IzukeneJr
JF-Expert Member
- Aug 4, 2012
- 758
- 753
Wakuu Salaam,
Sioni kama ni busara kutunishiana misuli na serikali yetu ilihali ndo kwanza hata mwaka wa uongozi wake haujaisha.
Ni kweli kwa maarifa yetu na akili zetu tunaweza kuona kwamba tunapokwenda hakuna tumaini, kwamba tunaenda gizani, tumeshasema na ameshasikia kwamba hatuna imani na anakotupeleka, kazi yetu imeisha.
Tumpe nafasi, maana kila kukicha anasema kwamba tumuamini na kumpa ushirikiano kutekeleza aliyoyaahidi, tumpeni nafasi. Haya mambo ya kutunishiana misuli yanatuondoa kwenye lengo. Badala ya Rais kupanga mikakati ya kutekeleza ahadi zake, tunamlazimisha aziache na kuanza kupanga mikakati ya kukabiliana na sisi. Tumpe nafasi.
Ikifika miaka mitano, tutarudi tumuulize, Umetufikisha wapi? Je ulipotuahidi kutufikisha ndo hapa? Then tutarud kwa wananchi tuwaambie, wataamua tena. Kwa wakati huu kama alivyosema, nadhan ni busara kumuacha afanye kazi yake. Kuna msemo wa kiswahili husema, "Miluzi mingi humpoteza mbwa" . Tumpeni nafasi kiongozi wetu atekeleze majukumu yake.