Kaskazini ndio mikoa gani? Na kusini ndo mikoa ipi?

Msulibasi

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
5,957
Reaction score
8,005
Kila mara katika mambo ya siasa utaskia" mikoa ya kaskazini "mara mikoa ya kusini" au Dodoma ipo kati .Chakushangaza kila mmoja an tafsiri yake na idadi yake ya hiyo mikoa. Napenda kufahamu kijiografia ukichora pande nne mikoa ipi ya kusini,ipi kaskazini,ipi mashariki ipi magharibi na upi wa kati ukilinganisha singida na dodoma maana wanasiasa wanatuchanganya. Maana utaskia raisi hatotoka kaskazini mara kusini tumetengwa mara---------nijibuni kwa mujibu wa ramani ya tanzania compass direction
 
Mashariki kuna Dar,Moro na Pwani. Magharibi kuna Tabora, Rukwa, Katavi na Kigoma. Kaskazini kuna Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga.

Mikoa ya kusini ni Ruvuma, Lindi na Mtwara. Mikoa ya kati ni Dodoma na Singida. Kanda ya ziwa kuna Kagera, Mara, Geita, Mwanza, Simiyu na Shinyanga. Nyanda za juu kuna Mbeya, Iringa na Njombe.

Kuna mikoa huwa inawekwa kwenye kanda tofauti kulingana na utashi wa waandaji wa shughuli fulani kama nane nane, michezo n.k. Kwa mfano Tanga unaweza kuikuta kanda ya mashariki kwenye nane nane, vile vile Shinyanga huwa wanaiweka magharibi wakati fulani. Ni hivyo mkuu
 
Wewe Ni Muongo!

​

Kaskazini (kijiografia) mwa Tanzania kuna Mikoa ya Mwanza, Kagera, na Mara pmj na Ziwa Nyanza, Tanga na KLM ziko Mashariki mwa nchi yetu!
 
Nchi huweza kugawanywa katika kanda ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa baathi ya mipango. Kijiographia hakuna kanda ya ziwa ila sisi kama taifa tumejigawanya hivyo kwa manufaa yetu. Sehemu yoyote ina pande 4 lakini yaweza kiugawanywa kukithi mahitaji fulani kama nilivyotaja ndio maana leo nchi tano tu zinajiita jumuiya ya Afrika mashariki. Uko hapo?

Unaoongea mambo yasiyoeleweka na kama hivyo ndivyo tunavyofanya basi hakuna ubishi ya kwamba sisi ni watu ambao hatuko intelligent na Wazungu na Watu wengine Duniani watakuwa siku zote walikuwa wanasema UKWELI ya kwamba Waafrika ni Binadamu ambao hatuna Akili za kutosha ukilinganisha na Binadamu wengine, kwa maana Kaskazini ni kaskazini na Mashariki ni Mashariki sasa wewe huwezi kuniambia ya kwamba KLM iko Kaskazini wakati ramani ya Tanzania inaonyesha ya kwamba Mikoa iliyo Kaskazini ni Mwanza, Mara na Kagera pmj na Ziwa Nyanza!
Kuna kosa gani kuiita nchi za Tanzania, Uganda na nyinginezo AM? Ni kweli ya kwamba kijiografia ziko AM, ingekuwa hizi nchi tunaziita A.magharibi hapo hoja yako ingekuwa na maana lkn ziko Kijiografia Mashariki mwa Bara la Afrika sasa kuna kosa gani kuziita Afrika Mashariki?

Lakini Kuiita mikoa wa Tanga na KLM kwamba ndio Kaskazini mwa Tanzania ni ujinga na kutokuwa na akili kwani kijiografia Hii Mikoa haiko Kaskazini kabisa mwa Tanzania, kuna Mikoa ambayo iko Kaskazini mwa Tanzania nayo ni Mwanza,Kagera na Mara!

​
 
Mi napata shida sana maana utasikia chama flani ni cha kaskazini ,au UMISETA kaskazini mara shuleni ukioneshwa zile pande nne tofauti ila hii ya kwako naikubali ndo maana hao wengine siwaelewi

Back
Top Bottom