Kambi ya Fisi
JF-Expert Member
- Feb 3, 2018
- 13,520
- 22,015
Kuna jambo ninaliona hapa kuhusu marufuku ya waziri Ndumbaro itakavyoshindwa kufaulu ni hivi.
Ikiwa watakao kagua passport za mashabiki wenye jezi sio askari wa uhamiaji bali ni FFU wale wanaoendaga uwanjani kutazama mechi na si kuzuia fujo hawataweza kuwabaini wazee wa passport feki, watadanganywa kirahisi mno kwa kuoneshwa passport feki zilizotengenezwa na Wataalam wa passport feki, hapo mashabiki wa bongo wataingia kiulaini tu Kwa kutumia hizo passport feki huku wakiwa na jezi pendwa kwao.
Hakuna ofisi ya uhamiaji pale kwa Mkapa hivyo tutegemee jangu wetu wakichukua jukumu lisilo lao la kukagua passport na hapo ndipo wataaibika katika kuhojiana na mashabiki maana njagu wetu wengi wao ung'eng'e haupandi.
Ni wazi waziri hawezi kushindana ama kuzimisha morari ya mashabiki Kwa kuwapangia cha kuvaa pale kwa Mkapa.
Ni heri aachane hiyo marufuku kabla hajaaibika kitaifa na kimataifa.