Kasulumbayi: Tegemeo la CHADEMA Sukuma Land | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kasulumbayi: Tegemeo la CHADEMA Sukuma Land

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 15, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 15, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145


  MWAKA 2010 ulikuwa wa kihistoria kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutokana na mafanikio makubwa kiliyoyapata kisiasa.
  Kwanza kabisa CHADEMA ilifanya vizuri sana katika Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na udiwani.
  CHADEMA ilipata wabunge wengi wa kuchaguliwa na mgombea wake wa kiti cha urais alipata kura nyingi zilizokiwezesha chama hicho kupata idadi kubwa ya wabunge wanawake wa viti maalumu, hivyo kukiwezesha kuwa chama kikuu cha upinzani bungeni.
  Pili, CHADEMA ilifanikiwa kujiimarisha na kujijengea imani kubwa miongoni mwa wananchi, hivyo kukifanya kiaminiwe na kutegemewa na wengi kama chama mbadala kinachoweza kuchukua mahala pa chama tawala - Chama Cha Mapinduzi (CCM).
  Tatu, CHADEMA ilifanikiwa kuwavutia wanasiasa wengi kutoka ndani na nje ya CCM, ambao walijiunga nayo na kugombea nyadhifa za ubunge na udiwani na kushinda, hivyo kuiwezesha kujiimarisha.
  Miongoni mwa wanasiasa walioingia CHADEMA mwaka jana na kugombea na kushinda ubunge ni Mbunge wa sasa wa Maswa Mashariki, Sylvester Mhoja Kasulumbayi.
  Kasulumbayi ni mmoja wa waasisi wa harakati za mageuzi nchini, ambaye alijiunga na vyama vya upinzani tangu mfumo huo uliporejeshwa mwaka 1992 akiwa mwanachama wa Chama cha Wananchi (CUF).
  Akiwa CUF, Kasulumbayi amekuwa diwani kwa miaka 14 (1994-2008), mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Maswa na hatimaye mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho, wadhifa alioushikilia mpaka wakati anajiuzulu uanachama wa chama hicho mwaka 2008.
  Baada ya kujiuzulu CUF 2008, Kasulumbayi alijiunga na Chama cha Ustawi wa Jamii (CHAUSTA), cha James Mapalala, ambako alifanikiwa kuchaguliwa tena kuendelea kuwa diwani wa Kata ya Ipililo.
  Hata hivyo, Kasulumbayi hakudumu CHAUSTA kwani mwaka 2010 alijiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na akagombea na kushinda ubunge wa Jimbo la Maswa Mashariki na udiwani wa Kata ya Ipililo.
  “Niliondoka CHAUSTA na kujiunga CHADEMA baada ya kufuatwa na viongozi wa kitaifa wa CHADEMA walioniomba kuungana nao ili kuunganisha nguvu na kusukuma mbele harakati za mageuzi nchini, nilikubali wito wa viongozi wa CHADEMA baada ya kuchunguza na kubaini kuwa hicho ndicho chama pekee chenye nia na mikakati thabiti ya kujijenga na kujiimarisha kisiasa kwa lengo la kuongoza nchi, CHAUSTA isingeniwezesha kutimiza malengo yangu ya kisiasa,” anabainisha Kasulumbayi.
  “Kuhusu kuondoka kwangu CUF, sababu kubwa ilikuwa ni kutokana na viongozi wakuu wa CUF kushindwa kuwatetea wanyonge wanaonyanyaswa na kuteswa, kinyume na malengo ya kuanzishwa kwa chama.
  “Kwa mfano, mara baada ya uchaguzi mkuu wa 2005, wafuasi wa CCM waliojifanya sungu sungu waliwavamia wapiga kura wangu na kuwapiga na kuwachomea moto nyumba zao lakini CUF walishindwa kulipia gharama za mawakili wa kuwatetea waathirika hao, hii ndio sababu iliyonifanya niondoke CUF”, anafafanua Kasulumbayi.
  Baada ya kuingia CHADEMA, Kasulumbayi anasema atatumia nguvu na muda wake wote kukijenga na kukiimarisha chama hicho katika ukanda wote wa Sukumaland ili kukiwezesha kushinda chaguzi zijazo hususan Uchaguzi Mkuu wa 2015.
  “Nimeanza kampeni kubwa ya kuijenga CHADEMA katika mikoa yote ya Usukuma, nimefungua matawi zaidi ya 100 katika Wilaya ya Maswa, nitakwenda wilaya nyingine zote za Shinyanga na Simiyu kukijenga na kukiimarisha chama changu ili tushinde chaguzi zijazo,” anasema Kasulumbayi.
  Kasulumbayi ambaye ni mwalimu kitaaluma, anayo historia kama ya marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ya kulazimishwa na watawala kuachana na kazi ya ualimu baada ya kutakiwa kuchagua kati ya ajira na siasa.
  Anasema aliamua kuchagua kuendelea na siasa ili aweze kutoa mchango wake katika kuleta mabadiliko ya uongozi yenye manufaa kwa Watanzania walio wengi kisiasa, kiuchumi na kijamii.
  Kasulumbayi anasema wakati wote amekuwa akishughulikia matatizo ya wananchi, kwa kutetea watu wanaonyanyaswa na kuteswa na baadhi ya watumishi wa serikali wasio waadilifu.
  “Vijijini kuna matatizo mengi yanayowakabili wananchi wanyonge, polisi na maafisa watendaji wa kata na vijiji huwabambikiza kesi wananchi na kuwalazimisha kutoa rushwa, wanaporwa mali zao hususan mifugo kwa kutungiwa kesi mbalimbali ikiwamo kesi za mauaji, kwahiyo natumia akili, nguvu na muda wangu mwingi kushughulikia matatizo haya,” anasema Kasulumbayi.
  Anasema aliamua kugombea ubunge baada ya kushawishiwa na wapiga kura wa kata yake ya Ipililo na wananchi wengine kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Maswa, ambao waliridhishwa na utendaji kazi wake wakati akiwa diwani wa Kata ya Ipililo.
  “Ni wananchi wenyewe walionishawishi kugombea ubunge baada ya kufanya kazi nzuri kwenye udiwani kwa kuboresha huduma za elimu, barabara na huduma za afya na maji, barabara zinapitika wakati wote wa majira ya mwaka, maji yapo ukaribu usiozidi meta 400 na shule zetu ni bora, mafanikio haya yaliwafanya wananchi wanikubali na kuniamini kuwa naweza kazi ya ubunge,” anabainisha.
  Kasulumbayi anasema kuwa kutokana na tabia yake ya kuwa karibu na wananchi, anategemea kupata ushirikiano wa hali ya juu kutoka kwao katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayolikabili jimbo lake.
  “Ninajua tuna changamoto nyingi katika sekta ya elimu, miundombinu ya barabara, maji, afya, na kilimo, lakini nina imani tutaleta mabadiliko makubwa katika kipindi cha ubunge wangu,” anasema Kasulumbayi.
  Anasema anatambua kuwa shule nyingi za Mkoa wa Shinyanga hazifanyi vizuri katika mitihani mbalimbali ya kitaifa, na tatizo la msingi ni kukosekana kwa walimu wa kutosha katika shule za mkoa huo pamoja na upungufu wa vifaa vya kufundishia na kusomea.
  “Nikiwa mbunge suala la elimu ni moja ya vipaumbele vyangu, nitawabana sana watendaji serikalini ili watuletee walimu wa kutosha na vifaa vya kutosha vya kufundishia na kujifunzia,” anafafanua Kasulumbayi.
  Kasulumbayi pia amepanga kuboresha kilimo na ufugaji katika jimbo lake kwa kuwaelimisha wakulima na wafugaji mbinu za kilimo cha kisasa na ufugaji wa kisasa kwa kuwatumia kikamilifu wataalamu wa kilimo na mifugo.
  “Ninakerwa mno na umaskini unaowazunguka wananchi walio wengi, ndoto zangu ni kuona watu wengi wakiboresha hali zao za kiuchumi, nataka kuwawezesha wananchi wengi hususan wakulima na wafugaji kukuza vipato vyao.
  “Kwahiyo, mipango yangu ya miaka mitano ni kuwawezesha wakulima na wafugaji kulima na kufuga kisasa ili kupata mazao mengi zaidi, nyumbani kwangu kuna mashamba ya mfano ambako watu wanakuja kujifunza”, anabainisha Kasulumbayi.
  Kuhusu ujenzi wa nyumba za kisasa, Kasulumbayi anasema ataendesha kampeni katika jimbo lake kuwaelimisha wananchi wake faida za kuwa na nyumba bora na kuwahamasisha kutumia sehemu ya mifugo yao kujengea nyumba za kisasa.
  “Kwenye kata yangu tumepiga hatua kubwa katika ujenzi wa nyumba za kisasa, karibu robo tatu ya nyumba katika kata yangu ni za kisasa, tutapeleka mabadiliko katika kata nyingine za Jimbo la Maswa Mashariki,” anabainisha Kasulumbayi.
  Katika kufanikisha mkakati wake wa kuboresha makazi ya wapiga kura wake, Kasulumbayi ameiomba serikali kuangalia upya suala la bei za vifaa vya ujenzi hususan saruji na mabati ili kuwawezesha Watanzania wengi kujenga nyumba bora za kuishi.
  Kasulumbayi alizaliwa miaka 61 iliyopita katika Kijiji cha Zobogo, Wilaya ya Shinyanga Vijijini, akiwa ni mtoto wa pili kati ya watoto wanne wa mzee Kasulumbayi Mahingu na mama Ngema Mayala.
  Alipata elimu yake ya msingi kuanzia mwaka 1959 mpaka 1965 katika shule za msingi Didia na Bugisi, Wilaya ya Shinyanga Vijijini. Elimu ya sekondari aliipata kutoka Shule ya Sekondari ya Kwilo, wilayani Mahenge, kati ya mwaka 1966 mpaka 1970.
  Alipata mafunzo ya taaluma ya ualimu, daraja la tatu A, kati ya mwaka 1971 na 1972, katika Chuo cha Ualimu cha Monduli, mkoani Arusha.
  Kasulumbayi aliajiriwa kama mwalimu wa kawaida kuanzia mwaka 1973, lakini alipandishwa daraja na kuwa mwalimu mkuu ndani ya miezi sita tu baada ya kuajiriwa. Kasulumbayi amefanya kazi kama mwalimu mkuu tangu mwaka 1973 mpaka 2000 alipostaafu kazi ya ualimu, akiwa amefundisha katika shule za msingi za Lalago Bweni (Maswa), Ng’wabagalu (Meatu), Ikungwilyankoma (Maswa), Kidema (Maswa), Ipililo B na mwisho Ipililo A (zote za Maswa). Ni baba wa watoto 15 kwa wakeze watatu, ni msukuma kindakindaki ambaye anaishi na kufuata kikamilifu mila na desturi za Kisukuma.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Watu kama huyu wanaitajika kwenye Chadema sababu wanatoa changamoto bora kwa chama hivyo kushinda kwenye majimbo mengine
   
 3. Chitemo

  Chitemo JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,293
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  nimeipenda sana history ya mh. MHOJA kwani inanipa hamasa kuleta mabadiliko jimboni kwangu, huyu mzee mi mwenzenu n skulmate wangu, hata mi nimesoma KWIRO (mahenge) shule waliyosoma watu maarufu kama fisadi late David Balal, Andrew Chenge, LIYUMBA na wengine waungwana kama mh. Mhoja.
  mwaveja baba mbunge......!!!?
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Good inspiring staff
   
 5. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Hilo jembe ulaya huko usukumani.Historia yake anakwambia tangu mfumo wa vyama vingi uingie yeye ni Diwani CUF baadae CHAUSTA.Hapo Kata ya Ipililo CCM huwaga wanaishia kunawa kata hiyo haijawahi kuwa chini ya CCM.Mheshimiwa MHOJA tunataka mkoa wa shinyanga uwe chini ya CDM ifikapo 2015 Wasukuma wako tayari kwa hili na wameonyesha hivyo pamoja na uchakachuaji wa CCM lakini wapi?? Komeja ong'wise.Nsuji go- Nva gugang'wiwagwa gutali nsebu.
   
 6. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hongera sana. Lakini je ameshawahi kushika wadhifa hata wa mwenyekiti au hata makamo wa mwenyekiti wa halmashauri ya huko Maswa? au anaishia udiwani tu.
   
 7. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Mh mkuu pole sana kwani kuwa mwenyekiti au makamo ndiyo kuwatumia wananchi? Wewe wa wapi wewe.
   
 8. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pujini kule Pemba.
   
 9. c

  chilljuice Member

  #9
  Mar 16, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu amjalie ale vya mwisho wenye sifa zao wanakuja kuchukua ubunge wa Maswa Mashariki, alipata kwa bahati maana CCM walichemsha kwa kuchakachua mtu waliemtaka wapiga kura wengi.
   
Loading...