Kashfa ya Upangaji Matokeo ya ligi ya Italy Vs Kashfa ya Upangaji Matokeo ligi daraja la kwanza Tanzania

Dkileo

Member
May 23, 2017
51
125
THE CALCIOPOLI SCANDALNipo na jaribu kuisoma kwa mara nyingine hii kashfa ya upangaji wa matokeo pale Italy..Najikumbusha kwa umakini mkubwa mno..Najikumbusha huku nikiliangalia hili jina la huyu jamaa anaitwa Luciano Moggi..
Wakati nazidi kuisoma hii kashfa iliyotokea ndani ya soka la Italy napata wasaa wa kukumbuka moja ya kashfa za upangaji wa matokeo iliyotokea hapa bongo katika ligi daraja la kwanza..Nakumbuka Geita Gold (Geita), JKT Oljoro (Arusha) na Polisi Tabora (Tabora) zilihusika

Ukiangalia wakina Luciano Moggi walitumia sim cards za Uswizi,Slovenia na baadhi ya namba zilisajiwa Liechtenstein ..Unaweza kuona jinsi ambayo walikuwa wajanja..Walikuwa wanazitoa zile laini baada ya maongezi yao..Walikuwa wajanja sana..Pia hata katika upangaji kulikuwa na umakini sana..Kwa mfano katika mechi kati ya udinese vs bologna luciano moggi alituhumiwa kwa kuwalazimisha waamuzi wawape kadi za njano baadhi ya wachezaji wa Udinese ambao walikuwa na kadi za njano za michezo iliyopita ili waweze kukosa mchezo unaofuata kati ya Juventus na Udinese …Hiyo ni moja kati ya tuhuma nyingi za Luciano moggi katika kashfa hii.

Ni hapa ambapo katika kashfa ya Calciopoli watu walienda jela,adhabu ya faini,adhabu ya kutoshiriki katika jambo lolote lililohusu mpira wa miguu kwa muda Fulani na wengine walifungiwa maisha kujihusisha na mpira wa miguu..Juventus walishushwa daraja na kunyang’anywa ubingwa..Ac Milan waliporwa points..

Najaribu kulinganisha na hii tuhuma ya hapa kwetu..Ambapo nakumbuka kuna timu ambayo katika hatua za mechi za mwanzo haikuweza kufunga walau goli 4 katika mechi moja …Lakini katiika mechi husika magoli yalikuwa kama maji..Nakumbuka kuna baadhi ya watu walilalamika kuwa wakati goli likiingia kwenye mechi ya huku basi simu inapigwa kwenye mechi ya kule ili nako goli liweze kuingia...
Nakumbuka hata zile hukumu zilizotolewa na TFF zilikuwa na utata utata..

Bado nawaza kama Calciopoli ingefanyika Tanzania..Sijui kama ingeweza kugundulika..Kama tu tukio kama hilo la ligi daraja la kwanza lilikuwa na dosari je hili lingeweza kuchukuliwa hatua zilizo sahihi???
Kuna mwandishi mmoja wa Makala za michezo hapa Tanzania aliandika jambo moja kuhusu raisi wa TFF aliyepita..Ambapo aliandika kuhusu ukabila ndani ya TFF..Leo hii rais yupo rumande..

Kuna mtu juzi baada ya kuondolewa Kilimanjaro stars alinifuata inbox na kuniambia kwanini sizungumzii matokeo ya Kilimanjaro stars..nikamjibu kuwa mimi si shabiki wa soka la Tanzania…
Tunakosea katika maeneo mengi sana katika soka letu…Ila eneo la uongozi ni nyeti sana na ndipo ambapo tunakosea sana..Nakumbuka katika uchaguzi uliopita wa TFF kuna mgombea mmoja mtu wa michezo na mchezaji wa zamani wa Tanzania alipewa chapuo la kuweza kushinda uraisi TFF..Lakini wajumbe wa TFF tayari walikuwa na mtu wao waliye muhitaji…

Wacha niendelee kuwa shabiki wa soka la watu wenye akili ya soka…Nipo tayari kupokea lawama za kuwa si mzalendo lakini siwezi acha kushabikia soka la walio endelea..Naamini mpaka tutakapo kuja kuzinduka na kufahamu ni wapi tunakosea na ni maeneo gani turekebishe itakuwa baada ya miaka mingi…Haswa kuweza kufikia ndoto yetu ya walau kuweza kucheza fainali za world cup..
 
Dkileo

Member
May 23, 2017
51
125
THE CALCIOPOLI SCANDAL

Nipo na jaribu kuisoma kwa mara nyingine hii kashfa ya upangaji wa matokeo pale Italy..Najikumbusha kwa umakini mkubwa mno..Najikumbusha huku nikiliangalia hili jina la huyu jamaa anaitwa Luciano Moggi..

Wakati nazidi kuisoma hii kashfa iliyotokea ndani ya soka la Italy napata wasaa wa kukumbuka moja ya kashfa za upangaji wa matokeo iliyotokea hapa bongo katika ligi daraja la kwanza..Nakumbuka Geita Gold (Geita), JKT Oljoro (Arusha) na Polisi Tabora (Tabora) zilihusika

Ukiangalia wakina Luciano Moggi walitumia sim cards za Uswizi,Slovenia na baadhi ya namba zilisajiwa Liechtenstein ..Unaweza kuona jinsi ambayo walikuwa wajanja..Walikuwa wanazitoa zile laini baada ya maongezi yao..Walikuwa wajanja sana..Pia hata katika upangaji kulikuwa na umakini sana..Kwa mfano katika mechi kati ya udinese vs bologna luciano moggi alituhumiwa kwa kuwalazimisha waamuzi wawape kadi za njano baadhi ya wachezaji wa Udinese ambao walikuwa na kadi za njano za michezo iliyopita ili waweze kukosa mchezo unaofuata kati ya Juventus na Udinese …Hiyo ni moja kati ya tuhuma nyingi za Luciano moggi katika kashfa hii.

Ni hapa ambapo katika kashfa ya Calciopoli watu walienda jela,adhabu ya faini,adhabu ya kutoshiriki katika jambo lolote lililohusu mpira wa miguu kwa muda Fulani na wengine walifungiwa maisha kujihusisha na mpira wa miguu..Juventus walishushwa daraja na kunyang’anywa ubingwa..Ac Milan waliporwa points..Najaribu kulinganisha na hii tuhuma ya hapa kwetu..Ambapo nakumbuka kuna timu ambayo katika hatua za mechi za mwanzo haikuweza kufunga walau goli 4 katika mechi moja …Lakini katiika mechi husika magoli yalikuwa kama maji..Nakumbuka kuna baadhi ya watu walilalamika kuwa wakati goli likiingia kwenye mechi ya huku basi simu inapigwa kwenye mechi ya kule ili nako goli liweze kuingia...

Gezuz

JF-Expert Member
Dec 17, 2016
1,009
2,000

Bongo bahati mbaya mkuu
 
DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
10,703
2,000
Ukweli ni lazma usemwe.
Hyo ya Italy kupanga matokeo IPO mpk leo.

Sema serikali ya sasa ya Italy imekaa kihuni na legelege sana.

Betting nchini Italy imeshika sana kasi.

Mwaka jana tu wameonywa na FIFA mara 2 kuhusiana na hilohilo swala LA match fixing.

Uefa nao walichachamaa sana kwa tuhuma za shirikisho LA soka Italy.

Walkua wana kula bingo na matajiri.

Matajiri hawa walkua wakihonga sana marefa na wachezaji.

Pia walkua wanaotaka baadhi ya timu zifanyiwe figisu kwny mechi za mwisho mwisho wa last season ili ziweze kushika nafasi za juu kwny msimamo kuweza kushiriki Uefa.

Kelele zilipokua nyingi serikali ikaingilia kati na kuanza kuwalipa mishahara marefa badala ya posho peke yake kwa kushirikiana na shirikisho.

Pia serikali ikapitisha mswada wa kuwa na kima cha chini cha mishahara ya wachezaji wa ligi mbali mbali ndani ya Italy.

MWAKA JANA HALI ILKUA MBAYA SANA HASA KWA WAZEE WA MIKEKA.

Timu za Italy zlkua znachana mikeka sana sababu ya upangaji wa matokeo.
 
kidunula1

JF-Expert Member
Apr 2, 2016
4,883
2,000
Achaneni na soka la bongo, si mliwaona walivyorudi juzi kama vibaka fulani wengine na vichupi na kocha wao mpumbavu sijui katokea wapi. Vilabu vyenyewe haijulikani vinajiendeshaje, Mungu saidia tu.
 
Attachments

  • File size
    8.9 MB
    Views
    23

Dkileo

Member
May 23, 2017
51
125
Achaneni na soka la bongo, si mliwaona walivyorudi juzi kama vibaka fulani wengine na vichupi na kocha wao mpumbavu sijui katokea wapi. Vilabu vyenyewe haijulikani vinajiendeshaje, Mungu saidia tu.
tumesha achana nalo mkuu ...ila tutabaki kuwa mashabiki wa samatta,ulimwengu ,msuva,abdi banda,farid mussa na watanzania wengine wanaocheza nje ya nchi
 
Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
5,956
2,000
Vilabu vikubwa barani ulaya vingi vina fitna ya soka. Juventus Turin ndio baba wa fitna barani ulaya. Kina Luciono Moggi na yule bwana aliyefungiwa maisha kule ufaransa asijishughulishe na maswala ya soko bwana Bernard Tappie wao ndio baba wa wafitna.

Hii iliyofanyika hapa bongo sio fitna au mech fixing kama unavyojaribu kufikiri. Walichokifanya ni utoto ulioambatana na ujuha na ujinga ndani yake. Unakumbuka kule nigeria kuna timu zilifungana mpaka goli 32!
Bongo hamna fitna kuna ujuha.
 
Dkileo

Member
May 23, 2017
51
125
hahahaaa mkuu hawa jamaa wa kwetu hapa huwa wanatuona sisi mashabiki kama wajinga..ni bora tubaki kushabikia soka la ulaya tuu
 
dos.2020

JF-Expert Member
Feb 17, 2009
3,582
2,000
Roberto Baggio wakati alipokua akiwika miaka ya 80 mwishoni wakati akiwa na Fiorentina. Vilabu vote vikubwa vilikua vikimuwania. Kwa wakati huo Ac milan, Inter Milan, Napoli, Juventus zilikua ndio team kubwa barani ulaya. Seria A ilikua onform hakua PL wala Laliga.
Ac milan na Inter milan zilitoa dau kubwa pamoja kuahidi mshahara mkubwa zaidi. na pia ki form kwa wakati huo Milan na Inter walikua ahead of Juventus. Hafla tu siku watu wameamka wanasikia Baggio amesajili Juventus. Lilikuo ni gimzo zito.
kwasasa kama vile mchezaji wakiwango cha juu awaniwe na Real Madrid na Barcalona alafu usike Atletico Madrid Ndo waibuke kidedea.

Inavosemekana Moggi alito offer kwa fiorentina ambayo Haikuweza kukataliwa. KWA wale wapenzi na wanaouelewa Godfather films nahisi tayari watafahamu.
 
kidunula1

JF-Expert Member
Apr 2, 2016
4,883
2,000
tumesha achana nalo mkuu ...ila tutabaki kuwa mashabiki wa samatta,ulimwengu ,msuva,abdi banda,farid mussa na watanzania wengine wanaocheza nje ya nchi
Sawa ndugu, hao kweli hatuna budi kuwasapoti!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom