Kati ya wawekezaji na serikali ya CCM mwizi ni nani ?

Mkwawa

JF-Expert Member
Jun 8, 2011
1,334
1,465
Kazi ya serikali kubwa ni kulinda na kutetea masilahi ya nchi na wananchi wake muda wote.

Tatizo kubwa la sisi watanzania tunapenda mijadala rahisi na mihemuko.

Tanzania ni nchi tajiri sana- ila tumeamua wenyewe kuibiwa.

Hii mikataba ya kiwizi imebarikiwa na viongozi wa serikali kuanzia mabaraza yote ya mawaziri tangia enzi za Mkapa, Kikwete, Mwinyi - kwa yeyote aliyekuwepo kwenye haya mabaraza ya mawaziri ana hatia sawa na Acacia.

Hawa watu wote wamekula fedha haramu za uwekezaji tanzania kuanzia IPTL, Gas, Madini, NCCF, Loliondo gate, nyumba za serikali , etc.

Tusipo fumua sheria kuanzia katiba ya nchi, mikataba yote nchini na kuweka sheria kali za kulinda mali asili zetu tutakuwa tunacheza ngoma za tumbili.

Ndio tunaibiwa , tumeibiwa na tunaendelea kuibiwa kwasababu sisi ni wajinga na tunaongozwa na wajinga. tunapenda sana kushangaa na ku tumia mihemuko kwenye mambo magumu.

Nasubiri kuona............................................................................
 
Subiri matusi yao.....
 
Niliwahi kumsikia Jaji Werema akiwa AG, akidai ktk kipindi cha DK 45 ITV kuwa mikataba hiyo ni mibovu na ni mibovu kweli. Lakini eti waliikubali kwa sababu eti walilazimika kuwabembereza wawekezaji ambao hawakuwa na nia ya kuwekeza hapa kwetu. Hivyo wawekezaji wakatoa masharti magumu nao wakakubali. Awamu ya tatu na nne wameingia mambo haya kwa kujua wananchi uelewa wetu ni mdogo na hatuwezi kufanya lolote

Viongozi wetu wanaamini wanaamini utajiri wa nchi hii ni mali yao na ndiyo maana wanafanya wapendavyo eg Ni mwaka juzi tu wabunge wetu wametumika vibaya kupitisha sheria ya Gas na mafuta usiku wa manane kisa tu kumridhisha boss aliyekuwa anamalizia muda wake, atoke ameweka dole.

Nidhamu ya wabunge wa CCM kwa viongozi wao ni kaburi kwa taifa hili.
 
Huyu anayejifanya kuumizwa na wizi huu

1. Hataki mikataba iwekwe hadharani idadavuliwe

2. Hataki kabisa kusikia tunapata katiba mpya ambayo ingekuwa dawa kwa hili tatizo

Najiuliza Magufuli anania ya dhati kweli au mbabaishaji?
 
Eee mungu,IUWE CCM na ikikupendeza pamoja na viongozi wake walaghai ili na wafuasi wake waamke tuijenge TANZANIA yenye neema,itakayowapa ZANZIBAR wanachokipenda zaidi ili basi TANGANYIKA na Unguja tuwe ndugu wa damu wa HISTORIA.ameen ameeen ameeen.
 
CCM ni MAJIZI,yamekula 10% kwenye kila mkataba,yanahangaika kukataana tu sasa.
CCM tujitafakari nchi ni yetu sote kuna watu wana ushauri mzuri sana kwa mustakabali wa nchi tusiweke pamba kwenye masikio tuwasikilize tuchukue hatua
 
Huu wizi umeanza kitambo sana na ndiyo maana ccm kazi yao kubwa ni kupiga vigelegele bungeni wakijua fika kwamba mgao wao umeshatengwa.

Hapa tusipotezeane muda mwizi ni ccm hakuna kumlaumu Muhongo ili ccm ipone hilo sikubali. Muhongo hawezi kutumika ili ccm ibaki salama huu mchezo umetosha kaeni pembeni.
 
Ccm ni wezi. Na kuhakikishia hawawezi kubadili hizo sheria walizozipitisha kuwanufaisha wawekezaji,hawatobadilisha na kuweka mikataba ya madini,mafuta na gesi hadharani.
Na hawatobadilisha katiba.
Hapa Magufuli anatafuta sifa tu na hatofanya chochote.
 
Mambo mengine yanatia hasira sana. Hivi bado wanajiita watetezi wa wanyonge wa Tanzania kwa makosa yao?
 
Mungu kwa upendo wake awapa mali na wao bila kujua kuwa wayafanyayo sio sahihi hawakukoma wakaendelee kuyafanya,alitokea msamalia mwema akawauliza ni kwa nn unafanya hayo?(lissu)wakamwambia hayakuhusu,tulipata bure tunatoa bure.
Lissu,akawauliza tena mnajua mfanyalo,wakamjibu hata tukijua ww hayakuhusu.
Baada ya miaka kumi na kenda alichowaambia(lissu) wanajiuliza mnakumbuka tuliulizwa na kushauriwa?

Kwenye hili mm nimejifunza jambo moja na dogo sana kusema bdiyo au hapana.kama mko 25 mnataka kuhalalisha jambo mkaanza kuulizana wangapi wanasema ndio na wangapi wanasema hapana.ukishafanya hivyo na kupata uhalali wa liwe lililotakiwa waulize hao waliosema hapana ttz lao nn,kama utakubaliana na waliosema ndiyo athari utaiona baadae.
Pale bungeni ndiko tulikoumizwa hawalitetei taifa bali wanatetea chama na chama ndicho kimeunda serikali.Ninavyoamini mm hii ni sehemu rasilimali za tz.tusubiri kushuhudia mengi sana.

Maoni yangu nikiwa nimeguswa na hili na vile ninavyowaona wtz.wavyohangaika na maisha,wtz tungepata viongozi tz.ni zaidi ya libya lkn ona,
Unga seme bei 2600
Mchele 2000/2500
Dona 1500
Nauli 650
Bahati mbaya ukiumwa ndio basi tena ni kelele na madoct.kuwa ni wezi kumbe ww ulishaibiwa kwenye mikataba iliyopitishwa na uliowachagua(wabunge)
 
Back
Top Bottom