Kati ya Computer Science vs Business Administration ipi ni kozi nzuri!?

Computer science vs Business Administration in terms of emploment opportunities na future nzuri. Ahsante

Kasehuye, ushauri wangu; kama umri wako bado mdogo, nikimaanisha kwamba ndiyo kwanza umemaliza elimu ya kidato cha sita au entry diploma pahala ukiwa chini ya umri wa miaka (wastani) 22 hivi, nashauri usome computer science kwanza. Ufanye hivyo tu iwapo masomo haya unayaweza na unayapenda. Iwapo huyawezi na unafikiria kusoma kwa kushinikizwa tu na mzazi, mlezi au nafasi ya ajira mbeleni basi kufanya hivyo halitakuwa jambo la busara sana kwa maoni yangu. Hayo ni masomo ya mtu mwenye mapenzi nayo. Na kujisomea ukiwa bado na umri mdogo ni vizuri zaidi maana umri ukiwa mkubwa kuna baadhi ya maeneo kitaaluma yanakuwa magumu mtu kuyaelewa kirahisi ukilinganisha na ukiwa na umri mdogo.

Kingine, masomo ya kibiashara kwa mwono wangu ni rahisi kwa mtu kujisomea bila kutegemea sana umri wake. Pia discipline nyingi kitaaluma zinatoa mwanya wa kujifunza mazingira ya kibiashara ndani ya taaluma husika. Kwa maoni yangu vile vile, ni rahisi kwa mtu kujisomea business administration baada ya kumaliza Computer science au taaluma nyingineyo kama udakitari, civil engineering, n.k. kuliko kufanya kinyume chake, hivyo mtu kuwa na viwili vyote kwa ratio iliyo stahili.

Kila la kheri kwa lolote utakalochagua kujifunza.

Steve Dii
 
Back
Top Bottom