Kasumba ya Kilimanjaro kupendelewa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kasumba ya Kilimanjaro kupendelewa!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Geza Ulole, Dec 5, 2009.

 1. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #1
  Dec 5, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,082
  Likes Received: 4,031
  Trophy Points: 280
  Naomba kuweka mambo wazi kuna hii kasumba ati mkoa wa Kilimanjaro unapendelewa na serikali kimaendeleo! Mimi kama mkazi aliyewahi ishi huko na kujua historia ya huu mkoa nina machache ya kusema haswa juu ya upotoshwaji wa bidii za wakazi wa Kilimanjaro! Mengi ya maendeleo ya Kilimanjaro yameletwa na wenyeji wa huko. Na hii ni kutokana na sababu zifuatazo


  1)Kabla ya uhuru serikali ya Kichifu ya Kilimanjaro tayari ilikuwa na serikali, mabaraza la ushauri [mawaziri], ikulu, bunge na yote ya kisasa Na kidhibitisho Rais akiwa kilimanjaro hufikia kwenye ikulu iliyojengwa na wachagga hao na bunge lao ndio makao makuu ya wilaya Moshi vijijini! Abishe mtu

  2) Kabla ya uhuru tayari serikali ya Kichifu ilikuwa imejenga chuo cha ushirika,chuo cha kahawa, Lyamungo etc. Baada ya uhuru Mchonga akataifisha! Who knows leo hii watoto wanagapi wangesoma huko kama vingeendelezwa chini ya KNCU?

  3) Kwa upande wa afya kwa kushirikiana na mashirika ya dini walishajenga hospitali kila tarafa. Hospitali za Kibosho, Marangu na Machame vielelezo. na kwa KCMC kupitia Good Samaritan, Mchonga alialikwa kuifungua akarudi Dar akaitaifisha as if ingehudumia Wachagga tu shutting its progress to become a teaching hospital leo hii may be ingekuwa biggest Medical college na Watanzania wengi wanaotaka kusoma utabibu wangepata nafasi zaidi za kusoma! Nadhani Mchonga kwake yeye aliona ni threat kwa serikali yake (Mawazo ya kimaskini!). Ati usawa, usawa my foot! "Na asiyefanya kazi na asile"principles rule the World from then, now and tomorrow!

  4) Kwa upande wa elimu ya msingi na sekondari, hamna ubishi nyingi zao zimejengwa kwa michango ya wananchi kupitia vyama vyao vidogovodogo chini ya KNCU walikuwa wakisambaza vitabu na madaftari na tayari walikuwa na KNCU scholarships fund kwa elimu ya chuo. Watani wao Wapare wanaweza kuwadhibitishia hili kutokana na kuishi pamoja wamepata msukumo wa kushindana pia kujenga shule nyingi Upareni pia! Nina uhakika kama Wachagga wasingekuwapo humo Kilimanjaro Wapare wasingejenga kwa nguvu namna ile!

  5) Kwa upande wa fedha na biashara, tayari kwa kupitia chama cha ushirika cha mwanzo afrika KNCU (Kenya na nchi nyingi za afrika including Ghana took a leaf from KNCU achia mbali vya Nyanza na Bukoba), walikuwa wakiuza kahawa nje baada ya kupigania haki hiyo toka kwa mkoloni na kushinda na walikuwa na hata akaunti za fedha za kigeni nje ya nchi na hata mabenki ya ushirika. Mchonga akaamua kuvunja KNCU na kulazimisha kahawa iuzwe serikalini kwa bei inayoipanga (contrarily to free market theories) matokeo yake wakafyeka kahawa yote baada ya gharama za uzalishaji kuwa kubwa zaidi ya bei ya uuzaji (Unyonyaji). From being in top 5 World leading coffee producer leo hii no one knows if TZ produce coffee na hata hizi juhudi za sasa unazoona ni baada ya serikali kujirudi na kuruhusu KNCU tena!


  6) Kwa upande wa umwagiliaji, hata kabla ya uhuru tawala yao ilikuwa imeshajenga mfumo wa umwagiliaji wa mashamba ya migomba na kahawa kwenye viijiji vyote na ikisimamiwa kimila. Barabara baadhi hasa za vijijini zilishajengwa kwa kujitolea na pia Mjerumani alijenga so za Mwinyi ni kurudishia zilizokuwepo na kwa KIA, serikali ililazimika kuujenga maana watalii wote walikuwa wanakuja Kilimanjaro tokea Nairobi na kuikosesha serikali mapato.

  7)Kwa Upande wa utalii tayari kulikuwa na KNCU hostel (inadaiwa jengo la mwanzo kabisa Tanganyika kuwa na lift!) na pia Kibo Hotel na hotel za Marangu kama hotel Capricorn na nyingine nyingi tu na hata leo hii hawa ndugu zetu wanachakarika kusukuma gurudumu la maendeleo huko Arusha na Kilimanjaro kwenye utalii!

  NB: MALI ZOTE HIZI PAMOJA NA AKAUNTI ZA FEDHA ZA KIGENI ZILITAIFISHWA NA SERIKALI NA WATU WA MKOA HUO WALA HAWAJAWAHI KUONGELEA KUDAI PESA ZAO ZA KODI WALIZOKUWA WAKILIPA KWA MANGI ZILIZOJENGA VITEGA UCHUMI HIVYO KWA SERIKALI!!

  Haingii akilini na ni kama tusi kusema wananchi wa kilimanjaro kuwa wameshapata upendeleo na serikali!

  AKIFUFUKA MTU ALIYEKUFA MWAKA 1967 MOSHI, HATAKUTA MKOA UMEBADILIKA SANA zaidi ya idadi ya watu na ukame kuongezeka na viwanda 16 vilivyokuwa vikizalisha kufa! Ni wazi kuwa kama upendeleo wowote ungefanyika kilimanjaro basi leo hii labda ingeweza kuwa mbele zaidi na tofauti ingeonekana dhahiri.

  Leo hii majengo mengi mazuri yanajengwa na vijana wanaoamua kuwekeza huko baada ya wazazi wao kukatishwa tamaa na Mchonga! kwani kwa mila zao huona aibu au laana kutokuwa na maendeleo na ni ushindani huu unawafanya kuhangaika

  Nadhani Watanzania tushindane kwa maendeleo. Na tuache hii kasumba na propaganda za chuki, ati fulani anapendelewa ni vema wakazi wa maeneo mengine nchini wakaiga mazuri na kujaribu nao badala ya kuwatuhumu na ukabila! hawa watu wako nchi nzima wanafanya biashara na makabila mengine hata na mataifa mengine ukienda Nairobi unawakuta! Ukienda Maputo, wapo! Arusha wapo! Mwanza wapo! sasa chuki inatokea wapi? Sidhani kama Mchagga atakataa ukimwomba kufanya nae biashara! hawana choyo ya maendeleo! tujiulize kama Tanzania ingekuwa Federal state Kilimanjaro ingekuwa wapi kutokana na juhudi walizoonesha toka kabla ya uhuru?

  Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni!

  nawakilisha!

  Mpigika
  Geza ulole
   
 2. N

  Ndakilawe JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2013
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 4,084
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  Hii mada yako iligusa wengi, ila kwa sababu ambazo wanazijua wao hakuna hata mmoja aliyejaribu kutia neno, pamoja na ukweli wote uliooandika hapo!
   
Loading...