Kasi ya utumishi

ElBaradei

Member
May 4, 2017
40
14
Wadau napenda kuipongeza utumishi kwa speed ya kuchuja na kuita waliofanikiwa makazini. Mfano mzuri ni TPA na NHIF mchakato wa NHIF Umekwenda kwa speed nzuri na sasa watu wameitwa kwa oral interview ndani ya mwezi huu huu.

Hongereni sana kwa speed nzuri. Naomba ndugu zetu wa Workers Compensation Fund, PPF na LAPF na taasisi zote za umma wafanye kwa mtiririko huu. WCF na PPF ni matapeli wa ajira, wameita watu written toka March 18 mpaka leo leo hawajamaliza kusahisha mtihani.Sijui wamesafirisha nje ya nchi kusahishwa au wanasubiri watu wajisahau waweke watu wao. TAKUKURU mpo wapi ?? Hawa WCF,EWURA, PPF,na LAPFni wa kuwachunguza na kuwafikisha mahakamani. Hawa ni wezi na matapeli hapa nchini.

Wanawaingiza watoto wa masikini katika madeni yasiyo ya lazima. Watoto wa wakulima wanakopa nauli pesa nyingi tu za kwenda interviews Dar toka kigoma, Namtumbo, Sengerema, Tarime na vijiji vyote Tanzania alafu mwisho wa siku wanafanyiwa mazingaombwe na kuachwa pasipokuelewa mwisho wao.

Hizi taasisi naomba iwe marufuku kutangaza ajira.Tume ya ajira na utumishi isimamie michakato yote ya kuajiri katika taasisi za umma. Tume ya utumishi tunaomba wasimamie hii michakato na ssio kuwaachia matapeli wanaotumia mwamvuli wa serikali. Asanteni
 
Hata PCCB walitangaza nafasi za ajira lakini hawakutumia mfumo wa utumishi wa umma, ndio wale waliotaka mpaka cheti cha darasa la saba na uwe under 25. Labda tuombe msaada polisi.
 
Polisi hawataweza kusaidia kabisa. Labda mkuu wa nchi awatumbue hao matapeli wa PPF,WCF, LAPF NA EWURA. Asuke upya kama alivyowanyoosha NHIF. Ndo maana umeona tangazo la kazi la madirectors kama 5 hivi. Piga chini wakurugenzi vihiyo ingiza majembe kazini.
 
Kweli kabisa mkuu! hilo tangazo la ma directors nimeliona, NHIF wamekuwa na uwazi kwenye fursa sasa.
 
Back
Top Bottom