Dotto C. Rangimoto
JF-Expert Member
- Nov 22, 2012
- 1,985
- 1,285
KATI YA ZITTO NA ANNA MGWIRA NANI BIG BOSS?
KIONGOZI WA CHAMA
Kuhakikisha itikadi, falsafa na sera za chama zinakufikia popote ulipo na unazielewa kabla ya kuamua kuzikubali na kujiinga na ACT.
MWENYEKITI
kuhakikisha chama kinatunga sera zake kwa kuzingatia itikadi na falsafa ya chama, lakini kuhakikisha serikali, wabunge, madiwani na wenyeviti wa mitaa, vijiji na vitongoji wanatekeleza matarajio ya wapiga kura.
KATIBU MKUU
Kuhakikisha kiongozi wa chama na mwenyekiti wa chama hawayumbi katika kutimiza majukumu yao kama nilivyo yayaja hapo juu.
NANI MKUBWA KATI YA KIONGOZI WA CHAMA NA MWENYEKITI?
Katika ACT hatuzingatii nani mkubwa bali tunachozingatia uongozi ni majukumu na si vinginenvyo. Kwasababu hiyo basi, sisi huku hakuna waheshimiwa, bali sisi sote ni ndugu na mbora kati yetu si yule mwenye majukumu makubwa ya kiongozi kwa mujibu wa katiba bali ni yule anayejitoa kwaajili ya chama chetu kwa hali na mali.
Pamoja na hayo, naomba nikuchoree picha kwa chama cha CCM na CHADEMA, na kwa picha hiyo huenda itakuongoza katika kumjua BIG BOSS wa ACT kwa wewe unayetaka kumjua.
Kwa mfumo wa nchi yetu chama ndio hudhamini serikali na viongozi wote wa kisiasa nchini wanaotokana na kura za wananchi. Ili uwe rais, au mbunge au diwani ni lazima udhaminiwe na chama cha siasa. Kama ndivyo nini hasa wajibu kwa chama cha siasa kwa serikali au mbunge aliyemdhamini?
MOSI.
Wakati wa kampeni, chama kina wajibu wa kuhakikisha huyo mtu aliyemdhamini anashinda, na katika kufanya hivyo chama kinabeba jukumu la kuuza sera zake na sifa za watu ambao wataenda kuzitekeleza hizo sera.
PILI.
Chama kikishinda ni jukumu lake kuhakikisha watu waliowadhamini hawaendi kinyume na matarajio ya wapiga kura. Mtu anapokupa kura kuna mambo ambayo anayataraji kutoka kwako, na unaposhinda anataka alione lile alilolitaraji ili uchaguzi mwingine akupe kura tena. Hivyo chama kinatakiwa kiwe kikali kwa serikali iliyotokana na watu wake au kwa wabunge wake ili kisipate tabu kuuza sera uchaguzi ujao.
MGONGANO WA VYAMA VYETU.
Kama sitakosea, mkutano mkuu CCM uliofanyika mwaka 2012 Dodoma, pamoja na mambo mengine ulikuwa unapokea ripoti ya utekelezaji wa ILANI YA CCM 2010/2015.
Mwenyekiti wa kikao kile alikuwa ni Jakaya Kikwete, na kiongozi mkuu wa utekelezaji wa ILANI hiyo ni Jakaya Kikwete ambaye kipindi hicho alikuwa rais. Hivi mjumbe gani wa mkutano mkuu angeweza kuikosoa ripoti ile kwa nguvu zake zote na kwa moyo wake wote?
Mwenyekiti wa CHADEMA ni Mbowe na kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni ni Mbowe. Kama mtakumbuka CHADEMA katika uchaguzi wa mwaka 2010 ilidhamiria ikiingia madarakani itaachana matumizi ya anasa na posho za kikao.
Katika kutekeleza hilo Mbowe alikataa kutumia gari alillopewa kama KUB na Zitto Z Kabwe akaacha kuchukua posho, lakini baadae Mbowe akaenda kuchukua gari kinyere na suala la kukataa posho likawa ni la Zitto na si la chama tena.
Katika vikao vya CHADEMA vya kujadili shughuli za kambi rasmi ya upinzani bungeni vinaongozwa na Mbowe kama mwenyekiti, mtu ambaye kimsingi ndio wa kuhojiwa na timu yake yote bungeni. Hivi ni nani katika kikao anaweza kuthubutu kusema wenzetu mliopo bungeni mmetuangusha?
ACT WAZALENDO.
tumetenganisha majukumu ya kukiongoza chama na majukumu ya kiutendaji au uongozi wa ofisi za serikali. Kwa kifupi tunaweza kusema tumetangenisha kati ya DOLA na CHAMA.
Ndugu Zitto kama kiongozi wa chama jukumu lake ni kuhakikisha wabunge, madiwani na wenyeviti wa ACT wanatekeleza majukumu yao kwa kufuata miongozo ya ACT.
Ndugu Anna Mghwira jukumu lake kuhakikisha ndugu Zitto na timu yake wanabaki katika mstari wa chama. Yeye kama mwenyekiti wa chama ndio ataongoza vikao vyote ambavyo ndugu Zitto atakuwa anatoa ripoti za utekelezaji wa sera za chama na maazimio ya chama kwa serikali ya ACT, wabunge wa ACT, nk.
Hapa ndipo unapoonekana umuhimu wa uhuru wa chama kuiisimamia serikali na wabunge wake, na kwasababu ni chama ndio kitaomba kura katika uchaguzi ujao, ni vema kihakikishe watu walioshinda uchaguzi uliopita hawaendi kinyume na matarajio ya wapiga kura na kiongozi yeyote ambaye atashindwa kukidhi matarajio hayo ni lazima chama kimshughukie kabla ya wapiga kura hawajachukua hatua za kukiadhibu chama.
Huenda bado wajiuliza, kati ya KIONGOZI wa ACT na MWENYEKITI wa ACT nani mkubwa. Kama bado soma tena majukumu ya watu hao wawili kama nilivyo yafafanua huenda utaelewa nani mkubwa, kwangu mimi, mwenyekiti ndio mwenye chama na ndio mkubwa, kama bado hujaelewa msome Thabo Mbeki wa South Africa na figisufigisu za ANC.
Njano5
whatspp/call 0622845394.