Ulimbo
JF-Expert Member
- Aug 14, 2009
- 3,767
- 4,035
Wana JF, awali ya yote, salaam, na pia niwatakie heri ya krismasi na mwaka mpya 2017.
Siku chache zilizopita Rais Magufuli amemteua mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Themistocles Kaijage baada ya Jaji Damian Lubuva kmaliza muda wake.
Swali ninalojiuliza na ambalo naomba mwenye ufahamu zaidi anifahamishe ni juu ya mambo makuu mawil.
1: katiba mpya.
2: Tume huru ya uchaguzi .
Kipindi kifupi hapa nyuma kulikuwepo na mchakato wa kupata katiba mpya, na fedha nyingi za walipa kodi zilitumika kwenye vikao vya tume iliyokuwa chini ya Jaji Warioba, ambayo hiyo tume ilipendekeza rasimu/katiba pendekezwa, ambayo ilihundiwa mbunge la katiba, ambapo pia kwenye vikao vya bunge la katiba fehda nyingi za walipakodi zilitumika.
Ndani ya katiba pendekezwa kulikuwepo na pendekezo la kuwa na tume huru ya uchaguzi, ambayo tulitegemea kuwa ingeundwa kabla ya uchaguzi uliopita October 2015. Jambo hili halikufanikiwa, na uchaguzi ulifanyika chinin ya tume ambayo haikuwa huru.
Nilitegemea Rais wa sasa angeendeleza mchakato wa kupata katiba mpya, ila kinyume chake yeye alisema katika kampeni zake hakutaja mambo ya katiba, na alichokisema anataka kunyoosha nchi.
Juzi kateuwa mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Je kuna mategemeo kweli ya kupata katiba mpya ambayo itakuwa na tume huru ya uchaguzi au ndo katiba ya sasa itaendelea kutumika hadi uchaguzi wa 2020?
Naombeni mawazo yenu.