Kassim Majaliwa na hadithi za Rashid Kawawa..

Kassim Majaliwa na hadithi za Rashid Kawawa..

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,320
Reaction score
117,613
Ukiwasikiliza watu wanaomsifia Mwalimu Nyerere kwa uongozi mzuri most of times wengi wao huwa 'wanambambikia' Rashidi Kawawa, mapungufu na makosa yote ya utawala wa Nyerere. Ni kama vile Kawawa ndo anestahili kubebeshwa kila baya la utawala wa Nyerere na mazuri yote ni ya Nyerere, licha ya Nyerere mwenyewe kusema mara kwa mara Hakuna 'mtu mwaminifu' aliewahi kukutana nae kama Kawawa, na mara zote mahusiano yao yalikuwa kama ya Mwalimu na mwanafunzi.

Kawawa alipewa tu maagizo na kuyatekeleza kwa uaminifu mkubwa. Kawawa aliwahi hata kuachiwa nchi, akawa Waziri mkuu wa Tanganyika huru na bado 'akamrudishia' Nyerere madaraka ya ukuu wa nchi. Lakini hata kwa waasisi ni nadra kutajwa...Utasikia Nyerere na Karume. kila lilioenda kombo wakati wa Nyerere lawama alipewa Kawawa.

Rais mpya Magufuli keshajipatia 'mashabiki' wenye jazba na wasiotaka hata akosolewe, ni kama wengine ni kama washaanza mchakato wa kumfanya Magufuli awe 'mtakatifu' mpya baada ya Nyerere, wakati ana siku 20 tu ofisini na wengine wameshaanza lawama kwa Kassim Majaliwa wakimtaka aende na kasi ya Rais.

Maswali yapo mengi ya kujiuliza.

Je Majaliwa ana sauti kiasi gani kwa Rais? je ataweza hata kumkosoa bossi wake? au kupendekeza watu kwenye baraza la mawaziri? au itakuwa kama Nyerere na Kawawa? Mwalimu na mwanafunzi? na je mapungufu na makosa yakijitokeza. Majaliwa hatageuzwa 'Kawawa mwingine'?

Je kama maamuzi yote yatatoka kwa Rais, Majaliwa atatendewa haki? au ndo tutarudi kule kule?

Sifa ni za Magufuli, na makosa ni ya Majaliwa?
 
Word!!!!

Hakuna rais anayependa kuwa overshadowed na PM wake Mkuu
 
ukitaka kutawala nchi weka surbodinate dhaifu ili asikufunike.jk alichemsha akamuweka lowassa akataka kumfunika.ndo maana enzi za mkapa hatukuona mbadala wake,sumaye na shein wote hawakuwa machachari.nyerere angemuweka kambona kuwa pm angempindua.hata kifo cha sokoine kinafanana na anguko la lowasa.kutaka kumfunika mkuu wako
 
Nzuri mkuu...... EL analipia kuwa bright zaidi kwenye kaz zake ndo maana tulisikia kauli kama " sina hisa ya uraisi na mtu yeyote"
 
Kazi ipo,mi ntaanza kuutathimini utawala huu baada ya miezi 3,
kwasasa ni mihemko tu
 
Mie unanikumbusha na zile hadithi za "Kawawa funika kikombe"
 
Mie unanikumbusha na zile hadithi za "Kawawa funika kikombe"

Ha ha ha ha ha! Maana angepasuka tumbo kwa chai alizokuwa anajaziwa kama sio Mwl. kumshtua nini alipaswa kufanya. Hii kali sana, sidhani kama .com wanaijua hii.
 
PM bwana. Kawageuka wenzake aliokuwa nao ofisi moja na kuwadai ripoti ya utekelezaji wa mradi wa DART! Hapa kazi ipo.
 
Cleopa Msuya pia alikuwa kwenye cabinet ya mwalimu kama Waziri Mkuu. Vipi na yeye dhaifu? Lakini pia Mwinyi naye hakufanya kazi na wadhaifu. Malecela na Warioba si watu wadogo. Lowassa tatizo lake alikuwa anafanya kampeni mapema mno na kuimarisha network. Kilichomponza pia ni kusahau kuwa hakuna Rais wa CCM aliyetoka nje ya Baraza la Mawaziri.
 
Kuna story ya maduka ya ushirika. Dhana ilikuwa yaanzishwe ili kutoa huduma nafuu kwa watu ambao pia wangekuwa wamiliki.
Ilidhaniwa yale ya watu binafsi yangekufa natural death.
What happened? Kawawa aliamuru maduka binafsi yafungwe. Kama ni kweli, kosa la Nyerere au Kawawa?
 
Kuna story ya maduka ya ushirika. Dhana ilikuwa yaanzishwe ili kutoa huduma nafuu kwa watu ambao pia wangekuwa wamiliki.
Ilidhaniwa yale ya watu binafsi yangekufa natural death.
What happened? Kawawa aliamuru maduka binafsi yafungwe. Kama ni kweli, kosa la Nyerere au Kawawa?


Wakati Kawawa anafanya hayo Nyerere alikuwa wapi?
 
Wakati Kawawa anafanya hayo Nyerere alikuwa wapi?
Obviously alikuwepo. Baada ya hapo Kawawa aliendelea kuwa PM kwa muda gani? Alitumbuliwa japo baadaye alirudi tena ulingoni! That was then. Ya Prof. Mgaya TCU na sasa NIMR. Nothing new!
 
Back
Top Bottom