Kati ya wanawake 10 waliopo kwenye ndoa; 6 kati yao wanacheat nje ya ndoa

Ngambako

JF-Expert Member
Dec 27, 2013
315
263
Habari ya asubuhi wana jamvi,

Kwanza kabisa naomba kutoa angalizo kuwa utafiti huu nilioufanya kwa takribani miezi miwili ilopita ni utafiti huru na usichukuliwe kwa mlengo wowote huo; dhamira ya tafiti hii ni kuifanya jamii iamke juu ya kuimalisha kwa mahusiano yaliyomo ndani ya familia zetu.

Kama kichwa cha habari kisemavyo; dhamira ya tafiti hii ilikuwa na lengo la kuibua na kuona kwa nini kwa takribani miaka ya hivi karibuni kumetokea ongezeko kubwa la watu waliopo kwenye ndoa kulalamika na hata kufikia kutoka nje ya ndoa na kuanzisha mahusiano mengine mbali na yale anayoendeleana nayo.

Mtafiti katika tafiti hii ametumia respondents halisi ili kupata picha kabili, na ifahamike kuwa utafiti huu umefanyika katika mikoa 5; Dar, Arusha, Mwanza, Iringa na Mbeya. Jumla ya respondents 50 kwa maana ya kuwa 10 kutoka kila mkoa walihusishwa kwa utafiti huu.

Kama nilivyotangulia kusema; utafiti huu ni halisi na sio wa kutunga au kubashiri, mtafiti aliweza kutumia main respondent mmoja (mwanaume) ambae ndio alitumika kuhusika moja kwa moja kwenye kufanya utafiti huu.

Utafiti huu ulihusika kwa main respondent (mwanaume) kujaribu kuwatongoza wanawake 10 kutoka kila mkoa, na endapo kama amefanikiwa basi alitakiwa kumalizia zoezi la kulala na wanawake hao kwa nyakati tofauti.

Uchanguzi wa sample size ulifanyika "kiholela" bila kujali aina ya mwanamke atakaekutana nae ambaye ni lazima awe mke wa mtu.

Tafiti inaonesha kuwa kila wanandoa wanawake 10, sita kati yao walikuwa wanakubali kutoka na kulala na respondent hiyo, tafiti ilienda mbali zaidi na kuangalia kwa nini wanawake waliopo kwenye ndoa wamekuwa ni rahisi zaidi kutoka nje ya ndoa ni kuwa; wengi wao asilimia 52 wamedai kuwa wanaume wao hawawaridhishi katika kuwapa haki yao ya ndoa; asilimia 12 wamesema kuwa wamegundua wanaume wao kuwacheat na wao kupelekea kurevenge, asilimia 16 wamesema kuwa waume zao wapo busy kiasi kwamba wanakosa haki ya ndoa, asilimia 14 wamesema kuwa waume zao wapo mbali na familia kwa kipindi kirefu hari inayopelekea wao kutoka nje ya ndoa na asilimia 6 wamesema wao ni tabia yao wanajisikia kuwa na mwanaume wengine mbali na mme wa ndoa.

Mtafiti aliona ni vyema kutoa angalizo kwa wanandoa, wote waume na wanawake kutokana na sababu mbalimbali zilizoelezwa na wahojiwa (respondents).

Nawatakia wakati mwema nyote
 
Sample size ni ndogo sana kuweza kutumika na kuaminika. Kiwango cha chini ni 30 na sio 10. Utafiti mufilisi huu
 
You don't need binoculars to see this.
Reference ya ripoti za TACAIDS zinaonyesha wazi uaminifu katika ndoa ni ndogo Sana.
Ndio maana watu wamekaa sababu za kwanini wana cheat.
Sample space yako unaweza sio toshelevu kutoa majibu ila response ya waliohijiwa unaweza kukuonyesha hali ilivyo.
 
Sample size ni ndogo sana kuweza kutumika na kuaminika. Kiwango cha chini ni 30 na sio 10. Utafiti mufilisi huu

Inawezekana sample size ilikuwa zaidi ya hiyo. Yeye amesema tu kuwa kati ya kumi, sita walitoka nje ya ndoa zao. Inawezekana alifanya utafiti kwa wanawake 1000, akapata 600 kati yao sio waaminifu, au alifanya kwa 100, akapata 60 sio waaminifu. Hapo muhimu ni ratio 3:5...6:10;....9:15 au hata 600:1000, haijalishi. Labda tumuulizeml mleta mada idadi ya waliohojiwa.
 
Huo utafiti ulienda mbali kiasi cha kuonyesha hao wanawake walipo kwenye ndoa wanatoka nje ya ndoa na wanaume wa aina gani? Namaanisha na wao wapo kwenye ndoa au hawajaoa? Isije ikawa tunaliangalia tatizo dogo la wanawake kutoka nje ya ndoa kumbe wanaume 9 kati ya 10 wanasaliti ndoa zao.
 
Kwahiyo huyo mwanaume aliwaf*nya wanawake wote waliokubali!! Tafiti nyingine kaaz kwelikweli
 
Tatizo kubwa katika ndoa nyingi ni kuoa wake za watu.
Wengi tunakutana na watu ambao tayari walishakuwa na watu kabla hivo akikutana na X wake huu utafiti unatimia pasina shaka.
 
Technologia ndiyo sababu kubwa sana ya uchepukaji. Watu wanashawishika vibaya sana...
 
Back
Top Bottom