THE CALCIOPOLI SCANDAL
Nipo na jaribu kuisoma kwa mara nyingine hii kashfa ya upangaji wa matokeo pale Italy..Najikumbusha kwa umakini mkubwa mno..Najikumbusha huku nikiliangalia hili jina la huyu jamaa anaitwa Luciano Moggi..
Wakati nazidi kuisoma hii kashfa iliyotokea ndani ya soka la Italy napata wasaa wa kukumbuka moja ya kashfa za upangaji wa matokeo iliyotokea hapa bongo katika ligi daraja la kwanza..Nakumbuka Geita Gold (Geita), JKT Oljoro (Arusha) na Polisi Tabora (Tabora) zilihusika
Ukiangalia wakina Luciano Moggi walitumia sim cards za Uswizi,Slovenia na baadhi ya namba zilisajiwa Liechtenstein ..Unaweza kuona jinsi ambayo walikuwa wajanja..Walikuwa wanazitoa zile laini baada ya maongezi yao..Walikuwa wajanja sana..Pia hata katika upangaji kulikuwa na umakini sana..Kwa mfano katika mechi kati ya udinese vs bologna luciano moggi alituhumiwa kwa kuwalazimisha waamuzi wawape kadi za njano baadhi ya wachezaji wa Udinese ambao walikuwa na kadi za njano za michezo iliyopita ili waweze kukosa mchezo unaofuata kati ya Juventus na Udinese …Hiyo ni moja kati ya tuhuma nyingi za Luciano moggi katika kashfa hii.
Ni hapa ambapo katika kashfa ya Calciopoli watu walienda jela,adhabu ya faini,adhabu ya kutoshiriki katika jambo lolote lililohusu mpira wa miguu kwa muda Fulani na wengine walifungiwa maisha kujihusisha na mpira wa miguu..Juventus walishushwa daraja na kunyang’anywa ubingwa..Ac Milan waliporwa points..
Najaribu kulinganisha na hii tuhuma ya hapa kwetu..Ambapo nakumbuka kuna timu ambayo katika hatua za mechi za mwanzo haikuweza kufunga walau goli 4 katika mechi moja …Lakini katiika mechi husika magoli yalikuwa kama maji..Nakumbuka kuna baadhi ya watu walilalamika kuwa wakati goli likiingia kwenye mechi ya huku basi simu inapigwa kwenye mechi ya kule ili nako goli liweze kuingia...
Nakumbuka hata zile hukumu zilizotolewa na TFF zilikuwa na utata utata..
Bado nawaza kama Calciopoli ingefanyika Tanzania..Sijui kama ingeweza kugundulika..Kama tu tukio kama hilo la ligi daraja la kwanza lilikuwa na dosari je hili lingeweza kuchukuliwa hatua zilizo sahihi???
Kuna mwandishi mmoja wa Makala za michezo hapa Tanzania aliandika jambo moja kuhusu raisi wa TFF aliyepita..Ambapo aliandika kuhusu ukabila ndani ya TFF..Leo hii rais yupo rumande..
Kuna mtu juzi baada ya kuondolewa Kilimanjaro stars alinifuata inbox na kuniambia kwanini sizungumzii matokeo ya Kilimanjaro stars..nikamjibu kuwa mimi si shabiki wa soka la Tanzania…
Tunakosea katika maeneo mengi sana katika soka letu…Ila eneo la uongozi ni nyeti sana na ndipo ambapo tunakosea sana..Nakumbuka katika uchaguzi uliopita wa TFF kuna mgombea mmoja mtu wa michezo na mchezaji wa zamani wa Tanzania alipewa chapuo la kuweza kushinda uraisi TFF..Lakini wajumbe wa TFF tayari walikuwa na mtu wao waliye muhitaji…
Wacha niendelee kuwa shabiki wa soka la watu wenye akili ya soka…Nipo tayari kupokea lawama za kuwa si mzalendo lakini siwezi acha kushabikia soka la walio endelea..Naamini mpaka tutakapo kuja kuzinduka na kufahamu ni wapi tunakosea na ni maeneo gani turekebishe itakuwa baada ya miaka mingi…Haswa kuweza kufikia ndoto yetu ya walau kuweza kucheza fainali za world cup..