return pia''. Yasipoandaliwa mazingira ya kuchukuliana na kizazi hiki nchi itaingia matatizo makubwa kwenye miaka mitano hadi kumi kutoka sasa. Viongozi wetu wakiwa na hekima wataelewa kwamba katiba imara na inayozingatia misingi na matakwa ya watu na inayokubalika na watu itaimarisha nchi yetu na kuipeleka mbali kuelekea kwenye neema. Kama watakosa hekima na kuamua kutumia ujanja ujanja tuendelee na katiba inayolinda maslahi ya CCM tu itatueletea matatizo. Kuna wakati atakuja Pharaoh asiyemjua Yusuf hapo ndipo tutakapolia na kusaga meno, asomaye na afahamu!

Tunataka hata akija Pharaoh asiyemjua Yusuf akute misingi imara ya mkataba wa watawala na watawaliwa na hivyo kutokuyumbisha nchi na kutuletea balaa. Sasa tayari kuna vijifarao vingi visivyomjua Yusuf vimeanza kujitokeza japo ni vidogo lakini si dalili nzuri. Na inawezekana kimojawapo kikachukua uongozi wa nchi ......itakuwa balaa mwanangu!

Hekima itumike kuanza mara moja mchakato wa kuandaa katiba mpya tuache visingizio vya oh, watu hawajaisoma iliyopo, Wananchi hawajui hata katiba ni nini na visingizi vingine lukuki. Kenya waliunda jopo la wataalamu wakakusanya maoni kisha wakayaweka kwenye lugha ya kitaalamu baadaye wakaviweka vipengele kwenye lugha ya mtu wa kawaida kuelewa, wananchi wakapiga kura kuikubali au kuikataa. si lazima tufuate mtindo huo. Huwezi kuniambia kuwa wananchi wate wa Kenya walisubiriwa kwanza mpaka waisome ile ya Zamani.

Tuchukue hatua na tuache visingizio,
 
Ahsante sana ndugu na nashukuru sana kwa mawazo yako yenye upeo mpana. Tatizo jingine lipo kwa upande wetu sisi waandishi wa habari, sauti zetu na kalamu zetu huwa hazilengi maslahi ya watanzania bali huwa tukiangalia maslahi yetu sisi pamoja na wale ambao wametuajiri katika magazeti ama redio zao.

Mara nyingi tunaandika vitu ambavyo ni matakwa na misimamo ya waajiri na kujikutaa maoni yetu kuangukia upande mwingine na kuupotosha uma hata kama hatupendi, kama mwenye gazeti hapendi na anapinga mabadiliko ya katiba kwa maslahi yake binafsi wewe muandishi wa chombo chake inabidi uandike habari kutokana na matakwa yake ili usikitie kitumbua mchanga. Hilo ni tatizo kubwa sana ambalo linatakiwa kutafutiwa ufumbuzi mapema. Lakini yote kwa yote ipo siku tutafika katika kilele cha mafanikio kwani tunaambiwa hataa Roma haikujengwa kwa siku moja.

Nakutakia siku njema, mwenza katika harakati
 
Me nimekuelewa vzuri sana.... Ingekuwa vzuri kama hiyo page ingetolewa watu wapate kuisoma na kuacha kupinga masuala ya maendeleo.....

Mfano ni hiyo kauli ya mkono....... Me naanza kuwa na wasiwasi kuhusu akili yake... inawezekana ameanza kuchan¤?*$_wa au ni mgonjwa.
 
Back
Top Bottom