Katiba Mpya Ipi?

Baija Bolobi

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
1,093
1,726
Katika mjadala unaoendelea kuhusu hali ya utendaji wa JPM, kuna sauti zinasikika zikidai kuwa ili aweze kutekeleza maono yake vizuri aharakishe katiba mpya. Yeye amesikia kuwa mchakato ulifika pazuri na imebakia yeye kumalizia. Nina maswali kuntu hapa:

1. Hivi katiba mpya inahitajika? Ile inayopendekezwa na BMK au nyingine?
2. Je hii inayopendekezwa ina tofauti sana na hii iliyopo kiasi cha kumpa nafuu?
3. Ni njia gani ya kufufua mchakato huu ambao kisheria umepitwa na wakati?
4. NEC imesikika kuwa ina fedha na kilichobaki ni kura ya maoni tu?
5. Matumaini ya katiba mpya yakikwamishwa na hiyo kura itakuwaje?

Wajuzi tusaidie hapa.

--Baija
 
Kwa namna tulivyomsikia Magu alivyokuwa anaongea siku anakabidhiwa ripoti ya NEC ya Lubuva, kwa kusema ataendeleza pale alipoishia Kikwete, ni kama alimaanisha kuwa kilichobaki ni kwenda kupiga kura ya maoni ya Katiba pendekezwa ya Lumumba.

Kwa maana hiyo pamoja na kuwa kwenye tukio hilo alimpamba Warioba kwa mgongo wa chupa kwa kumsifia kwa kazi kubwa iliyozaa Rasimu ya Katiba ya maoni ya wananchi, lakini kiukweli Magu naye anaelekea kufuata nyayo za Kikwete kwa kuamua kuendelea kuitupa kwenye 'dust bin' Rasimu iliyotokana na maoni ya wananchi.

Mbaya zaidi Magu ameendelea kueleza kuwa yapo maoni yatakayokuwa 'added'.

Lakini hakufafanua maoni hayo yatakuwa added kivipi.

Upo uwezekano kuwa maoni hayo yatakayokuwa added nayo yatatoka mtaa wa Lumumba!

Kwa kuwa kwa mwendo tunaokwenda nao ingawa theoretically tupo kwenye murtypartism, lakini practically ni kama tupo kwenye mfumo wa Chama kimoja....
 
Agreed. Rasimu inayotegemewa kupigiwa kura ilipitishwa na chama kimoja, ilipigiwa kura kura na marehemu, na pia wabara walipiga kura wakahesabika ni Wazanzibari ili kukidhi madai ya kikatiba. Wapo waliodaiwa kutuma kura kutokea Mecca, lakini walikuwa kukana kuwa hawakuwahi kutuma kura zao.

Linapokuja hili tamshi la Magu kuwa kuna mambo yatakuwa added, unashtuka atayaongeza vipi? Bunge lile liliishavunjwa, tume ilivunjwa, na timeline ya shughuli ilifika mwisho kwa sababu sharia ile ilikuwa inataja mpaka muda wa tukio moja kwenda jingine.

Kwa maoni yangu, unahitajika muafaka wa kitaifa kuendelea na jambo hili bila kuonekana ni tunda la chama kimoja.
 
Bufa waweza kuwa sahihi. Kipimo halisi cha kuona kama katiba mpya inaweza kusaidia, ni kwa kuangalia kama iliyopo inaheshimiwa na watawala. Viongozi wanapoamua kuchagua kipi waheshimu na kipi waache inatia mashaka. Ebu fikiri, kwa suala la Zanzibar mtu anakuwa mnyenyekevu kabisa kuwa "hawezi kuingilia", "katiba haimpi nafasi", n.k. Lakini mtu huyo huyo anasimama na kubana msuli kwa kusema anapiga marufuku shughuli za kisiasa nchini mpaka 2020! Au mtu huyo anayeheshimu katiba kwa suala la Zanzibar, anamteua mtu kuwa mbunge, halafu anamteua kuwa Waziri, kisha anamwapisha kuwa waziri kabla hajaapa kuwa mbunge!

Katiba mpya inaweza isitusaidie kama watawala bado wanakuwa juu ya sheria. Ingesaidia kama kungekuwa na taasisi na mihimili yenye nguvu kumwajibisha rais pale anapokwenda nje ya msitari.
 
It is very true.

Ni muhimu tukapata Katiba ambayo itampunguzia madaraka makubwa Rais, yakiwemo ya uteuzi mbalimbali wa nafasi nyingi za utendaji serikalini.

Tukumbuke Mwalimu enzi za uhai wake aliwahi kusema kuwa Katiba tuliyonayo inampa madaraka makubwa sana Rais, akaendelea kusema kusema kuwa tuendelee kumwomba Mungu asitokee Rais atakayechaguliwa mwenye elements za udikteta.

Akahitimisha kuwa iwapo nchi 'itapotea' step na kuchagua Rais mwenye harufu ya udikteta kwa Katiba tuliyonayo itakuwa ni disaster.....
 
Ebu imagine, kila wiki kuna tangazo la "Rais Kamteua Fulani". Sidhani kama hata anawafahamu wote anaowateua. Matokeo yake, hii inageuka kuwa biashara nzuri sana ya wale wanaofanya kazi ya kuchunguza watakaoteuliwa. Bingo linaweza kukuangukia ukiwa baa ukaona mtu anasogelea meza yako na kukuambia E bwana eh, nipe CV yako! Halafu in a week unasikia so and so kateuliwa kuwa "mwenyekiti wa wanaokesha baa".
Institutions ziwe na mechanism ya kuteua watu wake na nyingine rais ateue lakini aweke kiti moto kutetea uteuzi wake mbele ya vyombo Fulani. Haya hayamo kwenye "Katiba pendekezwa".
 
Back
Top Bottom