TAECOLTD
JF-Expert Member
- Mar 2, 2013
- 1,051
- 1,835
Habari za leo ndugu zangu?
Naomba kidogo leo nijitokeze kuongelea kinachoendelea katika mkoa wetu na mitandao ya kijamii kwa ujumla wake. Sote tunafahamu kuwa muheshimiwa Makonda ni mkuu wetu wa mkoa wa Dar es Salaam kabla ya kushika wadhifa huo alikuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni. Hivi karibuni yameibuka masuala mbalimbali yakimhusisha kiongozi huyu,
baadhi yake ni
1) Jina la Daudi Bashite
2) Kuhusishwa na Utajiri mkubwa wa kumiliki ghorofa na magari ya dhamani kubwa huko jijini Mwanza
3) Picha zake kuhusisha na matukio ya watoto mchele (mashoga) kutokana na mikao yake
4) Kuhusishwa kuwa kimapenzi na Agnes Gerald (Masogange) n.k
Ukitazama kwa haraka haraka hizi sekeseke zimeibuka soon baada ya kampeni mbalimbali za madawa ya kulevya na zile za mashoga kuanzishwa, hata tukikubali kuwa hizo tuhuma hapo juu kuwa ni za kweli
Je kwa nini hazikuzungumzwa mapema au ndio ile system ya niue nikuue (win win situation)? Awali nilifuatilia skendo zote zinazomlenga mkuu huyu kisha nikajaribu kuchambua na mienendo yake, ni kweli kuna mahala anapindisha sheria na kujivika madaraka yasiyo ya kwake ila penye ukweli tunapaswa kusema ukweli.
Mimi sio mnazi au ya kwamba nipo mrengo fulani wa siasa na nimewahi kusema hapo awali mimi sitetei mtu sababu ya uchama wake ila sababu ya misimamo yake katika nafasi aliyo nayo.
Sote tumeshuhudia watu walivyopukutika na madawa ya kulevya, nina ushahidi wa baadhi ya watu ambao wameshakufa sababu ya kutumia madawa, ninawafahamu vijana ambao wamekuwa wezi na vibaka sababu ya kujipatia hela ya kuondoa arosto hii.
Nikikumbuka mwaka 2005 nikiwa kidato cha pili asubuhi ya saa 12 nikielekea shule mjini tukiwa maeneo ya Kagera kwenye kigari cha kipanya akaja teja mmoja akamkwapua mama wa watu mkoba wake na kutokomea gizani, mama wa watu akielekea kazini akawa ameshamlostisha.
Ni wangapi tunaowafahamu wameshatiwa hasara ya kuibiwa vitu vyao sababu ya watumiaji hawa wa madawa ya kulevya ambao wanaishia kuwatajirisha hao mapapaa ambao huishia kumwaga mapesa jukwaani huko klabu kama mtu anayemwaga maji?
hebu tusiibue mambo mengine ya vyeti ili kujipooza na kutokomeza swala hili la mapambano dhidi ya madawa ya kulevya, and by the way uongozi ni kipawa na sio elimu ya darasani. ni Maprofesa wangapi ambao wanaweza kuwepo katika uongozi lakini wakawa viongozi wabovu?
Elimu inakupa mwanga zaidi wa kufanya maamuzi mazuri na sio kuwa ndio kigezo cha mtu kuwa kiongozi akiwa na elimu kubwa. Wapo watu fuata upepo daily wanashinda mitandaoni wakiponda elimu ya Makonda lakini watu hawa wapo katika makundi kadhaa
1) Hawana kazi ya kufanya hivyo kushinda mitandaoni na kubishana elimu ya mtu ambaye hata ufanyeje huwezi kuifikia nafasi hiyo kwa kupoteza muda wako bure.
2) Kutokana na wauza madawa kudorora kiuchumi hivyo wameanzisha kampeni ya kumchafua kiongozi huyu ili kuwasahaulisha wananchi kuwa janga la madawa ni kubwa sana nchini
3) Vijana wanalipwa ama wamenunuliwa kifikra maana ni bora kununuliwa kimwili kuliko kununuliwa kiakili, hivyo wanunuliwa hawa wamejikuta wanaibua mambo mbalimbali ili kudhoofisha nguvu ya mapambano haya.
Kuna mambo mengi sana inatupasa kuyatilia mkazo na sio kuanza kuhoji elimu ya mtu katika mambo ya msingi, okay hata kama yeye ni Daudi Bashite iwapo alirudia mtihani kwa jina lingine kisha akafaulu na kusonga mbele wewe unalifahamu hilo au unafuata upepo tu?
Kwani hatuwafahamu watu ambao walifeli kidato cha nne au shule ya msingi wakarudia kwa jina la mtu mwingine ambaye ama alishafariki au alikimbia shule na mwanafunzi huyu akafaulu na kusonga mbele? Nyie kweli sio wafuatiliaji wa mambo, kwani hamumfahamu yule profesa mwenye dhamana ambaye alirudia shule ya msingi mara tatu kwa majina tofauti tofauti lakini hivi leo ndio amekuwa profesa tena mwenye dhamana?
Acheni ushabiki usio na tija na badala yake muda unaoutumia kubwata mambo ya watu wewe fanya kazi utaona matunda yake, Kwa hili mimi ninampongeza muheshimiwa Makonda ila na yeye akikosea basi asinichukulie hatua pale ambapo nitaamua kumponda pia maana mimi sio mnazi na wala sinunuliki!!
Niwatakie maandalizi mema ya sabato na Ijumaa kareem ndugu zagu...!!!
Mtenga Gerald
24/02/2017