Katambi imara zaidi ya kingo za mnara

Katambi imara zaidi ya kingo za mnara

Mwanawakati

Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
10
Reaction score
12
P1410271.JPG
Mwenyekiti wa Balaza la Vijana la CHADEMA Taifa, Mhe: Paschal Patrobas ambaye pia ni mgombea Ubunge wa Ukawa kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Jimbo la Shinyanga, jana majira ya saa 2:45 asubuhi maeneo ya Ibinzamata, akielekea stendi, amevamiwa na watu wasiojulikana na kumchania fomu za ubunge alizokuwa njiani kuzirudisha Halmashauri.

“Ni kweli tumevamiwa na kundi la vijana saba, ni wazi wametumwa! Nadhani wapo coordinated na mtu ama kundi fulani kunihujumu ili nichelewe kurejesha fomu. Nimewamaki sura zao na ninamshukuru Mungu fomu za ubunge walizochana zilikua vivuli, hawakufanikiwa kuchukua fomu halisia, nilijiandaa vyema nikachukua tahadhali,”alisema Patrobas.

Akiwa na dereva wake, anasema walianzia safari ya kwenda stendi mpya ya Shinyanga kutuma mzigo wa Mhe. Godbless Lema Arusha ndipo gari aina ya Noah yenye rangi ya Silva ambayo namba zake hazikujulikana kwa haraka ikagonga chombo chao aina ya RAV 4 chenye nambari za usajili T 781 AKT kwa nyuma na waliposimama Noah hio ikapaki mbele ya gari lao, wakashuka vijana saba walioonesha nia njema kuwataka radhi juu ya kusababisha ajali hiyo.

“Tulipofika katika tuta la kupunguza mwendo, Ibinzamata tulishitushwa na kishindo kikali na kugundua gari aina ya Noah iliokua ikija kwa kasi imegonga chombo chetu, tukasimama kukagua, ndipo vijana wapatao saba wakaanza kutushambulia,” alisema dereva wake, Ndg. Albert Katambi.

Baada ya fujo za muda mfupi kwenye tukio hilo la aina yake, mapambano dhidi ya washukiwa hao, hayakufua dafu kuwazuia, wakawashuhudia wengine wakitoa fomu hizo katika eneo la kioo cha mbele (dashboard) na kuchana nyaraka hizo, pia wakaiba fedha taslimu milioni 2.5 zenye thamani ya kitanzania pamoja na simu ya mkononi kisha watano wakapanda gari lao nakutoweka huku wakiwashuhudia wengine wawili wakikimbia kwa miguu na kutokomea.

Kamanda mkuu wa polisi mkoani humo,Kamanda Justus Kamugisha alipoongea na waandishi wa habari, amethibitisha kuripotiwa kwa tukio hilo. Amelaani vikali kitendo hicho na akasema wamechukua maelezo ya mheshimiwa pamoja na dereva wake na tayari amewaagiza polisi kupeleleza.
“ Nimewatuma vijana, wapo mtaani tayari kwa upelelezi na yeyote aliyehusika na tukio hili hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake,” Alisema Kamugisha .

Mengi yamesemwa, uvumi wa kila aina umesambaa mitandaoni kwamba, Mhe. Patrobas ametekwa na kupelekwa kusikojulikana, wengine wakazusha amepata ajali akaumia vibaya,na wengine wakasema amelikacha jimbo baada ya kununuliwa.
Huo ni Uzushi! Japo hali si shwari, Katambi yupo salama, na imara zaidi ya kingo za mnara.

Zoezi la kurudisha fomu lilikamilika saa nane mchana na mheshimiwa huyo akaondoka kuelekea ofisi kuu za Chama cha demokrasia na Maendeleo Mkoani humo.
 
Mmeanza Movie sasa. Hivi ile ya Sosopi Iringa iliishia wapi?
 
Nimesha nunua popcorn za kutosha maana Leo ntakua online kufatilia hii movie iliyoanza leo
 
Back
Top Bottom