Katiba mpya hoye

Yaani hata katiba nayo yahitaji kampeni...

Upotevu wa fedha huu...
 
daa yani nchi hii kila kitu ni fulsa tu ya kumimina minoti tu
 
Hivi ikitokea mtu mwingine akachapisha Kofia kama hizo na kuandika KATIBA MPYA HAPANA watamfanyaje.?? Na je kama nembo ya taifa imeisha tumika hapo kuna sababu ya kufanya uchaguzi. Mi nijuavyo ni kwamba hii nembo hutumika kufanya kapeini pale ambapo hakuna chaguzi. Mf. Kampeni za ukimwi kifua kikuu Ebola bk.
 
Nafasi nyingine hiyo kutafuna pesa ya umma!!!!


Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
...nasikia wanajeshi wanapelekwa Zanzibar kukamilisha akidi, dadeki walai...
 
Reactions: BAK
lazima ufanyike uharamia wa hali ya juu na hawa Mainterahamwe kama uliofanyika wakati wa kikao cha posho kuchakachua maoni ya Watanzania.

...nasikia wanajeshi wanapelekwa Zanzibar kukamilisha akidi, dadeki walai...
 

Upo sahihi mkuu, ni nani mwenye mamlaka na hii nembo ya Taifa? Hebu learned brothers (lawyers ) njooni mtusaidie juu ya hili.
 
Huo upuuzi (kofia) umetengenezwa kwa fedha za serikali au za chama? Kama ni za chama its ok,ila kama ni za serikali ni mwendelezo wa kutafuna fedha zetu kiholela tu
 
Walishaona wabongo ni watu wa kudanganyika kwa kofia na tshirt!!!
 
hapo wakiweka kofia ya rangi ya kijani nitakuwa wa kwanza kuinunua
 
Yaani badala ya kutugaia hiyo katiba pendekezwa wanatupa kofia??kweli???sijui wanatuonaje???sema hapana katiba ya Chenge!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…