Kati hili nani mkweli kati ya CCM na wapinzani?

VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,129
2,918
Ndugu zangu wapendwa naomba tujadili mada hii kwa moyo mweupe uliojaa kweli kama wacha Mungu na wapenda haki.

Rais Magufuli anatumbua majipu tangia aingie madarakani na swala hili limewafurahisha wananchi wengi, je haya majipu anayotumbua Rais leo ni tofauti na yale wapinzani waliokuwa wanalalamikia na ccm ikawaita kwamba ni waongo na wazushi? nitatoa mifano michache tu.

1-swala la safari za viongozi nje ya nchi hasa Rais wapinzani walidai zinaletea nchi hasara ccm wakadai zinaleta faida ila wapinzani wana wivu

2-swala la wakurugenzi tunaona Wenje akitaja hata jina la Kabwe bungeni ila ccm walimtetea na hata spika anamwambia Wenje na wewe pia ni muhusika kutaka kumtetea Kabwe

3-Swala la watumishi hewa wapinzani walipolalamika waliambiwa ni wazushi sana

4-Swala TRA

5-Swala la uda na mikataba mibovu nchini

6-Swala la mikopo ya elimu ya juu

7-Swala la NSSF na mengine mengi
CCM walikuwa watetezi wa serikali ya awamu ya nne kwa juhudi zote kwamba ni sikivu sana na kwamba nchi imepata maendeleo makubwa sana. Lakini takribani hotuba zote za Rais wa awamu ya tano ni kulaumu utendaji mbovu wa serikali ya awamu ya nne uliosababisha watu wachache kuwaibia wananchi na kuwafanya kuwa maskini wa kutupwa. Leo hao waliokuwa wanatetea na kusema kwamba wapinzani ni wazushi wamesahau hayo yote na kujifanya kwamba wameshuka leo kutoka mbinguni... je nani mkweli kati ya wapinzani na ccm? je kuna sababu ya kushindwa kushukuru wapinzani?
 
Mpaka sasa maghufuli yuko vizuri kwenye suala la uwajibikaji, tatizo ninalo liona kwa maghufuli ni kuendesha siasa za kuwagawa watz kuliko kuwakusanya na kuwa na sauti moja ya umma, kauli kama nimemchagua ili wabaya wake wakome, kwa kuwa mmeichagua ccm (segerea) basi nitawaletea maendeleo kama waliochagua ukawa si watz, naona pia anatengeneza maadui wengi ndani ya chama na nje ya chama, lakini jana naona kama kabadilika au amesoma alama za nyakati aliposema anawaomba wana ccm waache siasa za visasi na wasifukue makaburi, maana kuna oparation kuondoa team lowassa
 
Ndugu zangu wapendwa naomba tujadili mada hii kwa moyo mweupe uliojaa kweli kama wacha Mungu na wapenda haki.

Rais Magufuli anatumbua majipu tangia aingie madarakani na swala hili limewafurahisha wananchi wengi, je haya majipu anayotumbua Rais leo ni tofauti na yale wapinzani waliokuwa wanalalamikia na ccm ikawaita kwamba ni waongo na wazushi? nitatoa mifano michache tu.

1-swala la safari za viongozi nje ya nchi hasa Rais wapinzani walidai zinaletea nchi hasara ccm wakadai zinaleta faida ila wapinzani wana wivu

2-swala la wakurugenzi tunaona Wenje akitaja hata jina la Kabwe bungeni ila ccm walimtetea na hata spika anamwambia Wenje na wewe pia ni muhusika kutaka kumtetea Kabwe

3-Swala la watumishi hewa wapinzani walipolalamika waliambiwa ni wazushi sana

4-Swala TRA

5-Swala la uda na mikataba mibovu nchini

6-Swala la mikopo ya elimu ya juu

7-Swala la NSSF na mengine mengi
CCM walikuwa watetezi wa serikali ya awamu ya nne kwa juhudi zote kwamba ni sikivu sana na kwamba nchi imepata maendeleo makubwa sana. Lakini takribani hotuba zote za Rais wa awamu ya tano ni kulaumu utendaji mbovu wa serikali ya awamu ya nne uliosababisha watu wachache kuwaibia wananchi na kuwafanya kuwa maskini wa kutupwa. Leo hao waliokuwa wanatetea na kusema kwamba wapinzani ni wazushi wamesahau hayo yote na kujifanya kwamba wameshuka leo kutoka mbinguni... je nani mkweli kati ya wapinzani na ccm? je kuna sababu ya kushindwa kushukuru wapinzani?

Hoja yako ni ya kweli ila bado sio kweli yote! Wapinzani nao wanasahau kuwa Magufuli anacheza ngoma yao i.e anakabili yale maovu/mapungufu waliyokuwa wana yapigia kelele! Kwa vile ni ngoma yao, wao ndio wangepaswa kumuunga mkono zaidi na kumwelekeza namna ya kuicheza ngoma kwa ustadi! Wangekuwa mstari wa mbele kupendekeza kwake njia bora na sahihi zaidi za kuyamaliza maovu hayo!
 
Uko sahihi, ila Magufuli katika hotuba zake hajawahi kuwaalika wapinzani kwamba njoni tushirikiane, kwahiyo wamezidi kubaguliwa na kuonekana hawafahi na hicho kinafanywa sana na ccm kutaka Magufuli asishirikiane na wapinzani hata kidogo...ila inawezekana yeye ana nia nzuri ila waliomzunguka hawataki....pamoja na hayo sijasema wapinzani wapo sahihi kwa kila kitu hapana
 
EPA,RICHMOND,ESCROW,KAGODA,DEEP GREEN,KIWIRA,MEREMETA,LUGUMI,n.k mbona yanapewa kisogo?

Kwa mfano,utapelekaje watumishi hewa mahakamani alafu ukawaacha watuhumiwa wa hizi kashifa alafu ukategemea tukuunge mkono?Sisi sio wajinga!

Kibaya zaidi,ni lini Magufuli na wana-CCM hawa waliwahi kuwaunga mkono wapinzani wakati wakipigia kelele madudu haya enzi za JK?
 
Magufuli alikuwa Upinzani kuanzia kipindi cha kampeni.

Mi nilipomsikia Magu ktk hotuba yake pale Jangwani kwenye uzinduzi wa kampeni nikaona yuko upinzani.
Katika ulimwengu wa siasa hakuna ukweli ila UKWELI WA LEO NI UONGO WA KESHO NA UONGO WA LEO NI UKWELI WA KWESHO
 
Back
Top Bottom