Katiba mpya inadawai kinyemela nyemela

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,873
Huwa nikifika hatua ya kuwaza,vyama pinzani TZ napata shida saana.

Anaandika
Abdul Nondo.

Chadema kinasemea mashariki,ACT magharibi,CUF kule, CUF nyingine huko,NCCR huko ,huyu twitter huyu fb ,huyu kalalamika huyu amelaumu .

Civil societies huko ,LHRC at least ila zingine huko ,viongozi wadini kule.

Nashauri kitu vyama pinzani visiwe kama havijui wajibu wao ,vyama pinzani wanawajibu wa kufanya vitu formally, fanyeni .wanataka waanze Fanya vitu kwa kuzima moto 2019 now ndio muda.

Kenya walipokuwa wanadai mambo kadhaa kipindi cha MOI 1994 kuendelea walikuwa formal ,waliamini kabisa kuwa hakuna kitu ambacho serikali inaweza Fanya kwa kila MTU kusemea kwenye tundu lake ,vyama kama FORD ASILI chini ya Matiba ,Kenyan National congress chini ya Rubia ,FORD Kenya ,na Democratic party ya kibaki walitaka mabadilko ya katiba na mabadiliko ya sheria ya uchaguzi njia ya kudai haki zao ,waliungana wakawa kitu kimoja ,wakaungana na taasisi za kidini Catholic church,pia taasisi binafsi Kenyan human rights commission, Kenyan law societies,na ICJ .

Angalau kwa umoja wao serikali iliitisha mpango wa kwanza mchakato wa katiba mpya 1995,mnakumbuka umoja wa UFUNGAMANO coalition,juu ya katiba muungano wa asasi,vyama na asasi za kidini kudai katiba ,mnakumbuka tume zilizoundwa chini ya UFUNGAMANO inaitwa The people's commission of Kenya) chini ya OKI OOOKO dhidi ya tume ya serikali CONSTITUTION OF KENYA REVIEW COMMISION ,hatimaye serikali iliomba kufanyike maridhiano kuwe na tume moja.

Mnakumbuka NAARC(National Rainbow coalition) umoja huu ndio uliyoitoa KANU 2002 ,mnakumbuka.

Ninachotaka kusema hapa upatikanaji wa katiba unahitaji akili kubwa,umoja wa hali ya juu.sababu mtawala yeyote huwa anapenda sheria zinazompa nguvu hiyo ni kawaida.

Hata iingie CHADEMA madarakani Leo ,au ACT iingie Leo haiwezi shadidia katiba kama inavyoshadidiwa Leo sababu itakuwa inakwenda kupunguza nguvu hakuna mtawala anapenda(Msome Nicole Machievel ,Prince).pia hii ilitokea kwa Mwai kibaki ktk uongozi wa Moi alikuwa anapiga kelele juu ya katiba ,alipoongana Kuwa NAARC coalition, uchaguzi 2002 akashinda dhidi ya Uhuru kenyatta akawa Rais akawageuka akina odinga ,Katiba ikaingizwa mambo ya hovyo 2005 ktk kura ya maoni (referendum 2005) ilikataliwa.

Hivyo swala la katiba ni nzito kuelekea 2020 ,ila linafanywa na kuratibiwa disorganizedly,roughly kila MTU ni msemaji,mlalamikaji .

kila MTU anasema mitandaoni kivyake ,madhabahuni ,yule ofisini kwake kwa muda wake ,hiyo ktk media ,hakuna serikali inayoweza kusikia kwa njia hizo yaani hiyo ni kawaida kwa serikali zote.

Ila kama vyama vya siasa CHADEMA,ACT,CUF,NCCR vitaamua kufanya lobbying kwa Civil societies, (NGO'S), INGOS, (yaani taasisi binafsi),viongozi wa dini wakaingia Muungano wa pamoja ,kuchagua mwenyekiti wa umoja huo ,wa vyama vya siasa pinzani,viongozi wa dini ,asasi binafsi na makundi mbalimbali mkaanza kubaliana mnataka nini hasa!

Mkakubaliana kuwa katiba ibadilishwe,mkatoa elimu kwa jamii why katiba inahitajika,makaanza Fanya lobbying kupeleka madai serikali rasmi ya kudai katiba.movement ikawa hot na kubwa .

Ila kwa njia ninazoziona hapa maana akiongea mmoja anaonekana yy mbaya,akiongea pastor au padre Fulani anaonekana mchochezi ,akiongea taasisi LHRC inaonekana ya kichochezi ,Akiongea Prof.Lwaitama anaonekana mchochezi ,akiongea zitto anaonekana mchochezi .Ni lazima muonekane wachochezi sababu mmesimana individually na disunited,disintegrated.

Hiyo sio njia sahihi ya kudai jambo nyeti kama hili linahatarisha kupunguza nguvu ya watawala ,sio Kwa Pres.Magufuli ni kwa marais wote ,kikwete mwenyewe alikubali sababu alijua anamaliza muda wake ,hili jambo ni zito.tujiangalie tena na tujitathimini.

Abdul Nondo
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom