Kabla huja-comment jipe mda kidogo wa ku-search taarifa usiyoielewa. Ni rahisi tu, just google it.Kuna shirika linaloitwa International Organization for Migration? Never heard it before!
NInachofahamu mimi kuna shirika linaloitwa United Nations High Commissioner for Refugees (UNHCR).
I stand to corrected.
Lipo mkuu...Kuna shirika linaloitwa International Organization for Migration? Never heard it before!
NInachofahamu mimi kuna shirika linaloitwa United Nations High Commissioner for Refugees (UNHCR).
I stand to corrected.
Chanzo chichi si ndo kile kilituambia kuwa lowasa hasafishiki, baadae akageuka mfalme wa chanzo hchihichi?Hiko chanzo chako cha habari nimepoteza imani nacho.
Pole kwa uelewa wako mdogo wa mambo ya kimataifa! Una umri gani mkuu? Yaani hujawahi kulisikia shirika linaitwa IOM? Hili mkuu linahusika na wahamiaji wa aina zote, wakati UNHCR linahusika na wakimbizi tu! Ila kuna issues wanashirikiana kwa ukaribu sana hasa linapokuja swala la kuwatafutia wakimbizi makazi ya kudumu nchi za Ulaya. Mfano kuna wakimbizi kutoka DRC, Burundi huwa wanatafutiwa makazi ya kudumu USA, Canada, Uswiss n.k.Kuna shirika linaloitwa International Organization for Migration? Never heard it before!
NInachofahamu mimi kuna shirika linaloitwa United Nations High Commissioner for Refugees (UNHCR).
I stand to corrected.
Kwa asilimia 100 hii ni kweli, na jamaa wa GSM kaweka wengi sana mifukuni kwake hadi ma-R. wapo.
Mwonee Huruma. Yeye kasoma kichwa cha habari na kukurupuka kupost. Contents hazijui. Mvivu huyo. Aibu kwakeUnaangalia chanzo au content?? Kama wahusika wamepiogiwa simu na wamekiri kufahamu suala hilo wewe unakosaje imani?
Hayo mashirika yote yapo,kuna la wahamiaji na la wakimbiziKuna shirika linaloitwa International Organization for Migration? Never heard it before!
NInachofahamu mimi kuna shirika linaloitwa United Nations High Commissioner for Refugees (UNHCR).
I stand to corrected.
International organization for migration lipo mkuuKuna shirika linaloitwa International Organization for Migration? Never heard it before!
NInachofahamu mimi kuna shirika linaloitwa United Nations High Commissioner for Refugees (UNHCR).
I stand to corrected.
Ameeeen.Huyo mlalamikaji kama bado yuko hai mpaka muda huu basi Mungu atukuzwe .
Lipo mkuu ....kwa sisi tunao Fanya kazi mipakani tuna shinda nao hao.Kuna shirika linaloitwa International Organization for Migration? Never heard it before!
NInachofahamu mimi kuna shirika linaloitwa United Nations High Commissioner for Refugees (UNHCR).
I stand to corrected.
Na sasa ndio limekwisha hivyo. Maelezo yenyewe hayashawishi ki hivyo. Mtu wa kujenga ghorofa anafugwa kama panzi hana kampuni ya ukandarasi hata makandarasi/ wahandisi wenzie wangemsaidia kulipwa. Milioni 250 si za kuzidai kitoto kitoto kama hivyo.Nsato Marijani, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Jeshi la Polisi pamoja na vigogo wengine wa serikalini wanatuhumiwa kushindwa kumsaidia Mtanzania Abdulswamadu Zacharia Omary (36) anayedai kutendewa vitendo vya kikatili.
Nsato Marijani, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Jeshi la Polisi. Picha ndogo, Ghalib Said Mohamed mmiliki wa kampuni ya GSM na Home Shopping Centre
Ukatili huo ni pamoja na kudhulumiwa mali na wafanyabiashara Said Sadi na Ghalib Said Mohamed.
Akisimulia mkasa huo huku akilia, kijana huyo anadai kufanyiwa vitendo vya kikatili ikiwemo kutaka kunyongwa ndani ya chumba cha mahabusu kilichopo Kituo cha Polisi Oystebay, kitendo anachosema kiliratibiwa na jeshi hilo kuwasaidia wafanyabiashara hao kupoteza ushahidi lakini amekuwa akilalamika bila kusaidiwa.
“Nimekuwa nikitumiwa na baadhi ya vigogo wa polisi wanajidai kutaka kunisaidia lakini wakifika kwa huyu jamaa wanakaa kimya, polisi wanashirikiana na huyu aliyekuwa mmiliki wa Home Shoping Centre (HSC), kutesa watu, na mimi wanakataa kunilipa milioni zaidi ya 250, nilizofanyia kazi nikiwa kwao Yemen,” anasema Omary.
Akisimulia mkasa wa tukio, Omary anasema alipewa zabuni ya kujenga jengo la ghorofa 3 nchini Yemen bila kupewa mkataba, akakataa lakini alinyang’anywa hati zake za kusafiria na kuteswa kikatili hali iliyopelekea akubali.
“Nilisaidiwa na watu wa shirika la kimataifa la wahamaji (International Organisation for Migration) kurudi Tanzania, lakini tangu nimerejea nchini, hawa jamaa wa iliyokuwa Home Shoping Centre na GSM wana nguvu serikalini hadi ndani ya vituo vya polisi,” anasimulia.
Katika barua yake ambayo amewaandikia viongozi kadhaa wa taasisi za serikali ambayo MwanaHALISI online imeiona Omary amesema, viongozi hao wamewekwa kwenye mfuko na wafanyabiashara hao, kiasi cha kuifanya serikali idharaulike.
“Unasikia, hili suala linajulikana pote polisi, afande Marijani analipotezea kwa muda mrefu, nilielekezwa kwa afande wa Interpol anaitwa Ngonyani.
“Pia Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa, (Takukuru) wanalifahamu lakini ndugu yangu kila aliyetaka kunisaidia huishia kukaa kimya, natamani sasa kumwona rais anisaidie,” anasisitiza.
Omary katika andishi lake ametaja hata viongozi wa dini ambao wamekuwa wakijipatia fedha kutokana na tatizo lake ambalo polisi wameshindwa kulifanyia kazi.
Ninatishwa, ninaambiwa hawawezi kufanywa lolote ndani ya nchi hii, wakisikia nimelalamika kwenye ofisi yeyote ya serikali hata polisi hunijibu “wewe unapolalamika unaenda kwao, sisi tunawaita wanakuja tulipo, unajihangaisha.”
Anadai tarehe 23 Julai 2015 alitekwa na Gharib Said Mohamed pamoja na Faisal kisha kupelekwa Masaki na kwamba, alipigwa na akawa hajitambua.
“Nilipojitambua nilijikuta Kituo cha Oysterbay nimefunguliwa mashtaka likiwemo la kumtukana rais, kutaka kulipua Ikulu, kukutwa na silala na niliwekwa rumande siku 46 bila kufikishwa mahakamani na namba ya jalada ilikuwa OB/IR/6365/2015, na OB/IR/11770/2015.
Nilipofikishwa mahakamani nilikuta mashtaka tofauti ambayo yalifutiliwa mbali na hakimu sababu hayakuwa ya kweli.
MwanaHALISI Online, limewasiliana na afande Lucy Ngonyani, aliyeshughulikia suala hilo na kukiri kuwa, analifahamu, yupo likizo na yeye sio msemaji wa jeshi hilo.
Alipoulizwa Nsato Marijani, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo alisema, “huyo kijana anapaswa afike ofisini kuniona, kama suala lake halijatekelezwa sio kuja huko kwa vyombo vya habari.”
Mtandao huu uliwatafuta watuhumiwa hao (Said Sadi na Gharib Sadi Mohamedi) kupitia simu zao za mkononi, pamoja na simu zao kuita kwa muda mrefu, hazikupokelewa.
Na hata walipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno kwenye simu zao, hawakujibu.
Chanzo: Mwanahalisi Online