Kasi ya UKAWA Ilala yamtoa mafichoni Mbunge wa CCM Segerea


Mwanahabari Huru

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Messages
13,517
Likes
27,448
Points
280
Age
48
Mwanahabari Huru

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined Mar 9, 2015
13,517 27,448 280
Katika kile ambacho kimezoeleka kwa wabunge wa CCM kujisogeza kwa wananchi na wapiga kura wakati wa kampeni na Mara baada ya kuchaguliwa wabunge hao hukaa mbali na wananchi wao na pengine hata cm zao kutopatika sasa umekuwa tofauti kidogo.

Hali hii imejitokeza kwa Mbunge wa Segerea (CCM) Bonnah Kaluwa ambaye amekuwa haonekani Mara kwa Mara Jimboni na muda mwingi simu yake kutopatikana sasa amelazimika kubadili utamaduni wa Chama chake CCM wa kukaa mbali na wananchi. Bonna umeamua kuuacha utamaduni huo na kuingia mtaani kutembelea wananchi wa Jimbo LA Segerea ambapo leo tarehe 12/07/2016 anatembelea Kata ya Bonyokwa, Kata ambayo inaongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Mhe. Charles Kuyeko.

Ziara ya Mhe. Bonna Katika Kata ya Bonyokwa imetafasiliwa na wananchi waliowengi ni kama kwenda kujifunza kwa Diwani wa Kata hiyo jinsi ya kukaa karibu na wananchi, kutimiza ahadi na kuwaletea maendeleo wananchi wanaowaongoza.

Bonna anaenda Bonyokwa huku kukiwa na miradi chungu nzima iliyoanzisha na kusimamiwa na Mstahiki Meya bila ya mbunge huyo kuonyesha ushirikiano wowote. Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa Madarasa mawili yaliyokamilika katika shule ya msingi Bonyokwa na mengine manne yanajengwa, barabara ya Segerea-bonyokwa mkandarasi huko site anajenga, daraja LA Bonyokwa-kinyerezi limekamilika, barabara ya Bonyokwa kimara iko njiani kuanza kujengwa, madawati, ujenzi wa soko na stendi ya daladala mtaa wa Msingwa mazunguzo yanaendelea ili ujenzi uanze ndani ya mwaka huu. Yote haya yamefanywa kwa kasi ya ajabu na Mstahiki Meya ndani ya miezi 8 wakati Mhe. Mbunge akiwa mafichoni na ndipo sasa ameamua kujitokeza.

Kasi hiyo ya kuwatumikia wananchi haipo tu kwa Kata ya Bonyokwa tu na Segerea kwa ujumla Bali kwa Kata zote zinazoongozwa na UKAWA kwa Ilala. Mfano mzuri wa kazi ya kuwahudumia wananchi ni Kata ya Kinyerezi, Liwiti, Vingunguti nk.

Aidha, wananchi wa Segerea wamemtaka mbunge bonna aache kujificha kwa kukaa mbali na wananchi Bali aungane na UKAWA wachape kazi. Lakini pia aache kudandia miradi ambayo inafanywa na Madiwani na kujifanya yeye ndo kafanya. Bonna alinukuliwa hivi karibuni akijinasibu kuwa yeye ndiye aliwezesha ukarabati wa machinjio ya Vingunguti baada ya kufungiwa na serikali kutokana na uchafu na miundombinu mibovu huku akijuwa wazi kuwa hajahusika kwa chochote na ukarabati wa machinjio hayo.

Baada ya Machinjio ya Vingunguti kufungiwa na serikali, ni Naibu Meya na diwani wa kata ya vingunguti mhe. Kumbilamoto kwa kushirikiana na Madiwani wenzake na kupitia kamati ya fedha, Manispaa iliweza kutoa fedha kwa ajili ya ukarabati wa machinjio hayo na siyo fedha kutoka mfuko wa Jimbo.

Hivyo basi ni vizuri mhe. Bonna akajipambanua yeye kuwa Mbunge wa wananchi wa Segerea na siyo Mbunge wa Dodoma na kuzima simu yake muda wote. Bonna siyo tu kwamba yuko mbali na wananchi Bali pia yuko mbali sana na Madiwani wa Jimbo la Segerea. Ni wakati sasa Mhe. Bonna akatambua yuko kuwawakilisha wana Segerea.

Na Alex Massaba
 
JT2014

JT2014

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2014
Messages
1,867
Likes
1,061
Points
280
JT2014

JT2014

JF-Expert Member
Joined Jan 18, 2014
1,867 1,061 280
Kwenye kata za UKAWA ulizozitaja umesahau kata ya kisukulu
tuko poa na diwani wetu Saenda na yuko sambamba na wananchi kwa kila
jambo.Naungana nawe kuwapongeza madiwani wa UKAWA
kama wapo ambao hawapigi kazi ni muda wa kuamka na kupiga kazi.
 
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Messages
33,813
Likes
13,869
Points
280
Age
34
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined Feb 21, 2013
33,813 13,869 280
Acha kutupotezea. Tunamsikiliza Rais wa nchi sasa.
 
dlnobby

dlnobby

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2014
Messages
2,537
Likes
3,241
Points
280
dlnobby

dlnobby

JF-Expert Member
Joined Jul 30, 2014
2,537 3,241 280
Hahaaa hiyoo ndo serikali ya CCM acha kusema ukawa....hao wote wanasimamiwa na ccm so hayo maendeleo yametekelezwa kulingana na ilan ya ccm
 
L

lebara

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2013
Messages
651
Likes
697
Points
180
L

lebara

JF-Expert Member
Joined Jul 9, 2013
651 697 180
Acha kutupotezea. Tunamsikiliza Rais wa nchi sasa.
Unamsikiliza wewe , hatuna muda wa kuangalia maagizo, miezi 9 baada ya uchaguzi bado mnaunda serikali wakati imebaki miaka minne kufanyika uchaguzi
 
M

magafumukama

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2016
Messages
742
Likes
196
Points
60
Age
68
M

magafumukama

JF-Expert Member
Joined May 31, 2016
742 196 60
UKAWA HOYEEEEEE!!!!!!!! Hawa jamaa ndio wenye sera ya kazi siyo kila siku vikao; kuchaguana kwa nani alifanya nini mwezi wa kumi 25. Hongereni sana madiwani na wabunge wa ukawa ambao tumeona matokeo ya kutoshirikishwa kwenye bunge la bajeti. Tunawaaminia makamanda wangu
 

Forum statistics

Threads 1,237,195
Members 475,497
Posts 29,280,990