Salamander
JF-Expert Member
- Dec 7, 2012
- 28,536
- 15,751
Klabu ya Yanga imetangaza rasmi kuachana na Golikipa wake Juma Kaseja kuanzia leo baada ya kuwepo kwa hali ya kutoelewana baina ya kipa huyo na uongozi wa klabu.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Jerry Muro amethibitisha taarifa hizo na kusema kuwa Juma Kaseja alivunja masharti ya mkataba huo kwa kutohudhuria mazoezini na kuongeza kuwa Jumamwenyewe alishaonesha nia ya kuondoka klabuni hapo hivyo ni bora klabu hiyo ikamuachia.
Muro amesema Yanga haijavunja mkataba na Kaseja bali imemuachia baada ya Kaseja mwenyewe kuvunja masharti ya mkataba kati yake na Yanga...
Baada ya kuachwa Yanga, unafikiri Kaseja atakwenda timu gani?
Habari imetoka: East Africa Television (EATV)
Mimi ninawaza tu: Kwanini hawakumuacha December 2014 kabla usajili wa dirisha dogo kufungwa ? Au hawajui soka ndio kibarua chake!