Katiba mpya itatukomboa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba mpya itatukomboa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by change we need, Aug 12, 2011.

 1. c

  change we need Member

  #1
  Aug 12, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 81
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tanzania kama inchi nyingine barani Afrika baada ya uhuru ilikuwa katika kipindi kigumu ikipitia katika mfumo wa Kikoloni ambao ulikuwa wa kebapari zaidi, wakati huo huo ikijaribu kujenga mfumo wake na hapo ndipo waasisi wetu walipojiunga katika mfumo wa ujamaa na kujitegemea ili kuweza kujikomboa na kulenga kujitegemea zaidi. Hata TANU ilipoanzishwa ilikuwa na malengo ya mkulima na mfanyakazi ikiwa ni chama cha kuwajali wanyonge kwa masilahi ya Taifa.

  Tumepitia historia nyingi na mambo mengi ambayo wengi wetu tunaweza kuwa tunayafahamu na sina haja ya kuyakumbushia,lakin nikijaribu kuangalia mfumo wetu wa sasa katika serikali yetu chini ya chama cha Mapinduzi ambacho ndicho kinachoongoza serikali sipati uwiano wa malengo yake kama ni kweli kimetokana na TANU.Maadili ya TANU na miiko ya uongozi ambayo CCM ilitakiwa iwe ndo msingi wake nadhani CCM haitumii sera za TANU tena.Sasa hivi CCM si chama cha wafanyakzi na wakulima ni chama cha Wafanyabiashara na matajiri (angalia matatizo ya maji,umeme,mafuta na mfumo wa uongozi ndani ya chama ni masilahi ya kibiashara zaidi kuliko matatizo ya wananchi mikataba mibovu na mengineyo)na serikali inafuata mfumo wa kibepari wakati viongozi wake wakijnadi ni ujamaa na kujitegemea.

  Tunashuhudia maliasili zikiuzwa kwa wageni tena kwa kumilkishwa kwa miaka lukuki angalia kasi ya uuzaji wa ardhi kwa wageni kwa sasa kwa kisingizio cha uwekezaji! hakuna maliasili yeyote ambayo tunajivunia inatusaidia kama ipo wadau mnijulishe mfano, kuanzia mbuga zetu wanyama wanavyochukuliwa na mpaka sehemu nyingine mbuga zimeuzwa(Loliondo) madini yametapakaa kila sehemu lakin nenda huko kwenye mikoa inayotoa madini maisha mabaya na hakuna kitu kinendelea,mashirika yetu na mali zetu kibao zinaliwa na wageni, ukija kwenye kazi sasa hivi nchi inachukua makampuni ya nje tu kwa kazi kubwa kisa?

  Wazawa hawana uwezo je ni kweli? inamaana hatuma wataalamu? lakin ukiangalia ni kuwa wazawa hawana uwezo wa kutoa hongo.Mfumo wa serikali sasa ni mgumu sana kwani hakuna watu wanojituma wala kuwajibika kwa masilahi ya Taifa kama wapo ni wachache sana kila mtu kama amekata tamaa, nenda kwenye huduma za serikali uone hali ilivyo! utoaji huduma hauridhishi watumishi hawajitumi na n.k. ukiangalia mambo mengi yanachangia masilahi duni, mazingira mabovu ya kazi na hakuna vitendea kazi bajeti zinazopitishwa ni 20% au 30% tu ndo zinatekelezwa,fuatilia utakubaliana na mimi.

  Kila mwaka mambo yaleyale na hayaishi kwa vile hayatekelezwi.Viongozi wa chama na serikali wanajinufaisha kulingana na nafasi zao kuna mengi hatujui hata Mzee wa vijisenti aliposema hivi ni vijisenti alikuwa na maana yake kuwa kuna watu wana hela katika nchi hii ila munamshangaa yeye kumiliki kiasi kidogo!

  Hivyo kama watanzania tunatakiwa tuangalie kwa makini nini kinaweza kutukomboa kutoka kwenye mfumo huu tulionao!Tupiganie katiba mpya ambayo inaweza kutusaidia kulinda mali zetu na kuwabana viongozi mafisadi wanaoitafuna nchi hii.
   
Loading...