22.-(1) Ardhi ndiyo rasilimali kuu kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi,
kijamii na ustawi wa nchi na watu wake wote. Serikali ya Jamhuri ya Muungano
itaweka mipango bora ya matumizi endelevu ya ardhi kwa faida ya kizazi
kilichopo na vizazi vijavyo.
(2) Ardhi yote itamilikiwa, itatumiwa na kusimamiwa kama
itakavyoainishwa na sheria itakayotungwa na Bunge kwa kuzingatia misingi
ifuatayo:
(a) raia wa Tanzania pekee ndiye atakayekuwa na haki ya kumiliki
ardhi ya Tanzania, na haki hiyo italindwa kwa mujibu wa Katiba hii;
(b) mtu ambaye siyo raia wa Tanzania atakuwa na fursa ya kutumia
ardhi kwa ajili ya uwekezaji na maendeleo mengine ya kiuchumi na
makaazi;
(c) haki ya kumiliki, kuendeleza na kuhifadhi ardhi kwa ajili ya
makundi mbalimbali ya jamii wakiwemo wakulima, wavuvi,
wafugaji na makundi madogo itatambuliwa na kulindwa kwa mujibu
wa Ibara hii; na
(d) kila mwanamke atakuwa na haki ya kupata, kumiliki, kutumia,
kuendeleza na kusimamia ardhi kwa masharti yaleyale kama ilivyo
kwa mwanaume.
Nimeipitia katiba kipengere kwa kipengere.
Hakika imekaa vizuri sana. nimekuwa nikijiuliza wale wanaoipinga wanapinga kwa hoja zipi!!?
Ailimia kubwa mambo yaliyopendekezwa na tume ya Warioba yamo.
Eti kwa sababu tu kwamba serikali tatu haipo.
Asilimia kubwa ya watu wanaisoma kwa mrengo wa kuipinga. Hawako na free mind.
Kuna mambo mazuri sana mengi. Mfano:
Na kuna mambo mengi sana nitaendelea kuya toa.
119.-(1) Kutakuwa na Serikali za Mitaa katika kila mkoa, manispaa,
wilaya, mji na kijiji katika Jamhuri ya Muungano ambazo zitakuwa za aina na
majina yatakayowekwa na sheria itakayotungwa na Bunge au na Baraza la
Wawakilishi.
(2) Madhumuni ya kuwepo kwa Serikali za Mitaa ni kugatua madaraka
kwa wananchi ili kuwapa haki na mamlaka ya kushiriki katika mipango na
shughuli za utekelezaji wa maendeleo katika sehemu zao na nchini kote kwa
ujumla.
(3) Bunge au Baraza la Wawakilishi, kwa kadri itakavyokuwa, litatunga
Sheria, pamoja na mambo mengine itakayoweka miundo ya mabaraza na
wajumbe wake, taratibu za uchaguzi, mamlaka, majukumu na kazi za Serikali za
Mitaa.
Usilete ushabik kwa mfumo uliopo wa serikali mbili hayo mambo hayawez kutekelezeka labda arudi masia" kwa utitiri wa wabunge 360 na makamu wa raisi watatu kwa budget ipi watz ebu zindukeni kutoka ucngizini hizi sanaa tu
wewe nenda taratibu soma Ibara ya 20 (2) tatizo lenu mnakurupuka sana! hamsomi as a whole!!
Hii katiba haifai kabisa.
SURA YA PILI
MALENGO MUHIMU, MISINGI YA MWELEKEO WA
SHUGHULI ZA SERIKALI NA SERA ZA TAIFA
11.-(1) Lengo la Katiba hii ni kulinda, kuimarisha na kudumisha,
haki, usawa, udugu, amani, umoja na utangamano wa wananchi wa Jamhuri ya
Muungano kwa kuzingatia ustawi wa wananchi na kujenga Taifa huru lenye
demokrasia, utawala bora, maendeleo endelevu na kujitegemea.
(2) Bila kuathiri masharti ya ibara ndogo ya (1), lengo hilo kuu
litaendelezwa na kuimarishwa katika nyanja zote kuu, ikijumuisha
nyanja za kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na kimazingira.
(3) Bunge litatunga sheria itakayofafanua juu ya utekelezaji wa
malengo muhimu kwa mujibu wa Katiba hii.
Unatakiwa uisome na utoe comment sio kuleta porojo mimi hapa natoa yaliyomo kwenye katiba wewe unaleta bra bra tu.
21.-(1) sera ya mambo ya nje ya jamhuri ya muungano
inalenga na kuzingatia maslahi ya taifa na mamlaka kamili ya nchi na
kwamba sera hiyo inatekelezwa kwa uwazi ili:
(a) kukuza ujirani mwema, ushirikiano wa kikanda na wa
kimataifa;
(b) kukuza maendeleo na ushirikiano wa kiuchumi wenye tija kwa
taifa na raia wake;
(c) kuunga mkono na kuendeleza jitihada za kuimarisha umoja
wa afrika, sera ya kutofungamana na upande wowote, na
kukuza ushirikiano na nchi zinazoendelea duniani;
(d) kuheshimu sheria za kimataifa;
(e) kuzingatia mikataba ya kimataifa na ya kikanda yenye maslahi
kwa jamhuri ya muungano na kutatua migogoro ya kimataifa
kwa njia ya majadiliano, usuluhishi, maridhiano au
mahakama;
(f) kukuza, kulinda na kuzingatia haki za binadamu na uhuru wa
watu;
(g) kupambana na makosa ya kimataifa ya jinai; na
(h) kuheshimu uhuru wa mataifa mengine.
(2) bunge litatunga sheria, pamoja na mambo mengine,
itakayoelekeza na kusimamia utekelezaji wa sera ya mambo ya nje.
Hayo ndiyo uliyoaona mazuri. Je,Nimeipitia katiba kipengere kwa kipengere.
Hakika imekaa vizuri sana. nimekuwa nikijiuliza wale wanaoipinga wanapinga kwa hoja zipi!!?
Ailimia kubwa mambo yaliyopendekezwa na tume ya Warioba yamo.
Eti kwa sababu tu kwamba serikali tatu haipo.
Asilimia kubwa ya watu wanaisoma kwa mrengo wa kuipinga. Hawako na free mind.
Kuna mambo mazuri sana mengi. Mfano:
Na kuna mambo mengi sana nitaendelea kuya toa.
Hapo ndio unapo shindwa kuelewa mantiki ya katiba hii. Ngoja nikukumbushe kitu kimoja tu..... Na Wala Hakuna Uzuri Wowote Hapo, Uvundo Tu. Mfano, Ardhi Ni Suala La Muungano? Mbona Lipo Kwnye Katiba Ya Tanzania.
Hayo ndiyo uliyoaona mazuri.