Kaseja alisababisha Yanga waingie mitini 2008

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
13,664
2,000
July 27, 2008, timu ya Yanga iliingia mitini kwa kutoileta timu uwanjani kucheza na Simba katika mchezo wa kugombea nafasi ya tatu wa masindano ya CECAFA Challenge Cup. Sababu iliyotolewa na Yanga ni kwamba walikuwa wanaidai CECAFA hela za ubingwa walioupata miaka kadhaa iliyopita.

Hata hivyo, baada ya uchunguzi siku kadhaa baadaye, ilikuja kujulikana kwamba sababu hasa iliyofanya Yanga kuingia mitini ni kukosa mtu wa kukaa golini, yaani golikipa. Yanga ilikuwa na makipa watatu, Ivo, Kaseja na mwingine hajulikani. Ivo Mapunda aliumia mechi ya nyuma, so akawa ni majeruhi. Kaseja akaasema kwamba hatadaka katika mechi itakayokuwakutanisha wao Yanga na timu yake aliyotoka kuihama wakati huo, yaani Simba. Yanga wakawa hawana imani na golikipa namba tatu ambaye hata hajawahi kudaka katika mechi za ligi. Ndipo wakaona isije ikawa fedheha, wakatafuta sababu na wakakumbuka deni wanaloidai CECAFA. Wakatoka na sababu hiyo, lakini ukweli ni kwamba kipa bora aliyekuwa fit kwa mchezo huo, Kaseja, alikataa kukaa langoni. Kazi kwenu Yanga, mmemsajili tena, mtumieni mechi zote tu, hata za watani wa jadi!
 

kovai tamil taiga

JF-Expert Member
Sep 28, 2013
617
1,000
Majangaa!!! ukuta wa yanga sawa sawa na 'cheke cheke'!! Yaani unavuja tu.unachotakiwa ni kuongeza pressure kidoooogo!Bhaaasi!watakuwa wanaokota tu kunyavu!!Hawana ujasiri tena kutamba mbele ya Simba kwa majina haya Bartez,Kaseja!!
 

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,144
2,000
Kaseja wakati wa segemnenge la kumuacha alitanabaisha kwamba yeye ni SIMBA DAMU
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom