KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amesema kasi ya utendaji kazi ya Rais John Magufuli inaweza kuua uwepo wa vyama vya upinzani nchini.
Hata hivyo alisema kuwa hangependa upinzani ufe kwa vile hiyo pia itakuwa imeua demokrasia nchini na kudai kuwa lengo la kuanzisha vyama vya siasa haikuwa kuviua bali ni kuviona vikiendelea kuwepo.
Hii kasi ya Magufuli inaiuwa CCM, basi tu huyu NAPE hajitambui. Ni wao CCM ndio waliozoea mambo ya figisufigisu ambazo Magufuli anazipangua.
Mpaka sasa ni CCM ndio walioisoma namba kwa sababu rushwa zao walizotoa ili kushinda uchaguzi hazitorudi , yeye mwenyewe huyu alibananishwa jimboni Mtama akitoa rushwa basi tu aliruka kimanga.
Kasi ya Magufuli itafanya upinzani uwe mkali ndani ya chama chao cha CCM, ni hivi majuzi tu wabunge wote wa CCM walijifungia makao makuu ya chama white house wakaanza kumteta rais chini ya uenyekiti wa katibu mkuu Kinana kwamba kasi ya rais wao itakiweka mahala pagumu chama hasa katika suala na kudai kodi wafanya biashara na kuwavunjia watu wa Dar waliojenga mabondeni wakati huu wa mvua.
Huyu Nape asijifanye mwendawazimu, uchaguzi mkuu ukiitishwa leo hii Dar CCM haiwezi kuambua kitu hili liko wazi, sasa katika hali hii ni vipi Magufuli ataweza kuuwa upinzani zaidi ya kukiuwa chama chake?
Nape asijifanye hamnazo.