Watanzania tumeingiwa na uvivu wa kufikiri, ukimwambia mtu tatizo, yeye anakimbilia, kusema he! mbona na kwafulani tatizo hili lipo, jamani hii maada ni muhimu sana ukisema eti wanakubalika, kwani nani hajui jinsi rushwa inavyotawala chaguzi zetu, na kutangazwa ambaye hajashinda?, jana nilichangia kuhusu huyu mtoto wa Maliccera, ila nikafokewa,
Naomba tuwe makini sana na hii tabia ambayo sisi tunaona kuwa ni dili, wakati waarabu sasa wanapigana kwa sababu ya michezo kama hii, walianza eti wanapendwa na wananchi wakaongoza miaka zaidi ya 30, na hapohapo wakawa wanawaandaa watoto wao, may take, mchovya asali hachovyi mara maoja na tukiendelea kushabikia mambo kama haya, itakuwa mabya kwani watoto wa Kayumba, hakika hatakama watasoma hawataweza kupata nafasi hizo.
Kuna hoja eti wanaopiga kura si babazao tu, kwani kamati za vyama vyetu siwite marafiki tu, NASISITIZA TENA NA TENA, WATANZANIA WENGI HUCHAGUA KWA KUPELEKESHWA NA NJAA NAWALA SI UTASHI WAO, na mara watakapo stuka hakika mimi naanza kuona kama giza mbele kwa Tanzania endapo tukiendelea kushangilia mambo kama haya